Fursa kwenye sekta ya elimu. Walimu tunakwama wapi kutengeneza hela kubwa?

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Oct 11, 2019
207
482
Kuna dhana kwamba sekta ya elimu ni sekta isiyo na pesa. Kuweka maisha yako kwenye elimu ni kutafuta umaskini, walimu na wadau wa elimu ni wanyonge na watu wanaodhaurika na wanapuuzwa sababu wanaonekana ni watu wenye kipato duni.

Mimi ni mwalimu professionally na nimefundisha kwa muda mrefu baadae nikaamia kwenye miradi ya elimu yenye ufadhili wa wageni. Kwa uzoefu wangu kuna kitu nimejifunza.

Nataka tujadili kidogo kwa nini walimu hatutengenezi pesa kupitia elimu.

Ni kweli kwenye sekta ya elimu hakuna fursa mpya zaidi ya kushika chaki?

Ukiangalia mashule mengi yanaanzishwa na watu baki. Why sio walimu?

Innovation kubwa kwenye elimu zinafanywa na watu baki. Why sio walimu? Shule direct, Mtabe, Ubongo kids hazijaanzishwa na walimu.

Ingia sasa kwenye miradi ya elimu asili mia kubwa inasimamiwa na watu wengine kabisa. Walimu hawaonekani wao wapo mashuleni wanashika chaki.

Kina Nyambari walijaribu wakapiga hela lakini nao wamepotea siku hizi.
Mwalimu akitaka kuinvest basi ataanzisha twisheni center, atengeneze kitini au ataacha ualimu akafungue genge.

Kwa nini watu hatuwekezi uwekezaji mkubwa kwenye elimu au hakuna fursa?
Sekta ya elimu haiwezi tengeneza watu wenye pesa nyingi?
 
sikiliza jamaa,
kuna headmaster mmoja kwa sasa ni marehemu ,alikua anaheshimika sana pale wizarani alijenga shule yake pale ukonga katika harakati za kutaka kusajili,walimwambia hatukupi usajili mpaka ukistaafu ,maana tukikupa usajili utatukimbia,
masikini yule headmster mpaka anafariki alikua hajastaafu na alishindwa fngua ile shule yake kwa sasa familia imegeuza yale madarasa kuwa vyumba vya kupangisha,achana na sekta ya elimu ,ningumu sana kutoboa aisee.
 
I'm speachless
 
Investment ya kwenye elimu siyo lele mama...

Assets, man power and resources (Stationeries) its not a joke...

Cc: mahondaw
Hapana sikubaliani na wewe, kuna investment haziitaji mtaji mkubwa. Nimetoa mfano wa elimu kwa njia ya technology wawekezaji sio walimu wakati walimu ndio wana content pana.
Uwezi sikia hata mwl anakuwa consultant wa mambo ya elimu wakati uwezo wengi wanao.
 
Ninaamini mwalimu ni mtu mkubwa NA mwenye kuweza kuleta mabadiliko ndani ya jamii ila kuna kasumba moja ambayo tunayo na hii ndiyo imekuwa msiba wa kuweza kutuzuia kufikia malengo tunayoyahitaji

Ushirikiano duni miongoni mwetu yaani mmoja anaweza kuja na wazo la biashara zuri kabisa na akawashirikisha wengine lakini shida inakuja pale ambapo anahitaji support ya wamzungukao ili kuweza kufikia lengo wataridhia mdomoni ila myoyoni hawako na wewe zaidi ya 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dhana kwamba sekta ya elimu ni sekta isiyo na pesa. Kuweka maisha yako kwenye elimu ni kutafuta umaskini, walimu na wadau wa elimu ni wanyonge na watu wanaodhaurika na wanapuuzwa sababu wanaonekana ni watu wenye kipato duni.

Mimi ni mwalimu professionally na nimefundisha kwa muda mrefu baadae nikaamia kwenye miradi ya elimu yenye ufadhili wa wageni. Kwa uzoefu wangu kuna kitu nimejifunza.

Nataka tujadili kidogo kwa nini walimu hatutengenezi pesa kupitia elimu.

Ni kweli kwenye sekta ya elimu hakuna fursa mpya zaidi ya kushika chaki?

Ukiangalia mashule mengi yanaanzishwa na watu baki. Why sio walimu?

Innovation kubwa kwenye elimu zinafanywa na watu baki. Why sio walimu? Shule direct, Mtabe, Ubongo kids hazijaanzishwa na walimu.

Ingia sasa kwenye miradi ya elimu asili mia kubwa inasimamiwa na watu wengine kabisa. Walimu hawaonekani wao wapo mashuleni wanashika chaki.

Kina Nyambari walijaribu wakapiga hela lakini nao wamepotea siku hizi.
Mwalimu akitaka kuinvest basi ataanzisha twisheni center, atengeneze kitini au ataacha ualimu akafungue genge.

Kwa nini watu hatuwekezi uwekezaji mkubwa kwenye elimu au hakuna fursa?
Sekta ya elimu haiwezi tengeneza watu wenye pesa nyingi?
Mkuu, Naeza pata nafasi ya Intern au volunteer kwenye hiyo Mirad. Maana hali sio poa Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wako wangapi na miradi ni mingapi? Kwa mfano ubongo kids ina crew ya watu wangapi wanaotoa misingi ya uwalimu?nainaga wazungu zaidi kule, wengine ni wasanii tu wa sauti na wataalamu wa multimedia na vinginevyo.

Pia jua elimu yetu inayotolewa na serikali ni mfu haina upana na haimpi mtu kuwa na creativity, ulimwengu wa sayansi huu, kila kitu ni tech, walimu kwenye ttc kule wanajifunza teaching aid kwa miti na makaratasi na vitambaa, maharagwe na mahindi. How will they be able to change that kuwa modern wakati hata masomo ya komputer huko vyuoni ni kujua kuwasha na kuzima tu mashine?

Tatu uwekezaji wa elimu ni ghari sana. Mathalani unataka kuandika app inayoweza msaidia mtoto kusoma, utahtaji kuwa na mtaalamu wa IT na wengine watakao intergrate ideas zako na tech, ni gharama, uchapishaji wa vitabu ni gharama kinyume chake soko unalotegemea kuuza huo ujuzi wako halipo definite na lipo saturated na unproffesional rubbish kibao zisizokuwa controlled. Watanzania hawajua elimu wala hawaipi thamani yake.

Nakupa mfano mwalimu mmoja maarufu Wa Geography ilikuwa inamlazimu kutembea mashuleni kuuza vitabu vyake, na ananunua mtu mmoja tena kwa kulia, kitabu cha elfu 30 anataka kwa elfu 3. Unauza kimoja vilivyobaki watu wanapiga kopi

Lakini saizi ni nani ana haja na material ya ubunifu wa elimu? Wewe si unafanya kazi kwenye sector ys elimu? Au hujui? Mwaka 2013, niliandaa DVD ya clips za picha zinazotembea physical geography, zikionesha vitu kwa uhalisia. Mfano mwanafunzi anaposikia volcano eruption, kwenye ile DVD anaona video kwa uhalisia.
Ili cover phycal geography yote, ukisoma stages of the river, mpk delta, types of rocks ile DVD ilionesha kwa uhalisi sio michoro.

Nilifanya hivi kuwasaidia wanafunzi wangu, na nikaenda shuleni kuitoa buree, ispokuwa tu kila mmoja alitakiwa aje na CD empty na tsh 500 ya ku burn, waliotaka zikiwa tayari niliwaambia wachangie 1500 tu. Kwakuwa nilitaka tu kufaulisha zaidi sio kupata fedha. I tell you. Walinunua wanafunzi watano tu kati ya 120 plus

kwahiyo Mazingira yetu, watu wetu, serikali nk nk ni tatizo kubwa katika kukuwa kwa sekta ya elimu na hii imeuwa walimu wengi na ubunifu japo kidogo uliopo, wengi sasa wanasubiri mishahara tu maisha yasonge aghalabu wachache wana miradi yao nje ya Elimu
Hapana sikubaliani na wewe, kuna investment haziitaji mtaji mkubwa. Nimetoa mfano wa elimu kwa njia ya technology wawekezaji sio walimu wakati walimu ndio wana content pana.
Uwezi sikia hata mwl anakuwa consultant wa mambo ya elimu wakati uwezo wengi wanao.

Dumelang
 
Walimu wako wangapi na miradi ni mingapi? Kwa mfano ubongo kids ina crew ya watu wangapi wanaotoa misingi ya uwalimu?nainaga wazungu zaidi kule, wengine ni wasanii tu wa sauti na wataalamu wa multimedia na vinginevyo.

Pia jua elimu yetu inayotolewa na serikali ni mfu haina upana na haimpi mtu kuwa na creativity, ulimwengu wa sayansi huu, kila kitu ni tech, walimu kwenye ttc kule wanajifunza teaching aid kwa miti na makaratasi na vitambaa, maharagwe na mahindi. How will they be able to change that kuwa modern wakati hata masomo ya komputer huko vyuoni ni kujua kuwasha na kuzima tu mashine?

Tatu uwekezaji wa elimu ni ghari sana. Mathalani unataka kuandika app inayoweza msaidia mtoto kusoma, utahtaji kuwa na mtaalamu wa IT na wengine watakao intergrate ideas zako na tech, ni gharama, uchapishaji wa vitabu ni gharama kinyume chake soko unalotegemea kuuza huo ujuzi wako halipo definite na lipo saturated na unproffesional rubbish kibao zisizokuwa controlled. Watanzania hawajua elimu wala hawaipi thamani yake.

Nakupa mfano mwalimu mmoja maarufu Wa Geography ilikuwa inamlazimu kutembea mashuleni kuuza vitabu vyake, na ananunua mtu mmoja tena kwa kulia, kitabu cha elfu 30 anataka kwa elfu 3. Unauza kimoja vilivyobaki watu wanapiga kopi

Lakini saizi ni nani ana haja na material ya ubunifu wa elimu? Wewe si unafanya kazi kwenye sector ys elimu? Au hujui? Mwaka 2013, niliandaa DVD ya clips za picha zinazotembea physical geography, zikionesha vitu kwa uhalisia. Mfano mwanafunzi anaposikia volcano eruption, kwenye ile DVD anaona video kwa uhalisia.
Ili cover phycal geography yote, ukisoma stages of the river, mpk delta, types of rocks ile DVD ilionesha kwa uhalisi sio michoro.

Nilifanya hivi kuwasaidia wanafunzi wangu, na nikaenda shuleni kuitoa buree, ispokuwa tu kila mmoja alitakiwa aje na CD empty na tsh 500 ya ku burn, waliotaka zikiwa tayari niliwaambia wachangie 1500 tu. Kwakuwa nilitaka tu kufaulisha zaidi sio kupata fedha. I tell you. Walinunua wanafunzi watano tu kati ya 120 plus

kwahiyo Mazingira yetu, watu wetu, serikali nk nk ni tatizo kubwa katika kukuwa kwa sekta ya elimu na hii imeuwa walimu wengi na ubunifu japo kidogo uliopo, wengi sasa wanasubiri mishahara tu maisha yasonge aghalabu wachache wana miradi yao nje ya Elimu

Dumelang
Hongera sana mkuu.....
Hii kitu bado unayo? Nawezaje kuipata kama bado unayo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sikiliza jamaa,
kuna headmaster mmoja kwa sasa ni marehemu ,alikua anaheshimika sana pale wizarani alijenga shule yake pale ukonga katika harakati za kutaka kusajili,walimwambia hatukupi usajili mpaka ukistaafu ,maana tukikupa usajili utatukimbia,
masikini yule headmster mpaka anafariki alikua hajastaafu na alishindwa fngua ile shule yake kwa sasa familia imegeuza yale madarasa kuwa vyumba vya kupangisha,achana na sekta ya elimu ,ningumu sana kutoboa aisee.
Wenye vyeo huko idara ya elimu wanachuki hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa za kielimu siyo lazima ziendeshwe na walimu tu, hiyo mifano ulotupa ya shule direct n.k lazima walimu wamehusika.
Walimu tuko sana limited shule shughuli nyingi kwa mfano unakuta mwl mmoja anafundsha form one hadi four, afu marupurupu hakuna, anaishi mtaani amepanga, anasafiri n.k mishahara iko chini tofauti na sekta nyingne ndo maana tunaishia kumiliki madeni tu.
Afu pia viongozi wa kielimu wana urasimu na kujuana kwingi, usipojipendkeza halmashauri ndo utaishia kula vumbi tu shuleni.
Binafsi nna mpango wa kuangalia fursa kwenye kilimo na ufugaji asee ualimu kwa maeneo fulani ni mgumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu wako wangapi na miradi ni mingapi? Kwa mfano ubongo kids ina crew ya watu wangapi wanaotoa misingi ya uwalimu?nainaga wazungu zaidi kule, wengine ni wasanii tu wa sauti na wataalamu wa multimedia na vinginevyo.

Pia jua elimu yetu inayotolewa na serikali ni mfu haina upana na haimpi mtu kuwa na creativity, ulimwengu wa sayansi huu, kila kitu ni tech, walimu kwenye ttc kule wanajifunza teaching aid kwa miti na makaratasi na vitambaa, maharagwe na mahindi. How will they be able to change that kuwa modern wakati hata masomo ya komputer huko vyuoni ni kujua kuwasha na kuzima tu mashine?

Tatu uwekezaji wa elimu ni ghari sana. Mathalani unataka kuandika app inayoweza msaidia mtoto kusoma, utahtaji kuwa na mtaalamu wa IT na wengine watakao intergrate ideas zako na tech, ni gharama, uchapishaji wa vitabu ni gharama kinyume chake soko unalotegemea kuuza huo ujuzi wako halipo definite na lipo saturated na unproffesional rubbish kibao zisizokuwa controlled. Watanzania hawajua elimu wala hawaipi thamani yake.

Nakupa mfano mwalimu mmoja maarufu Wa Geography ilikuwa inamlazimu kutembea mashuleni kuuza vitabu vyake, na ananunua mtu mmoja tena kwa kulia, kitabu cha elfu 30 anataka kwa elfu 3. Unauza kimoja vilivyobaki watu wanapiga kopi

Lakini saizi ni nani ana haja na material ya ubunifu wa elimu? Wewe si unafanya kazi kwenye sector ys elimu? Au hujui? Mwaka 2013, niliandaa DVD ya clips za picha zinazotembea physical geography, zikionesha vitu kwa uhalisia. Mfano mwanafunzi anaposikia volcano eruption, kwenye ile DVD anaona video kwa uhalisia.
Ili cover phycal geography yote, ukisoma stages of the river, mpk delta, types of rocks ile DVD ilionesha kwa uhalisi sio michoro.

Nilifanya hivi kuwasaidia wanafunzi wangu, na nikaenda shuleni kuitoa buree, ispokuwa tu kila mmoja alitakiwa aje na CD empty na tsh 500 ya ku burn, waliotaka zikiwa tayari niliwaambia wachangie 1500 tu. Kwakuwa nilitaka tu kufaulisha zaidi sio kupata fedha. I tell you. Walinunua wanafunzi watano tu kati ya 120 plus

kwahiyo Mazingira yetu, watu wetu, serikali nk nk ni tatizo kubwa katika kukuwa kwa sekta ya elimu na hii imeuwa walimu wengi na ubunifu japo kidogo uliopo, wengi sasa wanasubiri mishahara tu maisha yasonge aghalabu wachache wana miradi yao nje ya Elimu

Dumelang
Ulikuwa una idea nzuri lakini ukakata tamaa mapema, endelea kudevelop wazo lako na ulisimamie. Lifanye kwa ukubwa litakutoa.
 
Write your reply...mda upo nahangaika na business zangu nafundisha nikipenda mitoto yenyewe INA dharau mazingira na vitendea kazi vibovu
 
Kuna dhana kwamba sekta ya elimu ni sekta isiyo na pesa. Kuweka maisha yako kwenye elimu ni kutafuta umaskini, walimu na wadau wa elimu ni wanyonge na watu wanaodhaurika na wanapuuzwa sababu wanaonekana ni watu wenye kipato duni.

Mimi ni mwalimu professionally na nimefundisha kwa muda mrefu baadae nikaamia kwenye miradi ya elimu yenye ufadhili wa wageni. Kwa uzoefu wangu kuna kitu nimejifunza.

Nataka tujadili kidogo kwa nini walimu hatutengenezi pesa kupitia elimu.

Ni kweli kwenye sekta ya elimu hakuna fursa mpya zaidi ya kushika chaki?

Ukiangalia mashule mengi yanaanzishwa na watu baki. Why sio walimu?

Innovation kubwa kwenye elimu zinafanywa na watu baki. Why sio walimu? Shule direct, Mtabe, Ubongo kids hazijaanzishwa na walimu.

Ingia sasa kwenye miradi ya elimu asili mia kubwa inasimamiwa na watu wengine kabisa. Walimu hawaonekani wao wapo mashuleni wanashika chaki.

Kina Nyambari walijaribu wakapiga hela lakini nao wamepotea siku hizi.
Mwalimu akitaka kuinvest basi ataanzisha twisheni center, atengeneze kitini au ataacha ualimu akafungue genge.

Kwa nini watu hatuwekezi uwekezaji mkubwa kwenye elimu au hakuna fursa?
Sekta ya elimu haiwezi tengeneza watu wenye pesa nyingi?

Hao walimu ungewahamisha TRA, BOT, TANAPA na wa Taasisi hizi ungewapeleka kwenye Ualimu majibu yangekua the same.

Kule TRA wanakutana na wafanyabiashara ama watu wa kampuni wenye access, connection, exposure hawa ndio wateja wao, walimu wanakutana na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom