Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 2,786
- 7,567
Wakuu,
Ni mwendo wa kuendelea kuangalia panapovuja mpaka iache kunyesha.
Meza Kuu inajumuisha;
Henry Kileo - Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Kinondoni - Nimekaa kwenye chama kwa uaminifu sana, lakini chama sasa kimepoteza muelekezo wa kiongozi, demokrasia hamna, na haya yametokea baada ya G55 kutaka kutoa maoni yetu. Sisi ni waasisi wa G55, Katibu Mkuu alituaita kwaajili ya No Reforms No Election, tukaunda group la watsap ili twende kushauri, tulieleza faida na hasara za kampeni hiyo na kushauri tushiriki uchaguzi na kuzuia uchaguzi tukiwa washiriki. Lakini tukaanza kuitwa wasaliti na kupangiwa mikakati ya kufukuzwa na matawi ya chama. Chuki hii inaendelezwa na baadhi ya viongozi wa kamati kuu. Natangaza rasmi nimejivua uachanama CHADEMA, nimefanya hivyo ili kwenda kutafuta jukwaa lingine la kuwatumikia wananchi kisiasa, nna uhakika jukwaa ntakalolipata nitalitumia vizuri. Natafuta Jukwaa lininge ambalo si CCM, ntawajulisha baadaye naenda jukwaa gani kwaajili ya kuendeleza mapigano.
Patrick Assenga - Mwenyekiti Jimbo la Segerea, Mweka Hazina Kanda ya Pwani
Nimewahi kuwa mbunge na diwani, na kukipigania chama kwelikweli, CHADEMA ilikuwa chama cha mapambano tulikuwa hatuogopi kitu, kulikuwa na demokrasia na kila mtu alikuwa anaweza kuongea na kushauri chochote, lakini toka uongozi mpya uingie haturusiwa wala kuhoji, ukifanya hivyo unaitwa msaliti. Kama alivyosema Kileo tulianzisha G55 kwa malengo ya kushauri chama kushiriki uchaguzi na si kukwepa, tukae chini na kutengeza mkakati wa kuwashinda CCM na si kuwakimbia. Kati ya sisi tunaotaka kupambamana na CCM nao wanaotaka kukimbia nani kahongwa? Leo Mei 14, 2025 natangaza rasmi kujivua uanachama CHADEMA na kuachia nafasi zangu zote. Tunaenda kuendeleza harakati kwengine, na hii ni nchi nzima na wanachama wengine ambao wapo nyuma yetu
Moza Ally - Makamu Mwenyekiti BAVICHA
Siasa na katiba ipo katika mfumo wa vyama vingi na mustakabali wa nchi yetu unatokana na siasa, mwanzo nilikuwa naunga mkono No Reforms No Election, baada ya kutafakari sana nimeona chama kimekosa kunipa mbinu halisi ya kwenda kuzuia uchaguzi. Nimeona nisisaliti dhamira ya kweli ya kuwasema watanzania kwenye vyombo halisi vya maamuzi, nitafute jakwaa lingine la kisiasa kuwasemea watanzania. Nitakapokwenda kwenye jukwaa jingine la kisiasa na tutaposema tunapoelekea ninaomba mniunge mkono. Natangaza rasmi kujivua uanachama wangu CHADEMA
Glory Tausi - Mwanzilishi wa CHADEMA Digital, Mtiania Jimbo la Morogoro Kusini
La kutoshiriki uchaguzi kwangu halijakaa sawa, kwenda kuzuia uchaguzi tunazuia na kumnyima raia haki yake ya kupiga kura na kuchaguliwa kama amekidhi vigezo vya kuchaguliwa. Suala hili kwangu limekuwa gumu na siko tayari kushiriki dhambi ya kumzuia raia kushiriki kwenye uchaguzi. Pia umoja, amani na demokrasia ambayo tumezoea ndani ya chama vimepungua au kuondoka kabisa, na hii imetukuta zaidi kwa sisi ambao tulikuwa tunamsapoti Mbowe. Nimejivua uanachama CHADEMA
Asha Abubakari - Katibu CHADEMA Wilaya ya Segerea, Mjumbe Baraza Kuu Tiafa, Mjumbe Kamati Kuu Taifa.
Nimekulia kwenye familia ya wapinzani, nimesomeshwa kwa pesa ya CHADEMA, na malengo yalikuwa nije kupila fadhila kwa chama lakini chama sasa hivi hakifuati Katiba, hatuwezi kuendesha chama kwa matamko. Unawezaje kuzuia uchaguzi wakati hauna silaha yoyote ya kupambana? Viongozi wetu wa juu wameongea sana kuhusu No Reforms No Election lakini hawajawahi kusema madhara ya kutokuwepo uchaguzi, ili watanzania wenyewe wapime. Chama cha siasa kinaenda na upepo, tulikuwa tunamsema Lowassa lakini 2015 alikuwa mgombea wetu, Lissu alipokamatwa maaskari hawakuzidi 20 lakini Watanzania hawa hawa walibaki kuangalia, hawakuweza kuzuia. Wanzania hawa tunaowategemea kwenda kuzuia uchaguzi bado hawapo tayari, naona chama changu kinaenda nje ya malengo. Najivua uanachama CHADEMA na nafasi zote nilizokuwa nashikilia