fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 388
- 666
Ilikuwa mwaka 1996 baba yangu ndipo alipotuaga pale nyumbani Karegeya
Ilikuwa ni safari ya baba kuelekea Mwanza kisha aweze kuelekea jijini dar Es Salam kikazi
Ilikuwa ni utamaduni wa baba kurejea nyumbani kila baada ya miezi mitatu kuja kututembelea nakutuletea mahitaji Muhimu kama familia
Baba yangu kabla ya kifo chake alikuwa ni afisa ugavi katika shilika la nyumba Tanzania
Kitaluma alikuwa ni mwanasheria ila baada ya kutafuta ajira kwa kipindi kirefu bila mafanikio ndipo alipoamua kujishikiza katika fani hiyo ya procurement officer
Ni habari zilizoretwa na jirani yetu pale kijijini ndio zilizoondoa furaha ya milele moyoni kwangu
Nilimpenda sana baba yangu kutokana na jinsi alivyonijari na hasa kipindi ambacho alipokuwa akirejea nyumbani kutoka dar Es sàlaam
Kuna wakati alinibeba japo tayari kiumri sikustahili fadhira hiyo
Baba alikuwa ni baba wa huruma na upendo dhidi yangu
Ajari ya MV Bukoba sintoisahau maishani japo nilikuwa mdogo kiumri lakini mengi niliyo yashuhudia yatabaki maishani kuwa kumbukumbu isiyo futika
Baada ya taarifa ya kuzama kwa meri familia ya baba ilikusanyika pale nyumbani agenda kubwa ilikuwa ni kwenda Mwanza kuweza kujiridhisha endapo baba alikuwa hai au amekufa
Katika kikao kile kila mmoja alitafakari nani wakwenda kule Mwanza kutokana na kutokuwa na wenyeji ambao wangeweza kutoa hifadhi ya muda
Pamoja na mjadala mrefu uliochukua Massa takriban nane bado muafaka haukupatikana
Asubuhi na mapema mama alinivisha nguo zangu ambazo baba alikuwa ameniletea kutoka jijini dar Es salaam kisha akaniambia kuwa kesho yake tungekwenda Mwanza ilipotokea ajari
Wakati huo nakumbuka nilikuwa darasa la pili
Mama aliniambia pindi tutakaporejea ndio nitaweza kuendelea na masomo
Jioni ya siku hiyo tulikuwa katika meli ya MV Bukoba tukielekea Mwanza siku hiyo meli haikuwa na mizigo kama jinsi ilivyokuwa imezoeleka kwa sababu wafanyabiashara wengi walikuwa wamepoteza maisha katika ajari ya MV Bukoba
Ndani ya meli walijaa kina mama zaidi huku wakiambatana na vijana chipukizi sikuona wazee wa makamo kwa wingi japo simanzi ilitawala katika nyumba hii ya Baharini kila mmoja alitafakari kile ambacho taswira ya uono wake ilivyokuwa ikimuijia kuhusu ajari ile
Kuna wakati meli iliyumba na kusababisha mtikisiko basi kila mmoja aliogopa na kuomba mungu amsaidie, Mama alinikumbatia ungedhani ruba kwa jinsi alivyokuwa ananingangania nisitoke karibu na kifua chake kilicho jariwa matiti madogo mithiri ya parachichi za mbeya..
Nilianza kuhisi unyevunyevu juu ya mabega yangu hii ilikuwa ni saa nane za usiku nilipo inua kichwa changu huku macho yangu yakifunikwa na repe la usingizi nilimuangalia mama yangu usoni hakika hakuwa mama niliemzoea kumuona katika furaha
Alikuwa mama aliegubikwa na huzuni juu ya mmewe ambae ni baba yangu
Niliogopa kumuuliza sababu nilijua kama ningemsemesha mama katika hali ya namna ile ningeambulia kipigo au Angelia zaidi kila Mara nilipo jaribu kumtazama nilimkuta analia
Hakika kwa umri wangu sikujua huzuni ya mama ilikuwa juu ya nini nilitani kama baba angekuwa nasi wakati huo huwenda angelimbembeleza lakini haikuwa hivyo...
Nilijua safari yetu ingetukutanisha na baba niliamini ilikuwa ni safari Muhimu sana kwangu kwa kuwa nulipenda sana mambo ya mjini hasa kutokana na vitu alivyokuwa akiniletea baba pindi alipo kuwa anakuja likizo
Mapambazuko ya alhamisi tayari kingora kilipulizwa na nahodha kuashiria kuwa tayari tulikuwa katika fukwe za Mwanza
Taa za jiji la Mwanza ziliangaza matumaini ya sisi kufika salama katika jiji la mawe
Baada ya kushuka mama alikwenda mojaja kwa moja kwenye call box moja iliokuwapo pale customs akaingiza card kisha akawa anapiga simu nilimsikia akisema kuwa tumefika na tupo hapo custom
Sauti ya upande wa pili iliitikia nakusema angefika pale baada ya saa moja
Tukiwa pale huku tukiwa tumeungana na wasafiri wengine tuliokuja nao katika meli tangazo lilitolewa la kwenda kuhakiki miili ambayo ilikuwa imeopolewa kutoka ziwani tulijongea kuelekea pale ambapo zilihifadhiwa maiti
Sehemu ile ilikuwa na watu wa msalaba mwekundu na askari Jeshi wa Tanzania ila walikuwepo askari baadhi wakizungu hawa inasemekana walikuwa wametoka south Africa
Maiti walipangwa mithiri ya samaki juu ya meza huku wakifungwa katika mifuko ya prastic nyeupe ila nyuso zao zikiachwa wazi..
Kulikuwa na maiti wengi sana kuna maiti walionyesha tabasam na wengine nyuso zao zilikuwa zimenuna huku wengine wakiwa hawana macho kabisa inasemekana macho yao yalikuwa yameliwa na sangara
Msitari wa paredi ya wafu ulipangika vilivyo watu walipita kwa heshima ya hali ya juu wapo ambao hawakuweza kuangalia nakuishia kuangua vilio
Nikiwa nimeongozana na mama katika kukagua ile paredi ghafura mama alisimama na kumshika usoni maiti aliekuwa mbele yetu, alimfunua uso wake vizuri ili kujiridhisha kama kweli macho yake yalikuwa sahihi ndipo nilipo muona mama akidondoka na kuikumbatia ile maiti pale chini huku kilio kikubwa kikifatia
Sikuamini macho yangu kumbe alikuwa ni baba yangu mzazi ambae siku nne kabla nilikuwa nae akiniimbia nakuniambia kujituma katika masomo yangu
Hakika uso wa baba ulijaa furaha pamoja nakuwa alikuwa amekufa lakini uso wake ulikuwa na furaha ya dhati naweza kusema
FURAHA YA MAUTI.