FUTILITY/ THE WRECK OF THE TITAN.

FUTILITY/ THE WRECK OF THE TITAN.

Huyu Mimi

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2019
Posts
2,575
Reaction score
2,121
Hii Ni Riwaya Iliyoandikwa Miaka Ya 1898 Na Mwandishi Morgan Robertson Aliyekua Mtoto Wa Nahodha Wa Meli (Captain). Masimulizi Ndani Ya Riwaya Hii Yanahusu Wasafiri Wanaotumia Meli Kama Chombo Cha Usafirii Kutoka Sehemu Moja Kwenda Nyingine.

Ndani Ya Riwaya Hii Inamuelezea Jamaa Anaeitwa John Rowland Aliyefukuzwa Kazi Katika Jeshi La Wanamaji Huko U.S Yeye Alikua Kama Afisa Wa Jeshi Hilo La Wanamaji. Baadae Jamaa Anapata Kazi Katika Meli Moja Kubwa Iliyojulikana Kama Titan. Siku Moja Usiku Mwez Wa4 Wakati Meli Hiyo Ikiendelea Na Safari Zake Iligonga Mwamba Wa Barafu Na Kuzama Katika Bahari Ya Atlantic. Hii Nimeeleza Kwa Kifupii Tuu Maana Riwaya Hii Inafanana Kabisa Na Story Ya Kuzama Kwa Meli Ya Titanic Japo Kuna Tofauti Ndogo Ndogo. Baada Ya Bwana Robertson Kuandika Riwaya Yake Miaka Kumi Na Nne(Mwaka 1912) Baadae Ikaja Kuzama Katika Uhalisia Meli Ya Titanic Na Ukiangalia Stori Zote Mbili Zina Ufanano Kama

KUZAMA KWA MELI.
Hapa Mwandishii Alielezea Meli Yake Katika Riwaya Ilizama Usiku Tena Mwezi Wa Nne Na Katika Maisha Halisi Ikatokea Hivyohivyo Meli Ya Titanic Ilizama Mwezi Wa Nne Usiku.

BAHARI MELI ILIPOZAMA.
Katika Riwaya Ile Meli Ya Titan Ilizama Katika Kaskazini Mwa Bahari Ya Atlantic Lakini Pia Meli Ya Titanic Pia Hivyo Hivyo Ilizama Katika Bahari Hiyo Hiyo.

UFANANO WA MAJINA Na SAFARI ZAKE.
Ukiangalia Tu Majina Ya Meli Zote Yanaendana Huku Kwenye Riwaya Iliitwa Titan Na Huku Katika Maisha Halisi Iliitwa Titanic. Pili Zote Meli Zilitajwa Kuwa Haziwez Kuzama Pia Ni Kubwa. Pia Zote Yaani Titan Ilikua Inafanya Safari zake Kutoka Uingereza Kwenda Huko New York Na Pia Hata Meli Ya Titanic Ilifanya Safari zake Hivyo Hivyo.

SABABU YA KUZAMA KWA MELI.
Katika Riwaya Tunaona Mwandishii Anaeleza Sababu Ya Kuzama Kwa Meli Ilikua Ni Baada Ya Kugonga Mwamba Wa Barafu Na Katika Maisha Halisi Chanzo Cha Kuzama Meli Ya Titanic Ilikua Ni Baada Ya Kugonga Mwamba Wa Barafu Katika Bahari Hio Hio Ambayo Mwandishii Aliiandika Miaka Kumi na 4 Kabla Ya Kuzama Kwa Meli Ya Titanic.

KUTOKUTOSHA KWA BOTI ZA UOKOAJI.
Katika Masimuliz Tunaona Kabisa Meli Ya Titan Ilikua Na Boti Chache Za Uokoaji Hivyo Kushindwa Kuwatosha Wahanga Na Zinakadiriwa Zilikua 24 tu Na katika Meli Ya Titanic Ilitokea Hivyohivyo Na Boti Za Uokoaji Hazikuwatosha Watu Na Inakadiriwa Zilikua Takriban 20.

REKODI YA WATU KUPOTEZA MAISHA.
Katika Pande Zote Mbili Tunaona Kabisa Watu Wengii Walipoteza Maisha Baada Ya Kuzama Kwa Meli, Katika Meli Ya Titan Watu Takriban 2,500 Walipoteza Maisha Wakapona 13 Na Katika Meli Ya Titanic Watu Takribani 1523 Walikufa Na 705 Kupona.

Baada Ya Kutokea Hivyo Watu Wakaanza Kumpongeza Jamaa Aliyeandika Riwaya Hio Na Akasema Hajui Chochote Maana Riwaya Iliandikwa Kiutalaam Kama Meli Zinavyotengenezwa. Japo Kuna Baadhi Wanasema Kuzama Kwa Meli Ya Titanic Kulipangwa.
 
Back
Top Bottom