Fursa ya Kurudi kwenye mfumo rasmi wa elimu

Fursa ya Kurudi kwenye mfumo rasmi wa elimu

Mbona hzo program mostly known as Foundation/bridge course zimeshakatazwa?.au mleta mada vipi?. From what i know and from experience ata usome hzo course bila kuwa na pass 4 Olevo huwez kwenda popote. NIKO VERY SURE, tho i stand to be corrected
 
Karibu sana. Watu wengi hawafahamu badala yake mtu anakwenda kurudia mitihani ya kidato cha NNE bila mafanikio. Sasa hii program ni nzuri kwasababu wakati unapata qualification ya kwenda mbele pia unapata ujuzi wa kuweza kuajiriwa na kufanya kazi
Mmm. Si kweli..unless tuoneshe usajili wa hicho kituo na other supporting documents.
 
Ahsante Mediocrist kwa kutaka kujifunza zaidi. Fungua hiyo image kwenye kipengele number 5 kinaonyesha. Pia kwa sisi ambao tupo chuoni kama admission officer tunaona vizuri zaidi jinsi gani tunawasajiri wanafunzi kwenye Institution Panel ya NACTE kuna option ya VETA kama mtu O level hana 4 passes.
Veta na maelezo yako ni vitu viwili tofauti. Me pia nasajili wanafunz. Icho kitu unachosema hakipo na hakiwezekani. Sikuharibii biashara lkn hicho kitu unachosena, embu usiwapotezee watu muda na gharama.
..
Yaani nyie vijana, mark my words" you won't even be able kuanza kusoma Certificate/astashada#
 
Umeongea vizuri.

Hii program ni mpya imeanza mwaka huu 2017. Zamani walikuwa wanazo zile NABE zilikuwa special kwa watu wenye uzoefu lakini wakawa wanachukua hadi fresh from school. Kwenye Chuo chetu tunatoa certificate, Diploma, na Bachelor Degree. Wanafunzi wengi walikuwa wanashindwa kujiunga na certificate kwa sababu hawana pass nne. Tukatengeneza carriculum inayoitwa procurement and supply under VETA ambayo haipo kabisa Tanzania kwenye level ya VETA. Baada ya hapo tukapeleka kwa bahati nzuri wakatujibu wao pia wapo kwenye mchakato wa kutengeneza course inayoitwa Business Operation Assistant ambapo wakasema procurement ipo ndani pamoja na course zingine mbalimbali zitakuwa ndani ya hiyo program. Walipomaliza kutengeneza wakatupa hiyo course rasmi tukaanza kutoa tokea mwaka huu 2017. Kama bado haupo updated unaweza kwenda VETA ukauliza kuliko ukawamislead watu.
 
Mbona hzo program mostly known as Foundation/bridge course zimeshakatazwa?.au mleta mada vipi?. From what i know and from experience ata usome hzo course bila kuwa na pass 4 Olevo huwez kwenda popote. NIKO VERY SURE, tho i stand to be corrected
Ahsante kwa mchango wako ndugu Cutel

Hii sio foundation/bridge course kama unavyosema. Nimedownload image ya TCU guide inayoonyesha sifa za kujiunga Degree na kwenye kipengele cha tano kuna equivalent qualification kwa maana ya Diploma na O level 4 passes pia kuna addition hapo ya NVA level III with less than four O level passes. Naomba ufungue tena hii images iweze kukusaidia uelewa wako.
 
Attachments

  • Screenshot_20171005-183522.png
    Screenshot_20171005-183522.png
    36.6 KB · Views: 71
Mkuu niko na pass 4 na Nina diploma ya IT kuto computer society of kenya. Ntaweza kupata nafasi ya kuingia chuo kweli
 
Mkuu niko na pass 4 na Nina diploma ya IT kuto computer society of kenya. Ntaweza kupata nafasi ya kuingia chuo kweli
Ahsante kwa swali lako.

Ni kwamba kama una pass 4 na Diploma with not less than 3. 0 GPA unaweza kujiunga na bachelor Degree program.
Karibu kusoma
 
Nashukuru Mediocrist kwa mchango wako. Kuhusu swala la kuingiza degree linawezekana. Ukiingia kwenye admission system ya Nacte au TCU kuna sifa za kujiunga na Degree. Kwa mfano kwa wahitimu wa Diploma wanatakiwa kuwa na Diploma pamoja na kidato cha nne wawe na ufaulu wa pass kuanzia nne na kuendelea lakini kama amemaliza hiyo program anaweza kuitumia kama equivalent qualification kuingia Degree
Nina rafiki yangu ana D tatu alianza certificate chuo kinaitwa Seki kiko Dodoma had Diploma akamaliza apo mwisho wa siku aliomba kujiunga na shahada Taasisi ya Uhasibu Tanzania na akadailiwa leo hii kamaliza kwenye Taasisi iyo na ana shahada yake ya Usimamizi wa biashara (BBA) kutoka chuo na kapata Upper Second ya 3.6

ukiwa na hata na D tatu unajiunga na degree
 
Ahsante mkuu kwa mchango wako.

Njia sahihi na rahisi ya kujua kwamba mwanafunzi anatakiwa kuwa na sifa gani ili aweze kujiunga na degree ni kwa kutumia TCU au NACTE guide book ndio itatusaidia kuondoa ubishi usio kuwa na kusaidia. Kama chuo kitakwenda tofauti na hizo guidelines basi hao watakuwa na Double standard.
 
Tangazo.

Fursa kwa vijana waliopata pass chache za kidato cha nne yaani kuanzia D moja na kuendelea . kuna Program imeandaliwa kwa miaka miwili inayoitwa Business Operation Assistant. Mwanafunzi akijiunga na hii program anaweza kupata faida zifuatazo:

1. Kupata fursa ya kujiunga na Diploma moja kwa moja kwenye fani aitakayo mara baada ya kumaliza.
2. Kurudi kwenye mfumo rasmi wa elimu ya Tanzania
3. Kupata professional skills na cheti kwenye areas kama Accounts,Procurement, Marketing, Stores, Logistics mgt, nk.

Wahi sasa kwa maelezo zaidi wasiliana na namba hii. 0718476238 au 0742934704. Course inatolewa na Institute of Procurement and supply IPS- chanika
Nina mashaka nahizo program, serikali hitaki tena foundation course hizo. So wahitaji hakuna kilicho rahisi kwenye maisha njia pekee ni kurudia mtihani wa kidato cha nne au sita. Njoo Excellent Training Center, wasiliana nasi kupitia excellenttrainingcentre20@gmail.com
 
Hii sio biashara ya kuuza dagaa. Tunasimamia jinsi ya kuendeleza jamiii na huwezi kuendeleza jamiii kama sio mtu wa kusema ukweli. Hiyo sio foundation program kama unavyosema kwa kutumia uelewa wako mdogo ni bola kama hujui kitu ukajifunza. Hiyo course IPO chini ya VETA ni serikali, pia TCU na NACTE wanazitambua unaweza ingia kwenye website yao ukapata kuongeza uelewa wako. Huko nyuma kwenye cooment zangu nimeweka kipande cha image ya hiyo guideline ya TCU. Sasa sijui unasema serikari ipi? Nakuwekea tena ujifunze ili kupanua mawazo yako.
 
Attachments

  • tapatalk_1507441148147.png
    tapatalk_1507441148147.png
    36.6 KB · Views: 70
Back
Top Bottom