four eyes
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 905
- 1,406
Sio siri mimi ni msikilizaji mkubwa na wa kudumu wa Clouds Fm na hususan vipindi vya Power Breakfast, Jahazi na kile cha michezo. Ni mshabiki pia wa watangazaji kama Masoud Kipanya, Ephraim Kibonde na Gadner Habash.
Nimekuwa nikipenda utangazaji wa Gadner kitambo sana toka enzi zile anatangaza bongo fleva pale Clouds mpaka anakuja kwenye Afrika Bambataa na hatimaye Jahazi hivi sasa. Vipo vingi vinavyonivutia kwa Gadner ikiwamo sauti yake, ufundi wa matumizi ya lugha na umahiri wa utangazaj na mahojiano. Ni mtu ambaye Sina wasiwasi na intelligence yake na navutiwa pia na umahiri alionao katika kujibu anapofanyiwa mahojiano.
Pamoja na yote hayo huyu jamaa huwa ananistaajabisha kwa kauli ambazo wakati mwingine anazitoa redioni hadi nastuka na kuanza kufikiria huwa anavuta nini? Ana kawaida ya kutoa kauli zisizo na maadili akiwa anatangaza tena bila kujali. Mfano wa kauli ambazo nimewahi kuzisikia akizitamka akiwa redioni ni "Mtoto ana sauti tamu mpaka unaweza kulikuruza nyeto ukimsikiza", "inasemekana Dully alipigwa back na wanaume kadhaa", "nilikuwa nimeenda kukata gogo", pamoja na Ile aliyoitoa jukwaani akiwa MC "Sina maneno na yule binti nimeshamkojoza kwa miaka..."
Hayo ni machache kati ya mengi ya kustua ambayo nimewahi kuyasikia yakitamkwa na huyu bwana na kunishangaza inakuwaje mtangazaji mwandamizi kama huyu kutokuwa na stara ya maneno atamkayo redioni?
Karibuni Wadau mnaofahamu hulka hii ya Gadner mchangie.