Galila: Wagombea wanaokubalika na umoja ndani ya chama ndiyo siri ya ushindi

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu
Buguruni Dar es Salaam

Novemba 24, Mwaka huu nchi yetu itafanya uchaguzi wa serikali za mitaa. Uchaguzi huu ni muendelezo wa ugatuzi wa madaraka kwenda kwa wananchi.

Vyama vya siasa vimeendelea kujipanga na kujiimarisha kupitia vikao na mikutano yao ya ndani vikihimiza wanachama wake kujitokeza kujiandikisha ili waweze kushiriki uchaguzi huu pamoja na kuchukua fomu kuviwakilisha.

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ameshiriki Buguruni ya kijani ambapo amefungua mashina matatu ya wakereketwa wa CCM na kuzungumza na wanachama wa chama hicho.

Katika hotuba yake Ndugu Galila amewataka wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kujitokeza kuomba nafasi mbalimbali zinazowaniwa kwa wenye sifa.

"CCM ni yetu sote, tusiwafanyie fitna wenzetu wanaotaraji kuonesha nia ya kugombea katika uchaguzi huu, viongozi na kamati za siasa ziache wanachama wachague mtu wanayeona anatosha kukiwakilisha chama chetu. Tuachane na ubabe, tuheshimu uamuzi wa wengi, kanuni na taratibu za CCM."

Aliendelea kuhimiza "CCM itashinda ikiwa tutawapata wagombea wenye sifa na kuondokana na makundi yatakayokiumiza chama chetu. Tuwapelekee wananchi wagombea wanaokubalika na tuhimize umoja ndani ya chama kwani hiyo ndio nguvu yetu ya kushinda."

Katika mkutano huu wa ndani Ndugu Galila aliwataka wanaccm na wananchi kwa ujumla kutumia uchaguzi huu wa serikali za mitaa kuwaadhibu wote wanaopinga jitihada za serikali ya CCM ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kutowachagua wagombea wao.

"Ili kuonesha tunakubaliana na kazi nzuri inayofanywa serikali chini ya Rais Magufuli, tukawachague wagombea wa CCM katika uchaguzi huu." Alisema Galila.


Ndugu Galila alisema wapo wanasiasa na baadhi ya NGO ambao kazi yao ni kuishambulia serikali yetu hususani Mhe Rais Dkt Magufuli kama vile hakuna kazi anayoifanya watanzania wote mfahamu hawa wanawaridhisha waliowapa mafunzo na kuwafadhili ili ufadhili uendelee lakini kiuhalisia wanajua kuwa kazi inafanyika.

"Wapo watanzania wenzetu wanayaaminisha mataifa ya nje kuwa serikali yetu inakiuka haki za binadamu, inabana demokrasia, ni katili nk kumbe wapo katika utafutaji wa riziki. Tuwapuuze."

Mwisho, Galila amewahakikishia wanaccm na wananchi kuwa CCM ipo imara katika kuisimamia serikali na kuendelea kuiongoza nchi yetu hivyo ushindi mnono unakuja katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa.
 
Back
Top Bottom