Fursa za Kibiashara kwenye ICT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fursa za Kibiashara kwenye ICT

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MwanaHaki, Dec 22, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  WanaJF

  Mara nyingi, wataalam wa ICT (programmers, developers, coders, etc.) huwa hawashiriki au hawashirikishwi moja kwa moja kwenye uwekezaji wa fursa za kibiashara, kwa kuwa, mosi, wengi wao hawana uwezo wa kifedha. Lakini, cha ajabu ni kwamba, kila anayewekeza pesa zake huwatumia wataalam hao, ambao wao hutumia taaluma zao kuendesha miradi hiyo ya kibiashara - wakiwa ndio nguzo na uhai wa biashara hizo - pasi na kunufaika moja kwa moja kwenye faida zinazopatikana, isipokuwa mishahara duni wanayolipa.

  Kama mjasiriamali na mbunifu, nimebuni miradi mitatu ya uhakika, ambayo nataka kuiendesha kwa kushirikiana moja kwa moja na watu ambao ni wataalam, wenye uwezo wa taaluma, kama vile, programming, development, etc. Kama wewe ni mtaalam wa JAVA, PHP, XML, PERL, Linux, ASPNet, na kadhalika, unakaribishwa tuwasiliane. Nitumie PM, kisha tutapanga nini cha kufanya, ili mimi na wewe tuwekeze taaluma zetu.

  Mimi ni mtaalam wa mawasiliano (communication) zaidi ya teknolojia (technology). Ninawatafuta wataalam wa teknolojia, ili tuunganishe taaluma zetu na kuanza kuwekeza na hatimaye kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

  Wapo wanaosema kwamba kuwa mwanataaluma hakulipi. Mimi nakataa. Taaluma yako ndio mtaji wako, na inalipa!

  Tuwasiliane.

  Nawatakieni nyote sikukuu njema na heri na fanaka kwa mwaka mpya 2010!

  ./Mwana wa Haki
   
 2. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  kaka upo pande za wapi? unataka kuanzisha kampuni au tayari unayo ila unataka watendaji?
   
Loading...