Fursa ya biashara ya maziwa

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Naomba ku share nanyi kuhusu fursa hii ya biashara ya maziwa nchini.

Kwa tathimini ndogo ambayo nimeifanya mimi mwenyewe hasa kwa kanda ya pwani kama mkoa wa pwani na morogoro nimegundua maziwa ni mengi kiasi cha kuizidi demand.

Naamini pia kutokana na mkoa wa tanga kushabiliana kwa hali ya hewa na mikoa tajwa hata huko nako hali itakua hivyo.

Wafugaji wanapata shida sana kwenye masoko ya maziwa na kutokana na hili inapelekea wanunuzi wakubwa wa maziwa huchukua maziwa ya wafugaji kwa mali kauli na kuwalipa baada yakuuza maziwa.
Kimsingi biashara hii haihitaji mtaji kikubwa zaidi ya vifaaa tu.

Lakini pia maziwa haya kwa kipindi cha mvua za masika wakati ambapo malisho yanakua yakutosha maziwa yanakua mengi zaidi kiasi ambacho lita moja ya maziwa inauzwa kwa shilingi 500.
Kwa anaefahamu soko la maziwa likoje anaweza tuka share mawazo humu pamoja.

Lakini pia namna bora ni kusindika kwani risk kubwa kwenye biashara hii ni maziwa kuharubika jambo ambalo limekua likisababisha hasara kwa wakulima.

Hapa namaanisha maziwa yanapochukuliwa kwa wakulima na kwa bahati mbaya yakaharibika yakiwa mikoni kwa mfanya biashara,hasara inabaki kwa mkulima na si kwa mfanya biashara.
Kwa mwenye ulewa zaidi anakaribishwa
 
sio rahisi mkuu kwani yale ma tank yakuhidhaa maziwa yenye cooling system ni ghali kiasi flani.
 
Sijawahi kusikia maziwa yameshuka bei hadi kufikia sh. 500/= kwa Lita moja, labda vijijini ila sio mjini.
 
Ndio maana nikaiita fursa,
Huko vijijini kwa wafugaji maziwa ni mengi na bei yake ni ya chini sana.
 
Nafuga Tu Na Kwa Sasa Napata Maziwa Kama Lita 25, Ila Baada Ya Miezi 3 Nitakuwa Na Lita Kama 80, Kwa Dalili Nazoona Nitauza Maziwa Yote
 
Unaweza kunisaidia ni Vijiji Gani yanapatikana kwa wingi
Ni rahisi bt inakutaka maandalizi,

Coast zone yote anza ruvu njoo chalinze nenda na njia ya tanga au njia ya moro huko vijiji vyote maziwa kwa wanunuzi wanaochukua kwa wingi bei ni ya chini mno,

Changamoto ni lazima uwe na kituo kwani sio rahisi kwa wewe mwenyewe kukusanya vijijini,wafugaji wanaishi vichakani na wapo mbalimbali,wapo wachuuz wanaleta kwenye vituo ambapo kunakua na ma tank makubwa yenye mfumo wakupooza waziwa yasiharibike
 
Changamoto kubwa katika suala hili ni kwamba wakati wa masika kuna kua na maziwa mengi sana hivyo bei inashuka maradufu na wakati wa kiangazi uzalishaji unakua mdogo kwa sababu ya changamoto za malisho.

Hilo Gap ni fursa, kwa wenye mitaji na uwezo wa kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza bidhaa zitokanazo na maziwa kuwekeza.
Karibuni.
 
Ni rahisi bt inakutaka maandalizi,
Coast zone yote anza ruvu njoo chalinze nenda na njia ya tanga au njia ya moro huko vijiji vyote maziwa kwa wanunuzi wanaochukua kwa wingi bei ni ya chini mno,
Changamoto ni lazima uwe na kituo kwani sio rahisi kwa wewe mwenyewe kukusanya vijijini,wafugaji wanaishi vichakani na wapo mbalimbali,wapo wachuuz wanaleta kwenye vituo ambapo kunakua na ma tank makubwa yenye mfumo wakupooza waziwa yasiharibike
Nakushukuru sana kwa maelezo yako Mazuri kuna kipindi nilitaka kufanya hii kitu sema kuna changamoto flan ilijitokeza Tukakwama...lkn mpaka sasa bado ninahilo wazo nakusanya nguvu tu.
 
Naomba ku share nanyi kuhusu fursa hii ya biashara ya maziwa nchini.

Kwa tathimini ndogo ambayo nimeifanya mimi mwenyewe hasa kwa kanda ya pwani kama mkoa wa pwani na morogoro nimegundua maziwa ni mengi kiasi cha kuizidi demand.

Naamini pia kutokana na mkoa wa tanga kushabiliana kwa hali ya hewa na mikoa tajwa hata huko nako hali itakua hivyo.

Wafugaji wanapata shida sana kwenye masoko ya maziwa na kutokana na hili inapelekea wanunuzi wakubwa wa maziwa huchukua maziwa ya wafugaji kwa mali kauli na kuwalipa baada yakuuza maziwa.
Kimsingi biashara hii haihitaji mtaji kikubwa zaidi ya vifaaa tu.

Lakini pia maziwa haya kwa kipindi cha mvua za masika wakati ambapo malisho yanakua yakutosha maziwa yanakua mengi zaidi kiasi ambacho lita moja ya maziwa inauzwa kwa shilingi 500.
Kwa anaefahamu soko la maziwa likoje anaweza tuka share mawazo humu pamoja.

Lakini pia namna bora ni kusindika kwani risk kubwa kwenye biashara hii ni maziwa kuharubika jambo ambalo limekua likisababisha hasara kwa wakulima.

Hapa namaanisha maziwa yanapochukuliwa kwa wakulima na kwa bahati mbaya yakaharibika yakiwa mikoni kwa mfanya biashara,hasara inabaki kwa mkulima na si kwa mfanya biashara.
Kwa mwenye ulewa zaidi anakaribishwa
Mkuu vip hii mishe bado unaiendeleza? Maana na ujuzi wakutengeneza bidhaa za maziwa kama mtindi plain na za flavour nipo bunju dsm kama vip tunaeza fanya iyo project yakusindika maziwa maana hapa dsm uhitaji ni mkubwa wa mtindi
 
Naamini hukunielewa mkuu,
Mimi nilijaribu ku share kwa minajili ya kufichua fursa ambayo inawezekana mtu akawa anahitaji maziwa lakini aidha anayakosa ama anayapata kwa tabu ama kwa bei kubwa kwasababu tu hajui maziwa ya bei chee angeyapata wapi.
Mimi binafai sijawahi kufanya biashara ya maziwa,hata hivyo sio kwamba sipendi kufanya hapana;ila biashara hii inahitaji pesa nyingi kidogo ili uifanye kwa uhuru,
Mfano,
1)Utahitaji standby generator kuondoa risk pindi umeme ukikatika,
2)Utahitahi ule mtungi wa kupoza ie kama friji ila lenyewe lipo kwa mfono wa tungi kubwa.
Zaidi ya hapo hii kazi itakusumbua kwani mara kwa mara utakua unaharibu maziwa.
 
Back
Top Bottom