jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,951
- 29,532
Leo siwalaumu wanasiasa wa pande zote na pia siwalaumu wananchi ...siwalaumu kwa kuwa ni vyema kukosea na kujifunza...mimi najitoa kwenye makundi hayo mawili kwani nimeshawahi kuchangia mara kadhaa juu ya ubaya wa neno hili la bure tena bure kwa hisani ya watu flani!!
Nimeingia JF nikipingana wazi wazi juu ya hizi bure...nimeingia JF na kibwagizo cha 'KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA'' Hakuna aliyewahi kukielewa au labda wapo waliokielewa na kubakia kucheka na kupuuza...lakini ni kibwagizo cha kuamsha ari na fahari ya Utanzania wetu.
Wnasiasa wa pande zote yaani wa Chama tawala na vyama vya upinzani walisukumwa na wananchi kulitamka hili neno baya la BURE...BURE KWA HISANI YA WAHISANI...!
TUMESIKIA KUHUSU ELIMU,AFYA NA MENGINEYO MENGI YAKITAJWA KUWA YATATOLEWA BURE...NA SISI TUKASHABIKIA SANA NA KUSHINDANISHA HIZI BURE.
Sasa kulingana na haya yanayojiri tunaweza kujifunza somo kubwa sana na kama tusipojifunza basi bila shaka tutakuwa na kilema cha maisha.
Kilichotokea ni ishara tu ya yanayoweza kutokea iwapo tutaendelea kuendekeza bure...
Tunatajiwa kuwa matibabu ya wazee,watoto,wajawazito,vilema,na makundi kadhaa ni bure ingawa kimsingi sio bure bali yanalipiwa na wahisanj ambapo mara kadhaa wamechelewesha au kutishia kutochangia hii bure ya hisani...
Iko siku Serikali itawekwa mkononi na wahisani kwa kutishiwa kukatishwa kwa misaada ya dawa...hapo ndipo kulia na kusaga meno kutakapotokea iwapo hatujajiandaa kibajeti.
Nimebahatika kupata uzoefu wa hii misaada na kujaribu kuipa thamani na kulinganisha uwezo wa wananchi katika kuchangia kiasi chenye thamani hiyo hiyo...
Nimejiuliza kuwa ni kwanini mwanaume rijali na msumbufu anapokuwa bar aweze kuoa kwa harusi ya milioni 15 na ng'ombe hadi 20 au zaidi lakini inapokuja suala la kulipia huduma ya kujifungua ashindwe kulipa japo sh 10000 tu?
Nimejiuliza pia kwa nini mwanaume mwenye uwezo wa kumnunulia vitenge na kanga mke wake na kumchinjia mbuzi anashindwa kuchangia malipo ya matibabu ya mtoto wake?
Inakuaje watu wawe tayari kuchangia harusi zaidi ya tatu kwa kiwango cha laki moja au zaidi lakini wanashindwa kulipia kiwango hiko hiko kama bima ya afya kwa familia kwa mwaka?
Hivi inakuaje haya yatokee kama sio kuendekeza na kuendeleza hulka ya kijinga?
Ni lazima sasa tujifunze kulipia huduma hata kama kwa kiwango kidogo...!
Ufahari wa kutia mimba uendane na fahari ya kulipia matibabi na sio kusubiri majasho ya wahisani..!