Fursa kwenye jamii inayokuzunguka

Fursa kwenye jamii inayokuzunguka

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Hamjambo waungwana!

Fursa

Nimepata nafasi ya kusikiliza kwa makini kaka yangu Ruge alipokuwa akichambua fursa alizozibaini katika kuzunguka kwake Tanzania nzima – hakika huyu kaka yangu anautumia vyema muda wake katika kufuatilia mambo ya maana yanayoweza kusaidia kizazi hiki na kijacho.

Labda kwa faida ya wale ambao hawakupata nafasi ya kumsikiliza (ni zamani kidogo 2016) alitaja fursa hizo kwa mtindo wa kuanzia ya kumi akielekea ya kwanza kama ifuatavyo:-

1. Technolojia ya habari na mawasiliano (ikiwa ndo namba 10) sikujua ni kwa nini haliipa namba kumi – kiukweli teknolojia inasimamia karibia kila fursa.

2. Huduma za fedha – (9)

3. Urembo / fashion

4. Usambazaji na usafirishaji

5. Uwekezaji kwenye majengo (real estate)

6. Huduma / biashara za kijamii (social business)

7. Media & entertainment

8. Chakula

9. Retail – E commerce

10. Agribusiness – hii ndiyo iliyokuwa nambari moja kwake.

Wakati akizitaja hizo fursa alikuwa akitoa mifano mingi tu ambayo kwa uhakika mtu ukijipanga unaweza kuzifanyia kazi na zikakusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Kuna namna alivyonijenga kwenye kuweza kufuatilia mambo, ila kikubwa zaidi ni kwamba .. kila mtu ana mtazamo wake. Alichokiona cha nambari kumi huenda wewe msomaji ukakiona ndo kilipaswa kuwa nambari moja au namba nyingine.

Alipomaliza tu! nafsini mwangu kukaibuka swali hili … “ELIMU SIO FURSA?”

Hapo nikamkumbuka mwalimu wa somo la CHAKULA CHA AKILI aliposema watu wote hatuwezi kuwaza sawa … na utofauti wetu kimawazo ndiyo jambo linalofanya maendeleo yawepo. Kukubaliana kwetu kwa kila jambo (pasipo upinzani) ndicho kikwazo kikubwa sana kwenye maendeleo yetu.

Fursa zote alizozitaja kaka yangu, bila elimu ni bure. Popote pale utakapogusa pasipo kutanguliza elimu lazima ukwame tu. Naiona fursa ya elimu kama nambari moja kwa sababu zifuatazo:-

1. Idadi kubwa ya watanzania ni wavivu wa kusoma .. hivyo kuwekeza kwenye kuwafundisha ili kwanza wabadili mtazamo ni fursa kubwa sana.

2. Elimu ni fursa nambari moja kwa sababu hakuna siku hata moja itakayotokea watu wote wakajua mambo yote. Fursa ya elimu haichuji.

3. Mambo yote hayo kumi yanabadilika na kinachoyafanya yabadilike ni elimu. Mfano – yale majengo marefu yaliyojengwa miaka ya 1970/80 - kwa sasa hivi baada ya teknolojia kubadilika yanaonekana kama uchafu tu kwenye miji.
 
Sawa zote ni fursa ila kitu muhimu ni "initial capital" ndokinacho tusumbua hayo yote tunavijua
 
Sawa zote ni fursa ila kitu muhimu ni "initial capital" ndokinacho tusumbua hayo yote tunavijua
Unamaanisha nini unaposema initial capital?
Kwa mfano nikuulize ukitaka kuanzisha biashara ya nursery school hapo ulipo jambo la kwanza unapaswa kuwa na nini?
 
Unamaanisha nini unaposema initial capital?
Kwa mfano nikuulize ukitaka kuanzisha biashara ya nursery school hapo ulipo jambo la kwanza unapaswa kuwa na nini?
INITIAL CAPITAL=MTAJI WA KIANZIO
 
INITIAL CAPITAL=MTAJI WA KIANZIO
Sikuhitaji tafsiri, mtaji wa kuanzia unao tayari, ndo maana nilitaka kuuliza unamaanisha nini?
1. Una uhai, una afya, una maarifa, una watu ... nchi yako tajiri .. mtaji upi wa kuanzia huo?
 
Sikuhitaji tafsiri, mtaji wa kuanzia unao tayari, ndo maana nilitaka kuuliza unamaanisha nini?
1. Una uhai, una afya, una maarifa, una watu ... nchi yako tajiri .. mtaji upi wa kuanzia huo?
HAPO BILA PESA HAMNA KITU
 
Unamaanisha nini unaposema initial capital?
Kwa mfano nikuulize ukitaka kuanzisha biashara ya nursery school hapo ulipo jambo la kwanza unapaswa kuwa na nini?
KODI, OSHA FEES, KODI YA ARDHI, JENGO, USAJILI WA KAMPUNI n.k
 
images


Baadhi ya fursa hapo zinahitaji capital kubwa
Baadhi naona ni ngumu sana ku predict profit yake.
Hiyo namba 1 ya Ruge(10) kwako mimi naipa namba 1 tena.

Kama mnataka Mali,mtazipata shambani.
 
Sikubaliani na wewe hata kidogo ...
Tumia vile ulivyo navyo kwanza .. pesa baadaye mkuu! Ukitanguliza pesa mbele huipati kamwe!
sijakata ila pesa usiitoe kwenye initial capital

''una uhai, una afya, una maarifa, una watu ... nchi yako tajiri''>>>>>>hivi vitu ulivyosema vinahusiana na pesa huwezi ukavitumia bila ya pesa, achilia mbali pesa ya mtaji
 
KODI, OSHA FEES, KODI YA ARDHI, JENGO, USAJILI WA KAMPUNI n.k
Jambo la kwanza ni ujuzi / maarifa juu ya uendeshaji wa hiyo Nursery .. hayo mengine ni baadaye mkuu! Ukiwaza hayo kabla ... ina maana unawaza kukwama! na utakwama kweli kweli.
Kuna watu nawafahamu kabisa walianzisha shule kwenye nyumba walizokuwa wakiishi ...
Kuna kijana mwingine ameanzisha chini ya mti na sasa hivi anaendelea vizuri ... kinachotakiwa ni kuanza .. mengine yanawahusu watakaoleta watoto wao.
 
Uko
images


Baadhi ya fursa hapo zinahitaji capital kubwa
Baadhi naona ni ngumu sana ku predict profit yake.
Hiyo namba 1 ya Ruge(10) kwako mimi naipa namba 1 tena.

Kama mnataka Mali,mtazipata shambani.
Uko sahihi kabisa mkuu!
 
Unaoongelea hapa "hope" tuu...uhalisia sio rahisi kama maneno yako!
Uko sahihi kwa ile hali uliyoizoea ...
Hauko sahihi kwa ile hali ambayo hujaizoea ...
Toka katika ukawaida wako .. utaona uraisi wa kile ninachokiongea.
 
Uko sahihi kwa ile hali uliyoizoea ...
Hauko sahihi kwa ile hali ambayo hujaizoea ...
Toka katika ukawaida wako .. utaona uraisi wa kile ninachokiongea.
Lugha tuu za mnaojifanya ni inspirational speakers tuu hizi..... theories tuu na quotes ......uhalisia ndio changamoto!
 
Lugha tuu za mnaojifanya ni inspirational speakers tuu hizi..... theories tuu na quotes ......uhalisia ndio changamoto!
Mimi sijifanyi, naongea kitu ambacho ni real ...
Ndugu ukianza jambo ndo njia zinafunguka zaidi ... nikupe mfano tu wa kawaida.
Nilianza majaribio ya Hydroponics .....
Kila nilipokwama ndo hapo nilitafuta ufunguzi ...
Kwa kuanza niliona kwenye mitandao namna wakenya wanavyostawisha mbogamboga bila udongo ... kifaa walichokuwa wakitumia bei yake iko juu na kinapatikana Kenya - Nairobi na kwa hapa Tanzania nimeulizia kinapatikana Arusha ... baada ya kuona sina hiyo hela ya kununua hicho kitu niliamua kutumia mifuko ya sementi ambayo niliikusanya kwenye sites bure .... nia ilikuwa ni kuotesha mbogamboga ... nilifanikiwa na hadi sasa naendelea ..
Baada ya hapo nikaingia kwenye kuzalisha chakula cha mifugo aina ya H-Fodder ... tatizo likawa ni trei za alminium - sheet moja ni Tshs. 70,000/= sikuwa na hiyo hela ya kutosha trei 30 za kuanzia ... ilibidi nijiongeze .. nikatumia madumu ya plastiki kwa kuanza ... wateja walipopatikana nikapata hela nikanunua trei ....
Siandiki haya kujisifia bali kuonesha kuwa moyo wa kuanza ndo kila kitu ... ingia kwenye website yangu uone kinachoendelea www.mwasenda.org
Anayesema NAWEZA yuko sahihi ... anayesema SIWEZI yuko sahihi pia.
 
Back
Top Bottom