Funzo kwa macashier wa benki, wenye vikundi vya vicoba muwe makini sana

uduzungwa

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
552
541
Wana Jamvi salama.
Naomba kwanza nianze na kumshukuru Mungu kwa kuweza kunifanya kuwa hai mpaka sasa.

Baada ya hapo niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Hapa nchini kumekuwa na utaratibu wa watu kujiunga kikundi afu na kuanza kujikusanyia hela kidogokidogo kwa malengo mbalimbali, ikiwemo kusaidiana hasa wakati wa matatizo.

Hivi vikundi hasahasa vikijulikana kama vikoba, au small saccos.
Wao huchangishana hela then nakuweka benki. Ukikuta kikundi ambacho ni cha siku nyingi kidogo unaweza kukuta wamefikisha karibia hata 200m na zaidi.

Sasa ishu iko hivi wana. Huko benki ambako tunaweka hizi hela zetu kuna mameneja na mabosi wakubwa ambao sio waaminifu kabisa. Wao hutumia uongozi wao vibaya kwa kuchota hela hizo ambazo mmeweka kwaajili ya matumizi yenu wao hufanyia biashara zao kabisa.

Kuna tukio kama la namna hii limetokea kwenye benki moja (jina kapuni ) tawi fulani hivi hapa jijini Arusha, meneja akishirikiana na meneja msaidizi. Wameweza kuchota hela karibia 400m kwenye vikundi mbalimbali.

Sasa lililowakuta hawa mabosi ni kwamba walikosea wakachota hela kwenye kikundi ambocho wao wana simbanking. Mana kila hela ikiingia wanapata taarifa. Walifanikiwa kumlaghali cashier wao kwa kumpelekea payslip ambayo wao washaiba hela ndani kiasi cha kama 75m ili aclear ile process ya withdraw ikiwa hela washachukua huku wakimwambia hela amechukua mtu wa kikundi. Baada ya kufanikiwa kutoa hiyo hela ile sms ikawafikia wahusika (wenye kikundi) kuwa wametoa 75m. Kumbe hakuna aliyeenda kutoa hela.

Wenye kikundi wakabidi watimbe bank kuulizia kulikoni. Mbona tunapata sms ya kutoa hela wakati hatujatoa hata senti. Yule meneja kwa sababu anajua mchezo akasema kuwa kuna mmoja wa kikundi wenu amekuja kutoa hela hapa.
Wao wakakataa kuwa hahusiki na utoaji wa hela.

Ikabidi kwanza wale waliohusika na ile transaction wawekwe ndani kwanza wote. Ikiwa ni yule cashier na msaidizi wa meneja mana msaidizi wa meneja yeye ndio alipeleka ile payslip kwa cashier akimwambia kuwa huyu mtu ameshachukua hela iclear hii payslip.

Ikabidi uongozi uanze kufanya uchunguzi nini kimetokea.
katika kupeleleza ikabainika kuwa meneja wa tawi aliingia kwenye main money draw akachukua hicho kiasi cha 75m na kufoji ile sign ya signatory wa kikundi then akampa menejamsaidizi akamlaghai chashier wake atoe hela mana hata angalia sahihi vizuri.

Baada ya uongozi wa benki kutambua huo huuni wakaanza kucheki transcation zote. Ikabainika kuwa meneja akisaidiana na menejamsaidizi wameweza kutoa zaidi ya 400m kwa stly hiyohiyo kwenye account tofautitofauti.
Mpaka sasa meneja na meneja msaidizi wapo wanakesi ya kujibu.

Na meneja amebainika anamiliki shule, magari ya biashara, na maduka ya bidhaa za jumla na rejareja.

Sasa funzo kwa macashier wote benki. Usimuamini hata kidogo meneja wako wa tawi, usitoe hela bila kuona mteja dirishani. kwa wenye vikundi nashauri mkifungua accounti hakikisheni pia mnajisajili simbanking msignatory wote. Ili kama kuna hela inaingia na kutoka muweze kupata sms.

Niwahusie wale mameneja wa benki msiwe na tamaa za hela za watu jamani. Tunawalipa gharama za kutunzia hela zetu mbona mwatufanyia hivi.
 
Back
Top Bottom