Fursa na Uenezaji wa Lugha ya Kiswahili Kimataifa

Fonimu

Member
May 20, 2018
28
27
Habari Wadau wa Lugha ya Kiswahili!

Mimi ni mdau wa lugha ya Kiswahili.

Nimekuwa nikijaribu kukieneza Kiswahili hasa kwa njia ya mtandao, hivyo nimeona si vibaya nikibadilishana uzoefu na wadau wengine wa Kiswahili ndani ya jukwaa hili.

Juhudi zangu chache zinaweza kuonekana katika blogu zangu:
www.ulingowakiswahili.blogspot.com ( Ulingo wa Kiswahili )
na
www.swahiliplatform.blogspot.com (SWAHILI PLATFORM )

Pia, mwaka 2017 nilifanya utafiti binafsi na kuandika ripoti kuhusu matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari vya kimataifa (Habari za Kiswahili katika tovuti). Naiambatanisha ripoti hiyo.

Nilisukumwa kufanya utafiti huo, baada ya kuchoka kusoma habari zenye makosa ya lugha ya Kiswahili katika tovuti za vyombo hivi. Kuna baadhi ya vyombo niliwasiliana navyo, lakini hakukuwa na maboresho katika uandishi, hivyo nikaona ni bora nifanye utafiti na kuandika ripoti.

Kuhusu Fursa za Kiswahili Nje ya Nchi;

Nimekuwa nikijifunza mambo mbalimbali, kuhusu fursa za Kiswahili nje ya nchi, kwa muda wote ambao nimekuwa nikikieneza Kiswahili kwa njia ya mtandao. Nitayabainisha mambo hayo kwa pamoja-changamoto na fursa;

1. Kwanza, wanafunzi wengi wa Kiswahili niliowasiliana nao kutoka nje ya nchi (hasa Marekani), wanaamini Kiswahili fasaha kinazungumzwa Tanzania.

2. Kiwango cha elimu kuanzia Shahada ya Uzamili (Master's Degree) ni muhimu, ili uweze kufundisha Kiswahili katika vyuo vikuu maarufu hasa Marekani.

3. Wakenya ni wengi sana wanaochangamkia fursa za Kiswahili, na wanafanikiwa kufanya kazi huko ughaibuni kuliko Watanzania. Inawezekana baadhi ya sababu ni juhudi binafsi na za serikali katika kutafuta ajira za Kiswahili ughaibuni.

4. Kama mtaalamu wa Kiswahili, unaweza kutumia TEHAMA na kujipatia pesa kutokana na lugha ya Kiswahili. Kwa mfano, unaweza kujitangaza na kufanya kazi za: Tafsiri, Uhariri, kufundisha Kiswahili kwa njia ya 'Skype', kuuza 'tutorials' za Kiswahili kwa njia ya mtandao nk (hizo ni baadhi ya fursa).

Kuhusu Kushirikiana katika Kukieneza Kiswahili na Kutengeneza Pesa;

Ili kuitumia TEHAMA na kutengeneza kazi za Kiswahili ambazo zina ubora wa hali ya juu, ni vyema wataalamu mbalimbali washirikiane.

Hivyo, napenda kuitumia fursa hii kuwatafuta wataalamu wafuatao: Wataalamu wa Kiswahili, Wataalamu wa Kiingereza, Wataalamu wa 'Website na Apps', Wataalamu wa katuni (Animation), Wataalamu wa Sauti (Sound Engeneers) nk.

Kwa mfano, niliamua kutengeneza 'tutorials' za kufundishia Kiswahili na nilizifanya kazi zote mimi mwenyewe.

Kiukweli, 'tutorials' hizo hazina ubora wa kiwango cha juu kuanzia sauti, lakini niliona ni bora kufanya kuliko kuacha. 'Tutorials' hizo nilizipakia katika akaunti yangu ya 'YouTube' yenye jina la 'Swahili Platform' ( Swahili Platform) Naziambatanisha 'tutorials' hizo.

Kwa nini nimeamua kuandika humu?

Nimeamua kuandika katika Jukwaa hili, baada ya kufanya uchunguzi na kugundua humu ndani, kuna watu wenye maarifa na msaada wa kufikia malengo mbalimbali katika jamii.

Naomba kuwasilisha.
View attachment RIPOTI YA UTAFITI KUHUSU MAKOSA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI, YANAYOPATIKANA NDANI YA HABARI, KAT...pdfView attachment The Swahili Sounds;-Types & Pronunciation.mp4View attachment The Sound Practice-Complex Style.mp4View attachment The Swahili Sounds-Exercice 1, with the Answers.mp4View attachment The Swahili Sounds-Exercise 2, with the Answers.mp4
 
Hongera sana kwa juhudi binafsi za kuieneza lugha yetu adhimu ya kiswahili. Mungu akufanyie wepesi ufanikishe lengo lako!
 
.....Kwenye bandiko lako sijaona maneno; 'Mathalani', 'Chambilecho', 'Rununu', 'Guru', 'Takirishi', 'Wabobezi' badala ya wataalamu, Hivyo basi nachelea kusema wewe siyo Guru katika Lugha hii adhyuimu( Isomwe Kwa sauti ya salim kikeke) ya Kiswahili! hakuna misamiati Konki kwenye bandiko lako.

Natania tu mkuu, Kila la kheri mwanaharakati wa kiswahili,

Kiswahili kitamu wallahy!
 
.....Kwenye bandiko lako sijaona maneno; 'Mathalani', 'Chambilecho', 'Rununu', 'Guru', 'Takirishi', 'Wabobezi' badala ya wataalamu, Hivyo basi nachelea kusema wewe siyo Guru katika Lugha hii adhyuimu( Isomwe Kwa sauti ya salim kikeke) ya Kiswahili! hakuna misamiati Konki kwenye bandiko lako.

Natania tu mkuu, Kila la kheri mwanaharakati wa kiswahili,

Kiswahili kitamu wallahy!
Ni kweli! Nimeamua kuandika kwa lugha rahisi ili kuwashirikisha wadau na watalaamu mbalimbali, kama vile; TEHAMA.

Nahisi ujumbe unaweza ukachelewa kufika, endapo tutaandika kwa Kiswahili cha Kikamusi.

Kwa mfano, nilitakiwa nitumie istilahi ya 'Mwanaisimu' wa Kiswahili badala ya 'Mtaalamu wa Kiswahili'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom