Fursa za kuingia Abroad kwa njia rahisi zaidi

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalam wakuu,

Kama kichwa cha uzi huu kinavyosema, Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wengi kutaka kujilipua abroad na hii ni Kutokana na Jua kuzidi kuwa kali hapa Bongoland, kukosekana kwa ajira baada ya kumaliza vyuo, mitaji ya kujiajiri nayo kuwa changamoto hivyo vijana wengi wamekuwa wakijaribu kuangalia fursa za kuingia abroad either kwa njia halali ama kuzamia ili mradi tu kuondokana na shida za hapa bongo.

Nikiwa mhanga mmoja wapo pia, hapo kipindi cha nyuma nilijaribu kupitia nyuzi mbalimbali zilizokuwa zikizungumza na kwa jinsi gani unaweza kupata nafasi ya kutoka na kisha kuzamia kwenye nchi mbalimbali duniani,
Wapo waliosuggest kwenda kwa njia ya kusoma kisha kuzamia baada ya masomo wapo walioona njia ya kutafuta mahusiano kisha kupata uraia n.k

Well, kwa upande wangu kwenye pitapita zangu nikapata njia murua kabisa inayonifanya nipate nafasi ya kuingia majuu pasipo shuruba yeyote wala kumdhuru au kumtapeli mtu. Twende sawa sasa

FULLY FUNDED CONFERENCES & EXCHANGE PROGRAMS
Hii ni mijumuiko maalumu ya vijana wa kada mbalimbali either za kiuchumi, kimazingira ama kitamaduni ambazo zinakuwezesha kukutana na kujadili mambo mbalimbali yahusuyo kada husika na vijana ama wanakada wengine wa majuu, yapo mashirika na makampuni makubwa yanayotoa nafasi kwa wanafunzi ama vijana waliomaliza vyuo kukutana kwaajili ya makongamano haya na mara nyingi huwa ni fully funded na hugharamia kila kitu ikiwemo upatikanaji wa visa etc, unachohitaji ni passport na skills zako tu kichwani.

Kupitia njia hii nimeweza kutoboa Germany kwa mwezi mmoja huku nikifanikiwa kutengeneza "koneksheni" na mazingira zaidi ya kurudi huko soon huku so far nikijiandaa na safari ya Denmark.

Nini unatakiwa kufanya?

Njia hii mara nyingi si gharama ila ni utundu wako wa kukwangua vocha na kutembelea websites mbalimbali ili kukutana na fursa hizo,
Hizi ni baadhi ya website unazoweza kuchungulia


Ukifanikiwa kupata nafasi then do what you think its right for you, ukitaka kuzamia moja kwa moja then do it, ukitaka kupata mama wa kizungu huko pia juu yako ama ukitaka kutengeneza routes zaidi kama nilivyoamua mimi pia ni juu yako.

Mengineyo Tutaendelea kujuzana zaidi.
@mafuayakuku


Kitabu ndio hivyo kishaanza kuchafuka.
1569836208437.jpeg
 
Ndio maana nikasema zipo njia nyingi za kuingia huko, so kama hii haiwezi kuwa suitable may be you can try nyinginezo.
 
Back
Top Bottom