Usikubali Kuondolewa Furaha Yako Na MUNGU

Usikubali Kuondolewa Furaha Yako Na MUNGU

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,232
Reaction score
1,741
Yer 25:10 SUV
[10] Tena, nitawaondolea sauti ya kicheko, na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi, na sauti ya bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na nuru ya mishumaa.

Ujumbe huu ulikuja kupitia kinywa cha nabii Yeremia, ulikuwa ni ujumbe wa hukumu ya Mungu juu ya Yuda na mataifa mengine jirani.

Mungu aliwatangazia adhabu itakayokuja juu yao siku chache zijazo kutokana na uasi wao uliokuwa wa kuabudu sanamu, na kupuuza manabii wake.

Hukumu hii ilikuwa ya namna yake, matokeo yaliyotarajiwa kwenye hukumu hii ilikuwa ni kuondolewa kabisa furaha yao, kuishi maisha ya kawaida, ule mwanga wa matumaini ungezima kabisa kwao.

Tunajua kuwa katika agano jipya moja ya tunda la Roho Mtakatifu ni Furaha, kwahiyo kuondolewa kwa furaha hii ilikuwa ni ishara mbaya ya kutengwa na uwepo wa Mungu, jambo ambalo litakuwa ni hatari sana kwa mwamini.

Gal 5:22 SUV
[22] Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

Mtu anapojitenga na Kristo, anapoamua kuasi na kujitenga mbali na Mungu, mtu huyu amechagua kuondolewa furaha yake, furaha ya kweli katika maisha yetu inatokana na Mungu, maana dunia haiwezi kutoa furaha ya kweli.

Mtu aliyechagua kumwamini Kristo, na kuishi ndani yake, amechagua furaha, hata kama dunia inamsoga na mambo mengi, bado anaweza akawa na furaha ambayo dunia imeshindwa kumpa.

Usifarakane na Mungu kwa matendo mabaya, maisha yasiyompendeza Mungu wako, maana kufanya hivyo utakuwa umeamua mwenyewe kujitenga mbali na furaha ya kweli.

Kaa ndani ya chanzo halisi cha furaha yako, ambacho ni Mungu, utaona ile furaha ya kweli ikidumu ndani yako, furaha hii haitegemei hali nzuri ya maisha yako, hata katikati ya masumbuko mengi utakuwa nayo.

Ukikosa furaha katika dunia hii, utakuwa umekosa ladha ya kuishi katika dunia hii, utakosa nguvu za kuendelea kupambana kwaajili ya maisha yako na familia yako, au wale unaowaongoza.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom