Wakuu,
Mimi nafikiri jibu zuri juu ya kashfa hii, kama ni kweli, ni lile alilotoa Rais Obama wa Marekani. Alipoulizwa, mbona wengi katika wale uliowateua wana kashfa za kodi na/au mambo mengine?
Akasema, "nikitafuta kuwateua wasiokuwa na kashfa ya aina yoyote, nitakuwa sina wa kumteua."
Kila mwanamume mwenye afya njema haachi kummezea mate mwanamke aliyekuwa halali yake. Kuwa alimwendea au hakumwendea haya ni msuala nyeti, si lazima wote wajue. Wanasema, "usilolijua ni usiku wa kiza."