Furahia uhondo wa Pride FM

Tundapori

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2007
Posts
652
Reaction score
277
Kwa ware wenye iPod, iPhone na iPad au smartphones zingine waweza kusikiliza mavituzi ya nyumbani kupitia radio iitwayo "Pride FM" toka Mtwara. Ni radio murua kabisa.

Download Application iitwayo "Tune In Radio" na search radio za Tanzania. Utapata Pride FM, radio Maria na Clouds FM. Ni radio nzuri kwa kujikumbushia vitu vya nyumbani hasa kwa wale walio ughaibuni. Utapata miziki na taarifa za habari live kabisa.
 
Hivi ni kwavile 'amechapia' kusema 'ladio' kuna watu wengi wanachangia humu ndani na wanakosa umakini wa R na L kama mmemwelewa potezeeni issue ya lugha
 
Ladio yenu ukiwa ukitaka kusikiriza hapa Mtwala unaipata kwenye Flikwensi gani... Jee ukiwa Rindi,Ilinga,Mologolo na Dalesaraaam inasikika PLIDE FM...
 
Mi naona kama joke vile. Mlionivunja mbavu zangu ni wachangiaji. Mbavu zangu jamani!
 
Nimefutilia post za Tinted na kugundua kuwa hana tatizo la R na L bali tu alikuja kwa style ya kufurahisha jukwaa ili, maana limepoa sana na wadau wake wengi wanaonekana kuwa na msongo wa mawazo sana.......
 
Rakini bandugu si ujumbi umefika. Munisamehe tu si unajuha malugha magum.

Pride FM inapatikenika katika flikwenzi ya FM 87.8
Mkuu Tundapori wew ni burudani tosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…