Furaha ya kweli hutoka ndani yako

Furaha ya kweli hutoka ndani yako

Immortal_MH

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2013
Posts
1,240
Reaction score
2,252
Habari za muda huu wanabodi
Sijawahi kuandika uzi jukwaa hili, huu ndo wa kwanza. Kilichonifanya niandike huu uzi ni magumu niliyopitia wiki mbili zilizopita

Nilikuwa kwenye uhusiano na binti fulani lakini mara ghafla akanitumia meseji ya kuachana, nilipata na mawazo sana nikajaribu kuokoa jahazi kwa nguvu zangu zote lakini binti akawa mgumu wa kuelewa, nilikuwa naandika meseji za kuomba msamaha ndefu kama makala za Mwanahalisi lakini alikuwa hajibu au akijibu anajibu kwa matusi na maneno ya kashfa.
Juzi nikiwa napitia uzi mmoja nilikutana comment moja ya Maserati ilinipa nguvu sana na nikiri kuwa iliniinua upya. Nimeambatanisha hapo chini

Nimegundua kuwa furaha ya kweli inatoka ndani yako hakuna mtu wa kukupa furaha ya kweli zaidi yako mwenyewe. Wengi huwa tunajikuta tunapenda sana wengine badala ya kujipenda wenyewe kabla. Huwezi kuwa unaumia kisa homosapien mmoja amekuacha. Ukijipenda mwenyewe huwezi kuishi kwa manun'guniko

Baada ya jaribio la kuomba turudiane na yule binti niliamua kumuacha tu ila yeye naona ameanza kuhangaika na mimi. Aliniambia kuwa ananichukia sana ila namuona kila saa anahangaika na mimi kwenye status yake kwa vijembe kibao. Nina amini ukimuacha mtu huwez kuwa muda naye ila yeye anawashwa washwa na mimi. Ila nimemvungia tu anitumia text namjibu kwa kifupi tu baada ya hapo anacharuka ila namjibu kifupi tu bila kujishusha au kumtolea mapovu au kumuomba msamaha. Nina amini muda unaponya sana kama utauruhusu tu. Unatakiwa uamini katika 'power of letting go'.

Hakuna mtu anayetakiwa kuwa amebeba furaha yako, wewe ndo mmiliki wa furaha yako maana furaha ya kweli inatoka ndani yako.

Muwe na jioni njema
e1e31761981aeb2c0953eacbf6aafe03.jpg
 
Ukiachwa unahis uko peke yako, kumbe kila cku watu wanaachana, ila inauma hata ujipe furaha ya namna gani bado yupo utakaeona anahitajika ili furaha yako ikamilike, pole sana
Mkuu upo sahihi lakini sidhan kuwa kabla ya kuwa na aliyekuacha haukuwa na furaha
Kuna vitu vingi ukifikiria au ukifanya vinaweza vikakupa furaha ya kweli, ni maamuzi tu.
 
Mkuu upo sahihi lakini sidhan kuwa kabla ya kuwa na aliyekuacha haukuwa na furaha
Kuna vitu vingi ukifikiria au ukifanya vinaweza vikakupa furaha ya kweli, ni maamuzi tu.
Mapenzi kitu kingine wewe, hata wiki haitoisha utaleta mrejesho umempata wa kukuliwaza, ukiachwa donda linapona pale unapopata mwingine
 
Mapenzi kitu kingine wewe, hata wiki haitoisha utaleta mrejesho umempata wa kukuliwaza, ukiachwa donda linapona pale unapopata mwingine
Kama umenielewa vizuri sijasema kuwa sitakuwa na mtu mwingine
Nilichosema ni kuwa haitakiwi furaha yako awe anai-control mtu mwingine au mpenzi wako
Ukiwa unategemea kupata furaha toka nje utakuwa unavunjwa moyo kila muda
 
Vijana kila leo mnaamka mnalilia lia sijui n lini mtaacha taabia hiii .

Hongera janja umekuwa na umejielewa

Jifunzen kulingana na makosa
 
Kweli Comment yake ni nzuri sana, pole chief ndo maisha lakini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom