Tatizo la chama kukaa madarakani muda mrefu ni kutokea recircling. Walewale vijana wa makamba, Nauye, Mwinyi na wengine ndio utawaona kwenye system. Ukienda balozi za nje utawakuta vijana wengi wa vigogo ambao hata hawajasomea kazi hiyo ila wale waliosomea na ni competent wapo mtaani wanazurura. Ni halali akina Makamba kutetea system ya CCM maana ikiendelea kuwepo wataendelea kuweka mirija yao hapo. Wewe kijana uliyetoka familia duni ukiiunga mkono CCM ina maana unataka wewe uendelee kuwekwa pembeni au ule makombo. Wakiingia watu wapya, nafasi zitafunguliwa na uwezekano mkubwa ni wewe kunufaika kuliko kupata tabu. Wakiingia wapya hawatakuwa na backlog ya kulipa fadhila na vijana tutakuwa na say ila hawa CCM ni ngumu wewe kuingia. Vijana 2015 tulete mabadiliko, tuanze upya na Chadema ndio chama muafaka. nao wakikaa miaka kumi tukiona wanaanza U ccm tutawabwaga, nchi itakuwa na uadilifu maana aliye madarakani atakuwa kwenye kiti moto muda wote. Sisemi tuingie nasi tule ila tuingie nasi tujenge nchi, tulete mambo mapya, wale wenye uwezo kiakili wapewe nafasi, tusiangalie wewe mtoto wa nani bali una nini kichwani kwa ajili ya ku deliver:hug: