Gaddafi: The end of a miserable despotic Tyrant!


Wewe umeongea la maana kama Great thinker. Nimeshangazwa sana hata Mzee Mwanakijiji kaingia kwenye mtego na propaganda za Mabeberu.
 
time to move on!

Sasa bado Bashir al Asad, na huyo wa Yemen sijui

control ya Mediterranean ni muhimu kwa NATO wajameni...so kama huwaungu mkono ndo imekula kwako.....
 

Hivi na wewe unaunga mkono uvamzi huu na kuua Viongozi wa Nchi nyingine??
Kwani hao wenzetu wa Magharibi ni mabaya mangapi wanayafanya??
"Think outside the Box" Grat thinker.

Mbona hawasogei hapo Somalia??????
 
Rip my dear comrade!! Kwangu mimi wewe ni shujaa!! Na umekufa kishujaa. Truly libyans wanatambua hilo. You know what comrade its a matter of time, they also gonna die . **** usa, uk , france and their allies.

Kutoka moyoni mwangu kifo cha Gaddafi kimeniuma sana....R.I.P Gaddafi
 
time to move on!

Sasa bado Bashir al Asad, na huyo wa Yemen sijui

control ya Mediterranean ni muhimu kwa NATO wajameni...so kama huwaungu mkono ndo imekula kwako.....

Kama mimi naona imekula kwangu! Ningewaunga mkono kama wangekuja na hapa kwetu
 
mimi binafsi siwezi kumhukumu gaddafi kwa aliyowafanyia watu wake, ila nafahamu kwamba alisimamia maslahi ya nchi yake hasa baada ya kutaifisha makampuni ya mafuta na serikali kumiliki vyanzo vyote vya utajiri huo, sio kama hapa bongo ambapo tunapata mrahaba wa asilimia 3,ukiangalia jinsi walivyomua napata picha kwamba waasi wale ni kama kundi la wahuni wasio na nidhamu waliopata msaada wa nato kushinda,utabiri wangu ni kwamba nchi ya libya itaishia kama iraq au somalia ie a failed state.
 
R.I.P Colonel Gaddafi., whoever celebrates his death ajakaa chini akatafakari ni mambo mangapi alisaidia walibya na Africa kwa ujumla.
 
Eti nato bombardment ya mashule, mahospitali, telecommunication centres, majumba na mauaji ya maelfu ya walibya kutoka angani , hayo si kitu bali kitu ni ghadafi kupambana na waasi wakishirikiana na alqaeda kupambana na serikali. Kweli kasumba ni kitu kibaya sana, tunakuwa kama parrots wa propaganda za west, watu hawafikirii nje ya wanacholishwa na obama na mama clinton, what a shame!. Rest in peace kamanda ghadafi!. Kamanda hakukimbia nchi amepigana mpaka mwisho kama alivyoahidi, huyu ndio mwanaume, shujaa wa ukweli!
 
Somoche punguza povu gadafi hakuwa kwenye mioyo ya wananchi wa libya maendeleo si vitu ni watu.

Kama sio vitu mbona mnapiga majungu kwamba dola imepanda na sukari bei ghali...akili iko wapi sasa?!! kaeni kimya mnyolewe sasa mlie vizuri MIAFRIKA ilishalaniwa na wazungu wanajua hilo ndio maana wanakuja wanaua tu wanaondoka...wewe nani kakwambia Waingereza wanamtaka Malikia!! tumia akili za kichwa..
 
Vibaraka utawajua tu

Unaomba visa kubaki zaidi USA nini?

Endelea kuwalamba miguu hao wazungu wako

Pathetic thread
 
Katika vita kati Tanzania na Uganda Libya ikiwa chini ya utawala Gaddafi ilitoa msaada wa kijeshi kwa nchi ya Uganda. Kutokana na msaada huo mamia ya watanzania waliokuwepo kwenye maeneo yalivamiwa na Uganda ( wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Idi Amin Dada) walipoteza uhai wao. Hivyo leo hii mtanzania ambae anasikitishwa na kifo cha Gaddafi hana moyo wa kizalendo. Au mnasemaje wanaJF kuhusu mtazamo wangu?
 

I'm glad you are aware of that!
 
nakubaliana na wewe kuhusu msaada aliopewa idd amin
lakini siwezi kufurahia kifo cha aibu namna ile,nataka ujue sababu za wazungu kumwondoa gaddafi kwa aibu
 
Qaddafi alimwamini Amin Dada cz at tht tym walihitajika viongozi wa aina ile! Alikuwa m2 thabiti kutetea haki na rasilimali za mwafrika hakuogopa ngozi nyeupe kama walivyo viongozi wetu wote wa Africa ambao hawana msaada wowote! limebaki jembe1 nalo ni Mugabe
 
Basi mimi hapa sijafurahishwa na kifo cha Gaddafi na usidhani kuwa watz wote wanachekelea wale watakuwa ni wale ambao hawajui kwanini libya ilivamiwa kama wewe, pitia maandiko na matamanio ya wazungu hasa marekani, vinginevyo si lazima kupost jf kitu ambacho hukijui.
 
Msaada sawa alioutoa huwezi jua maelewano kwa kipindi hicho yalikuwaje

llakini tofauti hizo kati ya libya na TZ hazikuwepo tena...kama binadam mwenye akili timamu huo sio uungwana

wangewaachia walibya wenyewe watafute suluhisho na si kumuua mwenzao kinyama hivo
 
Habari za uzalendo dunia ya leo? Unaonekana ume-stuck kwene group-think na meaningless mottos za 1950s mazee. Dunia ya sasa it's all about individualism.
 
Hayo yalishapita!! Mbona mkwerè amenda sana libya na kama kawaida kapiga naye picha kibao..kuonesha mambo yalikuwa fresh.
 
Nashukuru mlouona uwezo mdogo wa kuliona lile wengi wenye akili na busara wanalolaani kihalali. Ghadafi kumjpa msaada Idi amini ilikuwa uaminifu kwa mtu alomkiri kuwa kiboko ya wanyonyaji wa Afrika. Hata Mandela alisaidiwa sana na Ghadafi kwa misingi hiyo hiyo. Leo tulaani ukombozi wa wazalendo kusini kwa msaada wake? Wanaojua wasema hawajawaona Walibya wanafanya vibarua nchi nyingine kuboresha maisha yao. Watu hutoka nchi nyingi Africa na ulaya kwenda fanya kazi Libya waboreshe maisha yao. Walibya wasio na ajira walilipwa $1000 kwa mahitaji muhimu kwa mwezi. Huduma zote za jamii bure. Miji yote ilobomolewa na NATO yaonekana ilivyojengeka. Kifo cha Ghadafi ni pigo kubwa kwa Afrika na tutaona mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…