Funzo: Ukiua vyama vya upinzani ,basi utapata upinzani kutoka ndani ya chama chako,na huo ndio upinzani mbaya

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,661
Sasa ni wazi,

Baada ya harakati za muda mrefu za kubomoa upinzani, kununua wabunge,kuzuia mikutano ya hadhara na kadhalika, ilidhaniwa kwamba upinzani umekwisha.

Lahaula, sasa upinzani umezaliwa ndani ya Ccm yenyewe,humohumo ndani, mapambano yanaendelea na tunaona tu chupa,rungu,mawe yanavurumishwa ndani ya Nyumba.

Ni wazi kwamba binadamu hata umpe nini, ukimnyima Uhuru, hata vitu vya thamani ulivyompa hataviona thamani yake.

Turudi mezani tupange mikakati upya,mbinu ya sasa imekwama na imeleta nyufa kubwa ndani ya Nyumba.

Na ni wazi kwamba wazee walioongoza nchi hii kwa muda mrefu hawaridhiki,nadhani Makamba na Kinana wametangulizwa kwanza kabla wazee wenyewe hawajasema
 
Bado kuna uchaguzi mkuu wa mwakani, mategemeo ni kutokea mtifuano na usaliti wa kutosha kati ya ccm asili dhidi ya wahamiaji haramu! 2025, ndiyo kabisaa ccm itakufa rasmi kwa sababu ya makambi yatayoibuka iwapo tu huyu mzee hatajigeuza kuwa Mu7.
 
Sasa ni wazi,

Baada ya harakati za muda mrefu za kubomoa upinzani, kununua wabunge,kuzuia mikutano ya hadhara na kadhalika, ilidhaniwa kwamba upinzani umekwisha.

Lahaula, sasa upinzani umezaliwa ndani ya Ccm yenyewe,humohumo ndani, mapambano yanaendelea na tunaona tu chupa,rungu,mawe yanavurumishwa ndani ya Nyumba.

Ni wazi kwamba binadamu hata umpe nini, ukimnyima Uhuru, hata vitu vya thamani ulivyompa hataviona thamani yake.

Turudi mezani tupange mikakati upya,mbinu ya sasa imekwama na imeleta nyufa kubwa ndani ya Nyumba.

Na ni wazi kwamba wazee walioongoza nchi hii kwa muda mrefu hawaridhiki,nadhani Makamba na Kinana wametangulizwa kwanza kabla wazee wenyewe hawajasema
Jpm endelea kukaba hao wapinzani feki mpaka wapotee.
Hata usemeje, kama hamjipangi mtaedelea kupotezwa.
 
Binadamu ni mpinzani by nature. Hata Adam, Musa na manabii mara kwa mara walipingana na Mungu.
 
Ni rahisi kuifanya Chato izidi maendeleo Dubai kuliko kuuwa upinzani. Upinzani ni nature ya mwanadamu.
 
Back
Top Bottom