Gamba la ccm limeishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gamba la ccm limeishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by iron finger, Mar 13, 2012.

 1. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  GAMBA LA CCM LIMEOTA SUGU?zilikuja kelele nyingi sana maamuzi ya kamati kuu ya CCM yalitamka chama hakina budi kurudishwa katika misingi na sifa zake,tamko likaonyesha chama kinahitaji kuzaliwa upya sio kwa staili ya kama mwanadamu yani kutokea tumboni kwa mama hapana wao CCM wakaenda mbali zaidi na kwa ukongwe wao wakaona bora wamuige nyoka,tabia ya nyoka anapozeeka hujirudisha ujana kwa kujivua ngozi yake ya zamani na kujivika mpya hivyo Chama cha Mapinduzi kikatumia stayle hiyo lakini kwa njia isiyo sahihi role model wao Nyoka anajivua ngozi yote wao waloba step na kutafuta watu watatu na kuwavika ngozi zee ya nyoka hivyo wakataka wawavue gamba ili chama kizaliwe upya,lakini kwa uelewa wangu huwezi kumaliza tatizo kwa kupambana na sehemu ndogo ya tatizo dawa ya kumaliza tatizo ni kukata mzizi wa tatizo wao CCM hawajui kama Chama Chote kimevaa gamba kuanzia juu mpaka chini lote ni gamba,ni ulimbukeni kutaka kuchuna gamba la kiunoni na kuacha la robo tatu ya mwili kisha unaenda kwa watu na kutamba kwamba umezaliwa upya,umejivua gamba ni **** tu awazaye kufanya hivyo.Lakini hata iyo robo ya gamba imegoma mmoja aliita waandishi wa habari akang'aka na kudai falsafa ya chama kujivua gamba ni mpango wa siasa uchwara ndani ya chama zenye mlengo wa kuharibiana jina akadai yeye ni mtu mwenye heshima kubwa hivyo kumuita gamba ni kumharibia hadhi ya jina lake katika biashara zake,kuweka kumbukumbu sawa katika maandishi yake ya kuachia ngazi hakuna mahala popote aliposema anajiuzule kwa tuhuma za kuwa gamba.Na Chama kuonyesha unafiki katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Gamba 2 kikampigia magoti na kuomba sapoti yake kutetea kiti cha ubunge ni unafiki mkubwa.Lakini walioitwa magamba wengine wakakomaa na kusema kama wamemwag ugali tutamwaga mboga,kuonyesha ubabe mmoja wao akatamka kwa tambo kwamba Gamba limefika kiunoni kumaliza kulivua ni mbinde labda mvuaji aende na shoka,wakati hadithi ya kuvuana magamba mtuhumiwa mkuu akaibuka yeye hakuleta unafiki mbele ya kikao cha halmashauri kuu ya Chama Taifa akainuka alivua gamba kiujasiri,hakulivua kukubali kushindwa bali yeye aliwaonyesha watanzania kuwa gamba si lake bali mwenye nalo ni kiranja mkuu angalau yeye alifanikiwa kuzima moto wa kuvua sehemu ndogo ya gamba na kuwaonyesha watanzania ukweli kwamba CHAMA kizima ni gamba lahitaji kuvuliwa kukazania sehemu ndogo ya gamba ni kutaka kulaghai wananchi.Na kweli vita ya ugamba ipo kimya walioianzisha wamenywea sijui ni kwanini lakini binafsi nakubaliana nao ni heri wakae kimya kuliko kuendelea kutuaminisha ujinga kuwa ndani ya chama magamba ni watatu.Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani akaenda mbali hadi kusema kuwa nyoka hata umvue gamba bado atabaki na sumu ile ile kama ina madhara kwa binadamu itamduhuru tu,akasema zaidi kuwa sumu ya nyoka CCM imeenea hadi kwenye damu suluhu sio kumvua nyoka huyu CCM gamba suluhu ni kumuua ili tishio la mdudu huyu isiwadhuru watanzania.Sumu ya nyoka CCM ni ufisadi ni ukweli ulio wazi ndani ya Chama ufisadi sio mtu mmoja mmoja ni mfumo mzima nani anaweza kuwa msafi ndani ya mfumo huu? ,nani atayeweza kumtupia mwenzie jiwe?hakuna aliye msafi ndani ya CCM wa kuweza kumtoa kafara mwenzie na kumuita gamba wote ni wachafu ufisadi unawahusu niseme tena kuanzia juu mpaka chini.Ipo wapi Vita ya Kuvuana gamba au limeota Sugu?
   
 2. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gamba la kobe ni nyumba yake halivuki mpaka afie ndani yake = Chama Cha Magamba
   
 3. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  "gamba limeishia kiunoni" Andrew Chenge.
   
Loading...