Furaha aipatikan kwa utajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Furaha aipatikan kwa utajiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 3, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,005
  Likes Received: 6,823
  Trophy Points: 280
  NI siku nyingine tena mpenzi msomaji nakukaribisha katika makala hii inayokujia kila Aalhamisi, lengo likiwa ni kujifunza mambo mbalimbali katika maisha tunayoyapitia.
  Mara kwa mara waweza kufikiri kuwa kama ungekuwa na gari la aina fulani, nafsi yako ingeweza kufarijika.
  Kama ungeweza kumpata mtu mtakayeweza kuishi maisha ya ndoa katika raha na shida, ungekuwa na furaha, kama usingekuwa na hali ya msongo kutokana na ukosefu wa fedha, ungekuwa umejitosheleza.
  Ni kweli unaweza kuwaza mengi zaidi ya hayo kwamba kama ungeweza kufanya jambo fulani ama kuwa na magari, nyumba, dhahabu na vitu vingine vya thamani, ungekuwa na furaha, lakini hicho si kipimo halisi cha kuhitimisha furaha yako.
  Sasa ni wapi ambako unaweza kuipata furaha, kama si kwenye utajiri, mazoezi na kukubalika ama kwenye mahusiano?
  Tunaona kuwa, ipo siri kwamba tabia yako ni muhimu kuliko hali halisi. Kinachotakiwa kufanya ni kuondoa mawazo hasi na kuwa na mawazo chanya.
  Kuna mfano wa mtu mmoja aliyeona kuwa kama angekuwa na gari zuri la kifahari, furaha yake ingetimia. Kutokana na kupenda kuwa na gari, mara kwa mara alikuwa akiota kuwa na gari hilo.
  Mtu huyo kila alipokuwa akijiwazia kama yupo kwenye usukani wa gari, alihisi ananusa harufu nzuri ndani ya gari. Na kwamba alihisi kama yupo barabarani analiendesha gari hilo.
  Muda mfupi baadaye, alipandishwa cheo ofisini kwake na kujiona kuwa yale aliyoyatamani ameyapata. Na kwamba ataweza kujitosheleza kwa kile alichokihitaji.
  Baada ya kupata gari lile alilokuwa akilihitaji, alijikuta tena akitamani kila mwanamke aliyemuona, hali iliyofanya matumizi yake kuongezeka kuliko kipato kile alichokuwa akikipata.
  Na wanawake aliowapenda hawakuwa na upendo wa dhati kwake, ila ni kwa kuwa walimuona anaendesha gari zuri la kifahari, na kutarajia kupelekwa katika hoteli nzuri za kifahari, pamoja na kupewa zawadi nzuri za gharama.
  Baada ya muda mchache alibaini kuwa gari hilo badala ya kumpatia furaha, alipata maumivu, kwa sababu pesa yake ilitumika katika mambo ya kifahari zaidi.
  Taratibu alianza kufikiria gari lake na marafiki wapya aliowapata baada ya kuwa na gari, pamoja na kujiuliza kama kweli wanawake wale walikuwa wakimpenda kwa dhati ama walilipenda gari lake.
  Furaha yake kuhusiana na gari lile ikaanza kutoweka, alianza kupata sononeko katika nafsi yake na kuona gari lile ni mzigo.
  Hali hiyo ikamkatisha tamaa kwa yale aliyoyategemea, kwamba gari ndiyo utimilifu wa furaha katika maisha yake.
  Ni vema kukumbuka kuwa vitu vinavyoonekana kwa macho haviwezi kuleta furaha ya kweli.
  Kwa sababu watu wanaotafuta furaha kwa kutumia fedha, ukuu walionao, utajiri ama mali walizowekeza ni sawa na kuitafuta furaha hiyo kwa muda tu na si ya kudumu.
  Kwa kuwa siku zote fedha haziwezi kununua furaha, kuna mifano ya watu wengi ambao ni matajiri, lakini wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi.
  Hawana furaha kama uliyonayo wewe au mimi. Ni ukweli kwamba fedha waliyonayo inawapa matatizo mengi na furaha kidogo.
  Watu wengi mashuhuri wamekuwa wakiishi maisha ya kukata tamaa, matokeo yake, wengi wao huamua kujiua.
  Hivyo basi, furaha haipatikani kwenye utajiri, marafiki, kutumia dawa za kulevya ila ni katika kuituliza akili yako.
  Tukiangalia katika maandiko matakatifu ndani ya Biblia, ambayo Wakristo wanaamini, yanasema heri wale walio maskini wa roho kwa maana ufalme wa Mungu ni wao, heri wale wenye huzuni kwa kuwa watarehemiwa.
  Heri wale wenye upole kwa kuwa watairithi nchi. Heri wale wenye njaa na kiu ya haki kwa kuwa watashibishwa.
  Na heri wale wenye mioyo safi kwa kuwa watamuona Mungu. Heri wale wapatanishi kwa kuwa wataitwa wana wa Mungu.
  Hivyo basi, neno heri lina maana ya furaha, hivyo bila kujali kama umeshinda ama umeshindwa, umefanikiwa ama hujafanikiwa, una furaha ama unataabika. Kwa hiyo mtu yeyote anayesoma maneno hayo na kuyarudiarudia moyoni mwake, anajikuta ni mwenye furaha wakati wote.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Utajili ndo mambo yote hata huyo mwANDISHI AMEANDIKA ILI APATE HELA SO ACHA UTANI WEWE WE HUSTLE EVERYDAY...
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...