ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Habari za Wiki Kwa Ufupi
Karibuni katika ukurasa mpya wa Gajetek Wiki, ukurasa ambao utakuwa unawaletea habari za wiki kuhusu gajeti na teknolojia kwa ufupi, habari ambazo hazikuzungumziwa katika makala zetu za kawaida, na baadhi zitakuwa ni muendelezo wa habari ambazo tumeshazizungumzia. Tunatarajia Gajetek Wiki itawasaidia wasomaji wetu kuelimika na kuhabarika zaidi katika masuala ya teknolojia na gajeti mbali mbali ulimwenguni. Ukurasa huu utakuwa unapatikana kwenye kurasa maalum itakayokulikana kamaGAJETEK WIKI
Facebook wametangaza rasmi Koti la Android waliloliita "Home", koti ambalo linamfanya mtumiaji aweze kuwa karibu zaidi na yanayojiri katika kurasa yake ya Facebook. Facebook wameshirikiana na HTC kutoa simu ya kwanza ikiwa na koti hilo katika OS ya Android toleo la Jelly Bean. Simu hiyo inatarajiwa kuanza kuuzwa mwezi huu. Uzuri wake ni kwamba ikiwa mtumiaji hatalipenda koti hilo ataweza kulivua na kutumia koti jengine lolote ambalo linapatikana kwenye Play Market.
Watumiaji wa simu nyingine za Android wataweza kulivisha koti hilo kwenye simu zao kwa kupakua kutoka kwenye Play Market. Kutokana na umaarufu na ukubwa wa Facebook; inatarajiwa kwamba huenda koti la Home likaifanya biashara hii iwe kubwa na muhimu kwani litawaamsha wengi kuanza kutumia sio tu home, bali makoti mbali mbali. Facebook ina watumiaji bilioni moja, ambapo kama Facebook ingekuwa ni nchi ingelikuwa ni ya tatu kwa idadi kubwa ya watu ulimwenguni baada ya China (Blioni 1.2) na India (bilioni 1.1)
Baada ya kukanusha shutuma za ubaguzi katika udhamini wa bidhaa (warranty), shirika la habari la Reuters limemkariri Afisa Mtendaji Mkuu wa Apple Tim Cook akiomba radhi kwa wateja wa China, nchi yenye soko la pili kwa ukubwa kwa bidhaa za kampuni hiyo. Cook katika taarifa hiyo amenukuliwa akisema "tunafahamu kuwa mawasiliano yetu katika soko hili si mazuri, wengine wanadhani kuwa Apple ina kiburi na haijali maoni ya wateja, lakini hii sio hali"Katika mtandao rasmi wa Apple nchini China, Cook amenukuliwa akisema "Tunaomba radhi kwa dhati kabisa kwa wateja ambao kumekuwepo kutokuelewa mambo au kuwasababishia matatizo yoyote"
Katika taarifa nyingine ya Reuters imeelezewa kuwa msamaha huo wa Apple umepokelewa vizuri kwenye vyombo vya habari vya China na hata miongoni mwa wateja. Katika makala hiyo ya Reuters ambapo imepewa kichwa cha habari "Apple iliyoomba msamaha yapata heshima" imeelezwa kwamba Apple imejitoa kwenye kuonekana msaliti na sasa kutukuzwa na vyombo vya habari vya China. Vyombo vya habari hivyo vilionogozwa na shirika la habari la taifa la China CCTV katika kuishutumu sera ya kibaguzi ya Apple kwa wateja katika udhamini (warranty)
Makala inayohusiana: Apple Yashutumiwa na CCTV Undumi la Kuwili
Mauzo ya Simu (Smartphone) kwa OS
Mauzo ya Smartphone ni uwanja wenye ushindani mkubwa huku OS nne zikiwa wakuu ni washiriki, Android ya Google inaendelea kuongoza ikifuatiwa kwa ukaribu na iOS ya Apple, ltaarifa hizi mpya zinaonyesha kwamba Windows Phone kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu, taarifa hii ni pigo kubwa kwa kampuni ya Blackberry ambayo inashindana na Microsoft katika kuipata nafasi hiyo. Tarifa hizi zimeripotiwa na kampuni ya uchambuzi wa takwimu ya Kantar.
Symbian inaendelea kukikaribia kifo chake baada ya kuwa ni OS inayopoteza hisa yake zaidi. Kampuni nyingine iliyopoteza hisa ambazo Windows Phone wamenufaika nazo ni Blackberry. Hali hii inazidi kuleta wasi wasi wasi kwa kampuni ya Blackberry ambayo imetupa shilingi yake ya mwisho kwa kutoa simu za Q10 na Z10 ambazo kuikoa kampuni hiyo kwa kuimarisha mauzo.
Makala inayohusiana: Blackberry Wabwaga Manyanga Kwenye BB Music
Chanzo: www.gajetek.com


