Wanasema hakuna aijuaye kesho na wanaume tunapigana kutafuta mali sio kwa ajili yetu bali watoto wetu wakati mwingine unatafuta kwa nguvu zote ukijua kesho hutakuwa juu ya uso wa dunia hii hivyo mali hiyo itumike kuwaendeleza watoto wako.
Kuna kisa kimoja kimetokea kwa mke wa rafiki yangu nacho ni hiki;
Mwaka juzi rafiki yangu alipata ajali akafariki lakini alikuwa ameacha mali nyingi tu ikiwemo nyumba mbili viwanja vitatu na magari mawili ya kutembelea na fuso mali zote alimrithisha mke wake walikuwa wamezaa watoto wawili, baada ya muda yule mama alipata mwanaume mwingine wakatumbua zile mali kimya kimya uza viwanja uza nyumba uza magari ndugu wa mme kushtuka anauza nyumba ya mwisho akahamia kwa huyo mwanaume wake baada ya muda wakashindana akarudi kupanga ninavyoandika hapa dada yupo mtaani kupanga kachoka vijana wanafanya yao watoto wanaishi katika hali ngumu sana wametoka shule nzuri wapo elimu bure lakini baba yao aliacha mali nzuri na kama ingelipata mtu makini ingeliwaendeleza mpaka wajitegemee, kwa tukio hili nimejifunza kitu mwanamke sio wa kuamini kabisa lakini pia sisi wanaume tuna la kujifunza hapa, je mali zako ni sahihi kumkabidhi mkeo?
Je, ipi nzuri itumike ili kama ikitokea haupo duniani mali hizo zitumike kuwasaidia watoto wako maana hakuna aijuaye kesho..