Fursa ya kilimo biashara kupitia taasisi za dini

ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
2,279
3,178
Tuna tatizo kubwa sana la ajira, watu wamefunga, wengine wanakesha wakisali na kuomba makanisani na misikitini wapate ajira lakini bado tatizo lipo.

Tanzania tumebarikiwa Ardhi, Halafu pia Tanzania tumebarikiwa kuwa na mfumo mzuri wa taasisi za dini. Makanisa na misikiti. Kwanini vijana tusipambane na umaskini huu kupitia taasisi za dini? Nimesema taasisi za dini sababu ndio njia rahisi ya kuonganisha raia katika Jamii.

Kama tujuavyo ili kilimo kiwe na mafanikio na mkulima aweze kuvuna basi kunatakiwa Kuwe na Ardhi, Mbegu, Mbolea, Madawa na Hali nzuri ya hewa. Baada ya mavuno kunatakiwa Kuwe na mteja ambaye atanunua bidhaa. Pia kutokana na kutokuwa na mkataba na hali ya hewa basi kunatakiwa Kuwe na Bima ya mazao ili endapo kutatokea majanga basi Bima itagharamia hasara.

Mambo yote hayo niliyoyataja yanawezekana endapo tu tutajitengenezea mfumo mzuri wa kibiashara kati ya vikundi ndani ya taasisi za dini, serikali na mashirika ya fedha.

Yafuatayo ni maoni yangu katika kupunguza tatizo la ajira kwa njia ya kilimo biashara:

Taasisi zitengeneze mifumo itakayowaunganisha makundi ya vijana na serikali ili watengenezewe mazingira ya kilimo biashara.
Waziri husika anaweza kusimamia hili lifanikiwe kwa mfumo ufuatao:

1. Kuwe na vikundi vya kilimo.
2. Serikali iangalie uwezekano wa kupata Ardhi na Soko nje ya nchi.
3. Mbegu, Madawa, na mbolea vinaweza kutolewa kwa njia ya mkopo halafu baada ya mavuno na mauzo serikali ikarudisha gharama zake.
4. Serikali inaweza kusaidia kwenye Bima ya mazao shambani ili pale kunapotokea majanga au ukame basi Bima ifidie hasara.
5. Kuwe na vikundi vya collection, processing na packaging
6. Kuwe na vikundi vya usafirishaji ili kumfikia mteja nje ya nchi.
7. Taasisi za fedha za ndani zitumike kutoa mikopo kwa ajili ya usafirishaji kwa riba nafuu.

Baada ya mauzo gharama za mbegu, mbolea nk zinatolewa, gharama za usafirishaji ili kumfikia mteja na riba kwa benki zinarudishwa na faida inayobaki inaenda kwenye kikundi husika.

Hapa wahusika ni
1. Wakulima + Wakusanyaji Mazao + Wauzaji: haya ni Makundi ya vijana chini ya mwamvuli wa taasisi za dini. Hawa watausika na kilimo, uvunaji, kuhifadhi kwenye maghala, usafishaji na kuweka mazao masafi kwenye vifungashio tayari kwa mauzo nje ya nchi.
2. Serikali: Wizara husika itakayopambania miundo mbinu, Ardhi, Pembejeo kwa njia za Mkopo, na masoko nje ya Nchi.
3. Taasisi za Fedha: watahusika kutoa mikopo ya usafirishaji kumfikia mteja aliyepo nje ya nchi kwa riba nafuu.
4: Taasisi za Bima kwa ajili ya kutoa elimu ya Bima ya mazao.

NB: Bima ya mazao ni muhimu sana endapo kutatokea majanga yatakayosababisha kusiwe na na mavuno basi Bima inarudisha gharama.

Naamini tatizo la ajira litakuwa limepunguzwa kidogo.
 
Back
Top Bottom