Fursa kwenye uzalishaji wa Madirisha ya Plastic (PVC Window)

kassamali

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
214
40
Today we are all witnesses of real estate boom in Tanzania the demand for housing is on top priority , I believe our eyes has not yet witness the future of real estate and construction industry in general when we compare to the coming few years

Today no new construction is without PVC Windows, in addition, more and more people want to replace old wooden Windows on plastic design. Due to the high demand of products, more and more entrepreneurs want to organize their own production of PVC Windows. Such companies can win against the competitors that offer products from woden window,
I personal supports and argues the PVC window


  • Maximum energy savings at thermal and acoustic levels. Providing comfort, insulation and tightness.
  • Respect and care for the environment within a sustainable development.
  • PVC Windows do not need maintenance and remain unchanged at the passage of time.


In the list of equipment for the manufacture of plastic Windows includes:

One - and two-head saw for cutting PVC profiles and reinforcement;
Roller conveyors;
Machines for welding PVC;
Copy-milling machines;
Saws for cutting reinforcing profile;
Pleasecontinue machines;
Machines for milling end face of the transom;
Saws for cutting glazing beads;
Cutting saws;
Bending machines;
Stands glazing;
Hood;
The washing machine;
Extruders;
Demineralization;
Mounting the lifting device
Business plan for the production of PVC Windows

Features of a Production workshop
The area depends on the volume of production. The company plans to produce standard double window size - 1400*1200. To open the workshop for the production of PVC Windows, which will produce 20 designs for change, enough space 200 square meters, it should be remembered that the ceiling height must be more than 3 meters.

Next should be the finished goods warehouse.

Machines for the manufacture of metal-plastic constructions will not be able to work without electricity. The supply voltage should be 380 V/50 Hz. Optimal room temperature of 18° C, in the opposite case can disrupt production technology.

Also in the room should have good ventilation. Special attention should be paid to the creation of the lighting system. Throughout the workshop is General lighting, and for some parts of the local light.
Recruitment
To organize a small enterprise for the production of PVC Windows need to hire about 10 people and install a special program.

Such a program with the least errors will calculate the cost of plastic construction and will provide all the information needed for production.

Control
Control of the production process should production Manager and chief technologist will be able to verify that the finished products meet the appropriate standards and requirements of the customer? It must also allocate tasks between work and to control the process.

The organization shall be the engineers, who will monitor the operation of the equipment and, if necessary, to remedy the damage. In the workforce the organization needs to hire at least 7 people, of whom one must be the storekeeper, receipt or dispatch of goods. The optimal organization of production lines and production sites

Curent the demand for Plastic window is more than a million pieces, the demand will increse year to year

Current only few companies are carrying this business the one i knw are only two of them probably there other making them localy

WHAT SHOULD BE DONE?
Tanzania is facing problem of unemployment and capital for many enterprises.We cant sit waiting for the Government in my opinion i think let the private sector drive the country

The only thing is to organize several people and create a cooperative if today 100 people will join together and contribute 1m within a year at the end of the year we will have 100 million

for such amount of money easy to start manufacturing of PVC window without depending from any one and 100 people will be shareholder of the future company the company will create direct employment and many indirect employment hence everybody will see the changes they wanted to see

MY VISION:i have always believed in unity UMOJA NI NGUVU that has always been my motto and inspiration

WHO AM I

If interested this is my profile:
https://tz.linkedin.com/in/anthonykassamali

Regarding the PVC Window i have not only touched them but i have made them i can lead the team for selection of the best and economical equipments and organizing the business to its final results to its fruits

If anyone needs to be a future shareholder of this company let him send email any opinions and coments better you keep them on public for the befenefits of all

in all these things we are more than conquerors (ROMANS 8:37)
 
Kwa kifupi sisi wote ni mashahidi wa wa miradi mbali mbali ya ujenzi kwa wale tulio Dar nadhani kila ujenzi tunauona acha miradi mbali mbali nje ya Dar es salaam.Ni wazi kwamba mahitaji ya nyumba kwa sasa ni makubwa kuliko kitu kingine chochote.Takwimu zinaonyesha kwa sasa kwa mwaka Tanzania inahitaji nyumba laki tatu ili kukidhi mahitaji.Ila kitu kingine japo sisi ni mashahidi wa hali ya maendeo ya ujenzi nataka kuwambia bado macho yetu hayajaona kitu...Macho yetu yataona mengine kuliko tunavyofikiri

Leo hakuna ujenzi unaoendelea bila kuwa na madirisha ya aluminum au plastic(PVC WINDOW)

Leo hii kutokana na mahitaji ya madirisha na milango ya aina kuchukua kasi ya juu makampuni mengi na hata wajarisimali wameamua kujikita humo na si hivyo tu madirisha ya plastic yanaonekana kuyapoteza madirisha ya mbao

JE KWA NINI HAYA MADIRISHA YAMEJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA SI TU TANZANIA BALI DUNIANI?

1)Kwanza yanapendeza ni mazuri machoni
2)Hayahitaji matengenezo yamara kwa mara na yanadumu kwa muda mrefu
3)Pia yanatabia yakutunza nishati –mfano mdogo yanapitisha mwanga kwa urahisi ndani ya nyumba ambapo kama ingekuwa madirisha ya mbao basi unehitaji kuwasha taa ambapo ni upotezaji wa pesa na nishati bure


JE MADIRISHA AINA HII YANATENGENEZWAJE JE NI KILA MTU ANAWEZA KUYATENGENEZA?
Madirisha aina hii kwanza hayatengenezwi kiholela. Ilikuyatengeneza yanahitaji mashine na vifaa maalumu na hata karakana utakayotumia pia lazima iwe na vipimo vyake kutokana na idadi ya madirisha unayoyatengeneza kwa siku na pia si kila mtu anaweza. Haya madirisha yanahitaji utaalamu na hasa linapokuja suala la utumiaji wa vifaa ambavyo karibu vingi vinatoka nje


Kwa sasa Tanzania peke yake bado sijazigusa nchi za jirani mahitaji ya madirisha ya plastic ni zaidi ya milioni kadha kwa mwaka.Kwa haraka haraka ukipiga hesabu nyumba ya kawaida tu ndogo inaweza kuchukua madirisha 10 mpaka 15 hapo hatujagusa miradi mikubwa na si kwamba Tanzania hakuna watu wanayoyatengeneza kuna kampuni moja ya Uturuki na nyingine sina uhakika nayo ni ya kina nani .Haya makampuni kwa sasa yanazungurusha hili gurudumu

Lakini hata ukiangalia kwa makini utaona makampuni haya na watu wengine hawawezi kutosheleza mahitaji

JE NINI KIFANYIKE?
Ukiangalia tatizo la ajira kwa vijana nchini kimekuwa ni kilio cha kawaida sina uhakika kama serikali inaweza kutokomeza hili tatizo kutokomeza hili tatizo lazima uwe na taswira inayoweza kuona mbali zaidi na zaidi na bado nina amini kuwa ni vizuri binafsi ikaendesha nchi

MAWAZO YANGU
Hakuna kitu chini ya jua ambacho kitamshinda binadamu na palipo na wengi siku zote kuna suluhisho,kushinda tatizo la ajira ni watu kujiunga na kukusanya mtaji na kufanya kitu Fulani

Mfano mdogo leo hii wakijikusanya watu 100 wakaanzisha kampuni ambayo itaendeshwa na bodi ya wakurugenzi watu hao wakachanga laki moja kwa mwezi kwa kila mtu ndani ya mwaka kampuni itakuwa na mtaji wa wa shilingi milioni mia moja.Na suala la kuanzisha kikundi ili kukusanya mtaji si jambo geni duniani makampuni mengi makubwa yameefika hapo yalipo kwa njia hii ambapo kila mwanashare anabeba risk zake

Huu ni mfano mdogo sana na unaweza kutumia si kwa hili hata katika mambo mengine mfano ujenzi wa shule za watoto wetu

Kwa shilingi milioni mia moja nirahisi kuanza biashara ya uzalishaji wa madirisha ya plastic na kuingia kwenye soko hichi kitu kina fadida nyingi sana kwanza kama ungekuwa peke yako na milio moja yako kamwe usingeanzisha kiwanda pili kama mngekuwa watu mi na mna kampuni bila kuwa na historia ya biashara sidhani kama kuna benki ingewapa mkopo labda zipo ila mimi bado sijakutana nazo

Taswira yangu kwa umbali naamini kuwa UMOJA NI NGUVU

FAIDA ZINGINE NI ZIPI?
Kwanza kabisa kwa wamiliki wa hisa ndani ya muda Fulani watakuwa wamejikwamua kiuchumi pili watakuwa wametoa mchango wao kwa Taifa kwa kutengeneza ajira kwa vijana wengine wengi wa Kitanzania ukiachilia mbali suala la kodo ambalo litaingia kwenye serikali

Suala la tekmologia ya madirisha haya sio tu nimeiona nimeshiriki kuanzisha miradi kama hiyo sehemu mbalimabli na mingi leo inafanya kazi ikitoa matunda ni mzoefu wa masuala ya biashara,sheria,ujasirimali unaweza kusoma maelezo yangu mengine na miradi niliyo ifanya

https://tz.linkedin.com/in/anthonykassamali


Kama kuna watu wako serious na hii biashara na wangetaka siku moja kuona mabadiliko kwenye maisha basi karibuni kwa mchango wa maelezo na maelezo mengine

Hii ni kwa watu serious tu .suala la mchango ni la mwisho kabisa manake hatuwezi kuongelea kisi cha pesa wakati hata kikundi hamna na hatuambatani na sera zozote za dini,siasa,rangi,kabila sera zangu na taswira yangu ni moja nataka kuona ajira za watu leo hii na si miaka mitano inayokuja,nataka kuona shule bora,hospitali bora na mengine mengi mazuri kwa sisi Watanzania LEO na si kesho

Ni katika Ujenzi wa nchi
 
How can we grouped?

Suala la kuwa grouped si tatizo kwanza tunatakiwa tujiorganized tukishajua idadi ya watu walio tayari then tutaanzisha kampuni.Kampuni ikishakuwa tayari pamoja na lisense zote basi suala la pili litakuwa ni feasibility study pamoja na mchanganyuo mzima wa biasharasitaki kuahidi itachukua muda gani hii kitu naweza nikaihandle kushirikiana na watu wengine wachache kutoka kwenye kikundi.Baada ya mchanganyuo ambao ningependa tuungeneneze katika hatua(phase) basi tutaanza suala la kutumbukiza pesa.Idadi ya pesa itakayopataika itatupa picha tuanzie wapi na kitu gani kinapungua na kama je tutahitaji msaada mwingine kutoka kwa wawekezaji wakubwa haya yote yatakuwa ni matoke ya mchanganyuo wa biashara yote
Pia suala la uchagua wa vifaa halifanywi tu kama kununua nyanya ni kazi kubwa ambayo inahitaji muda wa kufanya analysis ya vitu mbalimbali kutoka kwa manufacture mbalimbali conclusion ya analysis ndo itatuonyesha ni vifaa vipi tuchukua

Suala la bodi

Tutateua bodi yenye watu kadha ambao wataifikisha kampuni pale ambapo inapasa kufika.Bodi itaundwa na watu wenye utaalamu wa mambo mbalimbali si tu kwenye uzalishaji wa madirisha

Ni makundi kama haya ni vizuri yanakuwa na independent audit
 
How do we join of create this group, am interested

Kwa sasa serious people basi watume email zao kwenye pm -idadi itakapofikia kubwa basi tutaanza kufanya mikutano au kukutana live na kila mtu.Kupitia email zenu tutawatumia updates zote.Asanteni
 
Suala la kuwa grouped si tatizo kwanza tunatakiwa tujiorganized tukishajua idadi ya watu walio tayari then tutaanzisha kampuni.Kampuni ikishakuwa tayari pamoja na lisense zote basi suala la pili litakuwa ni feasibility study pamoja na mchanganyuo mzima wa biasharasitaki kuahidi itachukua muda gani hii kitu naweza nikaihandle kushirikiana na watu wengine wachache kutoka kwenye kikundi.Baada ya mchanganyuo ambao ningependa tuungeneneze katika hatua(phase) basi tutaanza suala la kutumbukiza pesa.Idadi ya pesa itakayopataika itatupa picha tuanzie wapi na kitu gani kinapungua na kama je tutahitaji msaada mwingine kutoka kwa wawekezaji wakubwa haya yote yatakuwa ni matoke ya mchanganyuo wa biashara yote
Pia suala la uchagua wa vifaa halifanywi tu kama kununua nyanya ni kazi kubwa ambayo inahitaji muda wa kufanya analysis ya vitu mbalimbali kutoka kwa manufacture mbalimbali conclusion ya analysis ndo itatuonyesha ni vifaa vipi tuchukua

Suala la bodi

Tutateua bodi yenye watu kadha ambao wataifikisha kampuni pale ambapo inapasa kufika.Bodi itaundwa na watu wenye utaalamu wa mambo mbalimbali si tu kwenye uzalishaji wa madirisha

Ni makundi kama haya ni vizuri yanakuwa na independent audit

Mkuu tunakushukuru sana, nimejaribu kusoma CVS zako inaonekana una uzoefu mkubwa katika masuala haya na sina shaka una picha kamili ni nini kinahitajika na wapi kitapatikana kwa bei gani and what have you - in otherwords unaonekana umekwisha fanya homework ya kutosha; sasa unapo sema tena kwamba utafanya brain storming na potential share holders una maana GANI?
 
Nashukuru ndugu yangu kwa mchango wako kwa faida pia ya watu wengine wacha nielezee kwa undani zaidi
Tukianza na suala la vifaa vya uzalishaji wapi na kwa kiasi gani vinapatikana .Kabla hatujafika huko wacha tuangalia mambo mawili matatu juu ya vifaa vya uzalishaji wa madirisha.
Ukiangalia soko la vifaa vya madirisha vingi vinatoka Germany, Italy, Turkey, Spain, China and Russia
Kwa ughali wa vifaa vingi vinatoka Ulaya magharibi na hasa Ugermani na vinavyofuata vifaa bei yake ya chini vinatoka Uturuki,Urusi,China.Vifaa vya Uturuki mara nyingi vina utofauti mkubwa sana kutoka nchi nyingine kwa kiwango,bei na pia muundo wake.Na hata kwa Uturuki kwenyewe pia kumegawanyika watengenezaji wakubwa wapo Istambuli na pia kuna utitiri mkubwa sana wa watengenezaji wadogo wadogo
Ukija kwenye ubora wa vifaa vingi vya Kichina –ubora wao ni wa kiwango cha chini sana
Na katika masoko ya vifaa vya uzalishaji mara nyingi utapata vipya au mtumba na kila mojawapo hayo ina faida na hasara zake

Faida na hasara za vifaa vipya

1)Mara nyingi viwango vyake vya juu
2)Durability yake pia ni ya muda mrefu bila kuwa na breakdown
3)Haili umeme mwingi hivyo kupekea cost za uzalishaji kuwa wa chini..
4)Upatikani wa bidhaa zenye kiwango na ubora wa juu

Hasara za vifaa vipya:

1)Mara nyingi kutokana na gharama zake zinapelekea gharama za mradi pia kuwa kubwa
2)Mara nyingi hivi vifaa vinakuja na warrant-warant ni nzuri ila kuna kipindi kunapotokea breakdown kubwa basi lazima kazi isimame mpaka atakapokuja mtaalam na kama ikitokea mtalaam yupo nchi nyingine basi ni shida zaidi ya shida wakati kumbe issue yenyewe ilikuwa ni dakika 20

VIFAA VYA MTUMBA

1)Mara nyingi ni bei rahisi na hasa ukivitafupa sehemu mbalimbali za ulaya kuna watu unakuta wanaviuza na hali yake pia huwa si mbaya
2)Mbali ya kuwa ni bei rahisi pia unaweza kupata option ambayo utendaji wake wa kazi ni wa hali ya juu kuliko hata vifaa vipya ukilinganisha na pesa uliyotumia

Hasara zake:

1)Mara nyingi unaweza kujikuta unanunua mbuzi ndani ya gunia kumbe mbuzi si mbuzi
2)Kuna wakati kuna kuwa na complex nyingi kwenye ufungaji wa mitambo yake na sababu kubwa unaweza kukuta hazina instruction documents au instructions zake hazijatimia
3)Kuna kipindi zinapunguza uwezo wa kufunga mitambo na hasa linapoingia suala la spareparts mpya kwa mfano mdogo tuchukua mtambo umenunua ni wa zamani sana na kiwanda kilisha acha kutengeneza aina hiyo ya mitambo kwa hivyo inakuwa shida kufanga mitambo mipya
Kw hivyo upatikani wa vifaa kwanza utategemea na nguvu yetu sisi wenyewe kwa mfano leo tukiwa watu kumi tu kwenye kikundi kwa vyovyote vile lazima tuendelee na wazo letu mpaka mwisho ila itatubidi kuchukua vifaa kutokana na nguvu yetu inavyoturuhusu ila na kama tutahitaji vifaa vyenye uwezo mkubwa wa uzalishaji na nguvu yetu ndi ndogo basi kwa vyovyote vile inawezekana hii inaweza kuwa kwa kuwafutia investor wengine ambao wataingia kwa mfumo wa equity hawa pia wapo lakini hili suala ni la mwisho na sit u suala la mwisho ili ni kama option kwani nia yangu kwa kila kitu kimilikiwe na sisi wenyewe kuanzia mwanzo mpaka mwisho
Kwa mafano labda baada ya miaka mitatu kama litaibuka suala la kutaka kujipanua zaidi kibiashara ili kukidhi sehemu mbalimbali basi pia kuna milango mingi na hata ikipidi kuipeleka kampuni punlic pia nayo inawezekana lakini hilo litakuwa suala la makubaliano ya main share holders ambao ni sisi

MAKADIRIO YA BEI ZA VIFAA VYA UZALISHAJI

Kiwanda kikubwa kabisa kinaweza kuanzia mpaka dola 100000 za kimarekani.Vilevile mwanzoni tunaweza hata tukaanza na kiwanda kidogo chenye samani kama ya dola elfu kimi na tano
Kwa mfano waturuki wanavifaa bora kabisa tukichukua complete line inaweza kugharimu kama dola 45000
Pia hatupaswi kusahau raw materials:
Vioo,PVC profile,fitting and seals kwa hizi raw materials basi hata tukizichukua china hakuna mbaya
Baada ya hapo llazima ikimbukwe kuna suala la gharama la uendeshaji wa kiwanda
Lazima ipatikane sehemu isiyozodi ukubwa wa metre square 200 pia na watu wasio zidi 10 ukijumlisha wengine kadhaa kama wahasinu,wakurugenzi walinzi nk

Huu ni mfano mdogo tu ila suala la bei kamili na wapi pakupatikana linaongozwa na mwongozo wa biashara ambao utaandaliwa baadae


Jambo la mwisho vifaa vimegawanyika katika makundi mbalimbali vipi ambazo vinauwezo wa kuzalisha madirisha 15,25,35,60 mpaka 100 kwa siku lakini kwa kawaida idadi haiwezi kutimia kwa kuwa kwa siku kuna mambo mengi yanayoweza kuiterfere process nzima kwa mfano umeme ulikatika kwa masaa mawili,kuna mfanya kazi kafiwa na mototo au matatizo yoyote

Tukichukua mfano wa madirisha 100 kwa siku basi kwa siku 26 za mwezi kiwanda kitazalisha madirisha 2600X BEI ya wakati huo=
Pia kiwanda kinaweza kufanya kazi kwa shift pia ya usiku kama oda ni nyingi-kwa hivyo kwa mwezi 2600 windows x 2=
 
Mkuu tunakushukuru sana, nimejaribu kusoma CVS zako inaonekana una uzoefu mkubwa katika masuala haya na sina shaka una picha kamili ni nini kinahitajika na wapi kitapatikana kwa bei gani and what have you - in otherwords unaonekana umekwisha fanya homework ya kutosha; sasa unapo sema tena kwamba utafanya brain storming na potential share holders una maana GANI?


Kaka nimekujibu hapo chini
 
Mada yako kassamali ni nzuri na inafunza mengi kitu ambacho nimekuwa nakifikiria mara kwa mara na hata kushawishika kuweka mada lakini nikawa sijajituma nikaweka kiporo.

Mtindo wa kwenda kwa fundi akutengenezee frames za milango na kisha shutters za milango hata madirisha imeshapitwa na wakati, enzi za leo ni za kila unapohitahi unatakiwa kwenye kwenye maduka yanayouza vifaa na zana za ujenzi ambako unapata kila kitu.

Kinachotakiwa ujenzi ufuate mfumo wa vipimo vya kiwango vya kimataifa measurements kwa milango ya kawaida nyumba za kifamilia na ile milango double ambayo hutumika kwa public buildings. Hali kadhalika kuna vipimo vya madirisha ambavyo kama mafundi wajenzi watakuwa makini watafuata vipimo vinavyokubalika ambayo havitasumbua katika door and window frame fitting.

Faida yake ni kwamba, milango na madirisha ambavyo huzalishwa viwandani ni bei nafuu zaidi kuliko ya kuagiza kwa fundi. Viwandani hufanya kwa wingi kwa wakati mmoja na hivyo kuokoa gharama za labor tofauti na kuagiza kwa fungi itachukua gharama kubwa ya labor. Pia uhitaji wa haraka huwa vigumu kwa amfungi wa mitaani tofauti na viwandani ambapo bidhaa hiyo huwa tayari kwenye maduka ya usambazaji.

Kwa vyo vyote kuna umuhimu wa mada yako hii ambapo tunahitaji:
  1. Frame za Milango mikubwa na midogo
  2. Shutters za milango ya aina zote
  3. Frame za madirisha kwa size zote
  4. Shutters za madirisha sizi zote.
 
Back
Top Bottom