Gabo kumbe anakula "Mary Jane"

Harry singo

JF-Expert Member
Apr 24, 2016
352
437
Asalaam alaykhum,

Kwakweli wale waliopata wasaa wa kusikiliza interview ya salama na gabo leo watakua wamepata kusikia confession ya Gabo exclusively kwamba naye anatumia mjani aka mjamaika aka maryjane marijuana.

Salama alimwambia anywe juice Haina kilevi kisha akamuuliza kama anatumia tarumbeta ama gambe akakanusha kwamba hatumii hajawahi tumia na hatakaa atumie.

Salama nae alivyo mnoko akachomekea na mjamaika je, Gabo bila kusita akasema kama kawa na maneno ya lafudhi ya kijamaika wakacheka Kisha akagonga, akasema tuongee kwa pin (password) Kisha salama akasema natumai ipo siku milango itafunguka wanaujua hizo pin wataelewa.

Story moja- kasema akiwa kijana siku hiyo katoka kusizi karudi kamkuta mshua na bi mkubwa wapo sebleni kapita chap hajasalimia kaenda ficha mzigo; ye mwenyewe kwa pin aliita chuma, kwenye frij akarudi ndio akasalimia akaulizwa we mbona husalimii kajitetea tetea happy kaona ni msala akaenda kutoa 'chuma' kwenye friji akapeleka nje ila akasikia kama anaongelewa hivi, wanamsema.

Nini naoni yako kwa star mkubwa Kama gabo anayeshikilia rekodi ya miaka Saba( kwa muktadha wake) ya star Bora wa kiume b/movie kutumia mjani?

Ni kweli wanaotumia wanakua vichaa? Ni kweli wanaotumia hawafanikiwi? Nimebaki na maswali
Hebu to maoni
 
Watu wengi sana mashuhuri na wakubwa wanatumia Kijiti.. huezi amini ukiambiwa / kuona.
 
Back
Top Bottom