Fursa Barani Ulaya kwa wajasiriamali wa Kitanzania.

jembelamkono

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
2,733
2,005
Modes naomba muulinde Uzi huu,nia na madhumuni kuanzisha thread hii ni kuwafungua macho wafanyabiashara na wajasiriamali wa Kitanzania juu ya fursa za biashara ndogondongo na za kati kati ya Ta zania na bara Ulaya.

Katika pitapita zangu kwenye masoko ambayo ni maarufu kwa watumiaji wa mwisho/walaji(major super markets),nitakuwa naweka bidhaa ambazo zinapatikana kwa wingi Tanzania lakini kwa Ulaya zina soko/bei nzuri.

Nitajaribu pia kuangalia vigezo kama ubora uhitajika,ufungashaji,bei,ladha (kwa uzoefu wangu wa bidhaa za nyumbani ukilinganisha na bidhaa zilipo sokoni hapa Ulaya) na bei pia.

NOTE;
Nita base sana kwenye washindani wengine wa kibiashara na soko letu la nyumbani.
Hapa namaanisha nitawekabidhaa ambazo zimetoka kwenye nchi mbalimbali,
Nia nikujadili wao wamewezaje na sisi tunakwama wapi,ikiwa wote tunabidhaa sawa au pengine za nyumbani ni bora zaidi.

Ifahamike hapa tunafunguana macho juu ya fursa,hivyo kwa maelezo zaidi ewe mjasiriamali unaweza kufwatilia kwenye mamlaka husika.

Wadau wote mnaoonafursa kokota mlipo tupia hapa pengine inaweza kumsaidia mjasiriamali mmoja au zaidi.

KWA KUANZIA HEBU TUANGALIE BIDHAA ZIFUATAZO:

MAJANI YA CHAI/BLACK TEE KUTOKA RWANDA.

UJAZO:
100gm

PACKAGE :
Mfuko wa Karatasi wa Kaki.

CERTIFICATIO/VIBALI :
Fair trade na EU cert kwa Wazalishaji nje ya Ulaya.

BEI:
Euro 5.99 (takribani Tsh 15,000) kwa pakiti moja ya gm 100
Hii ni bei ya rejareja sokoni kwa nchi za Austria,Uswiss na Ujerumani.

UBORA (based kwa uzoefu wangu):
Haya kolei kwenye chai pia haya ladha nzuri kama tunazozipata kwenye chai bora n.k nadhani kutokana na kukaa kwa muda mrefu na kukaushwa sana.

PARACHICHI
NCHI :

Amerika ya kusini
UBORA :
Hazina nembo

UJAZO :
Kama zinavyo onekana kwenye picha hapo.

PACKAGE :
Unpackage/hazija pakiwa.
BEI : Euro 2 (takribani Tsh 5,000) kwa moja (Austria,Uswiss na Ujerumani)

UBORA.
Nyingi ni ngumu sana,na huwezi kulinganisha na parachichi zenye unga kutoka Marangu mwika,Machame,Mbeya au Bukoba.
Note:Ni ndogondogo kama zinavyo onekana kwenye picha hapo,na zote ni za rangi ya kijani hata zikiwa zimeiva sana,sielewi kwanini haswa.

20190416_122745.jpeg
20190416_123057.jpeg
20190416_193000.jpeg
20190416_192518.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran sana Mkuu kwa uzi mzuri. Mimi swali langu ni kwenye issue ya kodi unapoingiza mzigo huko Cost yake inarange vipi. Kuprint hzo details (kwnye package)najua sio shida. Tatzo linaweza kuja kwenye usafirishaji na kupata soko la uhakika ili usikae sana na mzigo.

Mkuu mimi sio mtaalamu wa maswala ya kodi,labda nilizungumzie tu kwa ufahamu wangu.Kama unavyoona hapo kwenye stika kuna nembo ya fair trade,naamini na sisi Tanzania tupo kwenye makubaliano na fair trade nafkiri kuna unafuu flani kwenye ku import ukiwa ndani ya fair trade,kikubwa umeet viwango vyao vya ubora.
Kwa maelezo zaidi ungefwatilia wizara ya kilimo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwenye viwango vya ubora kwanza ndipo tunapoanza kukwaa visiki maàna tulio wengi hatujui ni vipimo gani wanavitumia au sisi tupeleke wapi hizo bidhaa ili tuweze kupimiwa na kupewa hizo certificates kuidhinisha ubora wa bidhaa zetu.

Wengine wenye uelewa mkuje pia huku tupeane mawazo.

"Proudly, brought to u by Bachelor Sugu"
 
Safi sana mkuu, ni watanzania wachache sana wanaweza kutoa taarifa za namna hii.

Tafadhali naomba ukiweza ulizia bei ya organic passion fruit per kg, turmeric/bizari, tangawizi, vegetables kama French beens, sugar snaps, macadamia. Ukiweza pm au hapa ni sawa tuyajenge

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Narubongo,hapa kwenye passion na Macadamia nitafanya tathmini,lkn kwenye spieces naona wako vizuri,nyingi wanalima wenyewe na nyingi zaidi zinatoka Uturuki,kusema kweli raw passions sijaziona kwa wingi sokoni,Ukipata zile quality nyeusi za mbeya ambazo zimelimwa bila madawa naamini hapa lazima utusue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kwenye viwango vya ubora kwanza ndipo tunapoanza kukwaa visiki maàna tulio wengi hatujui ni vipimo gani wanavitumia au sisi tupeleke wapi hizo bidhaa ili tuweze kupimiwa na kupewa hizo certificates kuidhinisha ubora wa bidhaa zetu.

Wengine wenye uelewa mkuje pia huku tupeane mawazo.

"Proudly, brought to u by Bachelor Sugu"
Mkuu nenda wizara ya kilimo,ukiona wazee gozi gozi huwaelewi nenda Export processing zone pale External.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Narubongo,hapa kwenye passion na Macadamia nitafanya tathmini,lkn kwenye spieces naona wako vizuri,nyingi wanalima wenyewe na nyingi zaidi zinatoka Uturuki,kusema kweli raw passions sijaziona kwa wingi sokoni,Ukipata zile quality nyeusi za mbeya ambazo zimelimwa bila madawa naamini hapa lazima utusue.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuu. Hapa tz tunauwezo wa kuzalisha kila zao, tatizo wengi hawajui hatua za kufuata mpaka kukidhi ubora wa ulaya.

Mkuu waombe mod wauhamishie huu uzi jukwaa la kilimo, ufugaji ili usipotee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Narubongo,hapa kwenye passion na Macadamia nitafanya tathmini,lkn kwenye spieces naona wako vizuri,nyingi wanalima wenyewe na nyingi zaidi zinatoka Uturuki,kusema kweli raw passions sijaziona kwa wingi sokoni,Ukipata zile quality nyeusi za mbeya ambazo zimelimwa bila madawa naamini hapa lazima utusue.

Sent using Jamii Forums mobile app
Purple passion za njombe, mbeya zimejiotea zenyewe porini kwahiyo kuuza euro market ni ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeanza kuprocess moringa oreifela ikiwa imemixiwa na ginger; vipi soko la huko likoje? La hapa nchini hakuna shida.
 
Halafu mbona majani ya chai ya kawaida tuu. Ngwazi kuja majani mazuri sana
 
Kwa ambao wanataka kuuza bidhaa nchi za Umoja wa Ulaya, pitieni hii tovuti:

Halafu kuna hii taasisi: http://www.intracen.org/country/united-republic-of-tanzania/
Huwa wanakuwa na programu za kujengea uwezo biashara ndogondogo na za kati, ikiwemo kupitia madarasa ya kwenye mitandao (e-classes), hasa kwa vijana na kina mama.

Mfano: http://www.intracen.org/news/ITC-GroFin-issue-call-for-women-entrepreneurs-to-join-SheTrades-Invest/

Fursa ziko nyingi za kilimo-biashara, muhimu ni kufahamu wapi upate taarifa sahihi
 
Back
Top Bottom