Gadafi Maji ya SHINGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gadafi Maji ya SHINGO

Discussion in 'International Forum' started by AMARIDONG, Feb 23, 2011.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Kanali Muammar Gaddafi maji ya shingo Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 21:15 0diggsdigg

  Andrew Msechu na Mashirika ya Habari
  UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya, sasa ni vigumu kwake kuepuka kikombe walichonywea aliyekuwa Rais wa Tunisia, Zine Abedine Ben Ali pamoja na aliyekuwa Rais wa Misri, Hosni Mubarak ambao waliondoka madarakani kwa kulazimishwa na nguvu ya umma.Kama ilivyokuwa kwa Ben Ali na Mubarak, Serikali ya Kanali Gaddafi aliyeitawala Libya kwa miaka 41 sasa nafasi yake kuendelea kuiongoza Libya ni finyu, baada ya maandamano makubwa ya umma ambayo jana yaliingia siku ya sita huku yakiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na matokeo mabaya kwa mauaji makubwa yaliyotokea.

  Gaddafi, kiongozi ambaye amedumu madarakani kwa muda mrefu huenda kuliko viongozi wote barani Afrika huku akijipambanua kama 'Mfalme wa wafalme' wa Afrika na kutumia umaarufu wake kutaka kuleta Muungano wa Dola za Afrika (USA), wazo ambalo hata hivyo, halikutekelezeka ameitawala Libya tangu alipofanya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969.Gaddafi ameweka historia kwa majigambo na kutumia askari walinzi wa kike, kutotumia hoteli za kisasa kila anapokwenda safari nje ya nchi yake na kutumia mahema binafsi ya kifahari kama makazi awapo ugenini.

  Hata hivyo, hali halisi inaashiria kuwa sasa huenda ni zamu ya kiongozi huyo machachari kukumbwa na nguvu ya umma na kuachia madaraka.Jumuiya ya kimataifa pia imenyoosha mkono wake kuwaunga mkono waandamanaji nchini humo baada ya kutokea mauaji yanayofananishwa na 'mauaji ya halaiki', ambapo Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon amemkemea akimtaka kuacha mara moja mauaji.

  Kwa upande wake, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likikaa kikao cha dharura jana kwa ajili ya kumjadili Gaddafi.Katika taarifa yake, Ki-moon alisema kwamba alipata fursa ya kuzungumza na Gaddafi kwa muda wa zaidi ya dakika 40 juzi usiku na kumtaka aache mauaji dhidi ya waandamanaji hao wanaodai mabadiliko.“Nimemwelewesha na kumpa ushauri wa kina kwamba, haki za binadamu na uhuru wa kukusanyika na uhuru wa kujieleza ni lazima vilindwe kwa nguvu zote,” alisema Ki-moon katika taarifa yake.

  Taarifa rasmi zilizopatikana jana mchana zilieleza pia kwamba Umoja wa Nchi za Kiarabu (Arab League) umekutana mjini Cairo, Misri kujadili umwagaji damu unaoendelea nchini Libya.Hata hivyo, tayari Gaddafi ameanza kupata pigo baada ya baadhi ya washirika wake, akiwemo balozi wake mdogo katika Umoja wa Mataifa, Ibrahim Babbashi kutangaza kujizulu nyadhifa zao kutokana na mauaji ya zaidi ya watu 300 wanaoelezwa kupoteza maisha kwa kushambuliwa na askari watiifu kwa kiongozi huyo.
  Shirika la Kutetea Haki la Human Rights Watch (HRW), lilieleza kwamba waliouawa walifikia 233 jana asubuhi, lakini mashirika mengine ya habari yamekuwa yakieleza kwamba ni kati ya watu 300 hadi 400.

  Maofisa wengine wawakilishi wa Libya katika balozi nchini Australia, China, India na Malaysia, walitangaza kujitenga na Serikali ya Gaddafi wakieleza kwamba amepoteza uhalali wake mbele ya umma wa Libya. Naye Balozi wa Libya nchini India, Ali al-Essawi aliliambia Shirika la habari la Ufaransa AFP mjini New Delhi kwamba anajiuzulu kwa sababu ya mauaji makubwa ya raia wasiokuwa na hatia nchini mwake ikiwamo kwa kuwashambulia kwa kutumia ndege za kijeshi.

  Hata baada ya uvumi kwamba kiongozi huyo alikimbia katika mji wa Tripoli juzi usiku na kuelekea nchini Venezuela, Gaddafi alizungumza kupitia televisheni alfajiri ya jana akieleza kwamba taarifa hiyo ni ya uongo na yeye ndiye kiongozi mkuu wa taifa hilo.Kanali Gaddafi alitokeza kwa muda mfupi na kutumia sekunde chache katika televisheni ya taifa, ambayo ilisema alikuwa akizungumza nje ya nyumba yake mjini Tripoli.

  Alikanusha taarifa za kuondoka kwake na kuwataka wananchi wa Libya kuwapuuza watu wanaoeneza uvumi huo akiwaitaka kuwa ni 'mbwa' wasiostahili kuaminiwa.Uasi dhidi ya Gaddafi umefikia hata kwa askari wake wa kikosi cha anga, ambao walikataa amri ya kutii ya kuwataka kutumia ndege za kivita kushambulia waandamanaji na kuamua kukimbilia uhamishoni kujinusuru.

  Askari hao walikataa kuwa miongoni mwa wale waliotumika kuwashambulia raia wasiokuwa na silaha kwa kutumia ndege za kijeshi, vifaru na magari ya kivita na kuchukua mwelekeo wa kuwaunga mkono waandamanaji wanaotaka kuiondoa Serikali ya Gaddafi.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Good ino bro....kip it on
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Lazima atoke nguvu ya umma haina salia mtume na hairudigi nyuma aisee
   
 4. W

  We can JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini badilisha END note yako juu ya kampeni za 2015. Nadhani unaudhi watu wengi kwa kufanya hivyo!
   
Loading...