donata fredy
Member
- Jul 22, 2016
- 45
- 87
ifahamike kwamba, ufugaji na kilimo ni uwekezaji mzuri hasa kwa wakulima wenye mashamba madogo na hata yule mkazi wa mjini ambaye anaweza kulitumia eneo lake la uwani kufuga.
Ifahamike pia kwamba, ukulima ni sawa na biashara na biashara nzuri lazima iwe na mpangilio mzuri hasa kwa matumizi ya pesa zinazoapatikana. Kabla ya kuanzisha miradi yako, lazima uwe na mpango mzuri hata kama unaanza mf na mifugo michache, kwani kwa kufanya hivyo utaweza kujua gharama zake na hiyo itakusaidia pia hata kuongeza mifugo mengine na kupanua mradi.
Utafiti wangu-:
Wengi sana wamekuwa na ndoto ya mafanikio lakini wameshindwa kuifikia. Wengi wametumia pesa nyingi sana katika kuanzisha project kwa ghalama kubwa sana lkn wameishia kudaiwa tu pasipo kupata faida. Lakini tatizo ni sisi wenyewe na wala si kingine...
Anza na kidogo kwanza. Usianze na kikubwa
Mpango wako wa mradi ndio pia utatoa taswira ya matumizi ya fedha kwa sababu kama hutakuwa na matumizi mazuri ya pesa hizo huenda iwe vigumu kununua vitu muhimu ili kuendeleza biashara hiyo.
Kwa maana hivyo, hata baada ya kuanzisha mradi huo, ni vyema ukumbuke kuweka rekodi ili kujua ikiwa unapata faida au hasara na ili kuweza kubaini matatizo yanayoikumba biashara yako.
Kilimo na fugaji ni mradi unaoweza kuanzishwa katika vikundi, lakini pia unaweza kuanzishwa na mtu mmmoja mmoja.
Endapo mtaamua kuungana ni lazima muunde vikundi au vyama ambavyo mtafaidika navyo na pia vitasaidia kupigania kupata bei nzuri ya bidhaa zetu pamoja uimarishaji wa sera za serikali ili kutuwezesha kufanya biashara yetu chini ya usaidizi mzuri kutoka kwa serikali.
Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizo na maofisa kilimo na mifugo (maofisa ugani) waliohitimu vizuri lakini Tulio wengi huwa hawawatumii maofisa hawa ipasavo ambao kazi yao kuu ni kukuhudumia. Ukitaka kufuga vizuri utafanikiwa ikiwa utatafuta msaada na ushauri kutoka kwa maofisa hao wa serikali walio kwenye eneo letu
Maswali ya msingi yanayoulizwa na watu wengi:
-Kwanini sifanikiwe
-Kwanini inakuwa hivi.
- kwann utumie pesa nyingi Afu ziteketee?