Benki ya TCB Tumbi Kibaha ni ya ovyo

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,618
Leo ni mara ya nne nimesafiri mpaka benki ya TCB iliyoko kwenye majengo ya Shirika la Elimu Kibaha kupata huduma za kibenki.

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwaambia uongozi wa hii benki, watupie jicho lao kurekebisha dosari nyingi za hii benki kabla mambo hayajaharibika.

Machache niliyozoea kuyakuta.

1. Very Poor Customer Care. Yani ni jambo la kawaida sana kwa wafanyakazi wa hii benki kupita bila kuzungumza na wewe au kuwasemesha wakiwa kwenye viti vyao na wao kukunyamazia kimya wakiwa Bize na simu zao. Yani hawajali kabisa.

2. Kwenye Counter yao iliyopo sambamba na dirisha la Posta, ni kawaida sana mteja kuwa kwenye foleni na Cashier kuwa Bize kuongea na simu. Yani hajali muda wa kabisa wa mteja wala hashtuki mteja kutumia muda mrefu kwenye queue.
Mbaya zaidi Wafanyakazi wa benki wenyewe hufika kwenye Counter wakati Cashier yupo na mteja na kuanza mazungumzo na mbaya zaidi ni mazungumzo binafsi yanayochukua mpaka dakika tano

3. Kubwa kuliko yote ni pale umeme unapokatika. Computer ya Cashier haina UPS. Umeme ukikatika na Kompyuta ya Cashier inazimika. Aibu iliyoje hawana Standby Generator. Ni mpaka mtu anaitwa Manumba sijui ndio akaiwashe. Akiwa hayupo mtakaa hapo kusubiri mpaka aje aiwashe. Kwa siku ya leo tumesubiri kwa zaidi ya masaa mawili ili jenereta liwashwe. Ni aibu kwa kweli.

Ni aibu mno kwa benki kubwa kama hii kuwa na huduma mbovu kama hizi.

Na wafanyakazi hawaonyeshi kujali. Huenda viongozi wa hii benki hawana taarifa ya kinachoendelea hapa kwenye tawi lao la pekee hapa Kibaha. Imagine mteja ana haraka zake tawi lipo tumbi mteja anatoka kwa Mathiasi, au Maili moja anakuja kukutana na vituko kama hivi.

Benki ya Posta Kibaha MJIREKEBISHE.
 
Shida inakuja hapo MENEJA kama ni MWANAUME basi kuna mchezo anafanya na hao WAFANYAKAZI wake ndio maana kuna dharau kama hizo.

Siku zote sehemu ambayo kuna mtandao wa Kimapenzi lazima kuwepo na UZEMBE.
 
Hiyo benki ibaki tu kuhudumia wazee waliostaafu wanaokwenda kutoa monthly pension kila mwisho wa mwezi.
 
Shida inakuja hapo MENEJA kama ni MWANAUME basi kuna mchezo anafanya na hao WAFANYAKAZI wake ndio maana kuna dharau kama hizo.

Siku zote sehemu ambayo kuna mtandao wa Kimapenzi lazima kuwepo na UZEMBE.
Hii ni kweli kabisa.

Nimewahi kua msimamizi wa mradi wa ndugu yangu, pale wafanyakazi wengi walikua wa kike, nikafanya technical mistake nikawatafuna 2 tena wale waliokua wachapa kazi wazuri, mambo yalianza kuharibika mwisho ilibidi nitimuliwe mimi😂.

Kula wafanyakazi hasa wewe ukiwa ni kiongozi hapo ni kosa kubwa sana.
 
Posta Masta Mkuu Maharage umesikia haya, nenda sasa ukarekebishe. Benki hii si ni ya Posta!! Kaoneshe utofauti sasa, tumia ujuzi wako unaokupa ufanisi kwenye biashara yako na TTCL. Fufua shirika la Posta
 
Yes TCB wakati mwingine wako na issues but naona kama bwana Mzito ana personal agenda. Mimi naishi Kibaha na TCB nina account yangu hapo. Sijawahi kukutana na hilo tatizo ambalo analiongelea. Hata jana nilikua hapo.
Wewe utakuwa mmojawapo wa wafanyakazi wa hapo au ndio 'damager' mwenyewe.
 
Yes TCB wakati mwingine wako na issues but naona kama bwana Mzito ana personal agenda. Mimi naishi Kibaha na TCB nina account yangu hapo. Sijawahi kukutana na hilo tatizo ambalo analiongelea. Hata jana nilikua hapo.
Hebu tuelezee kuhusu huo wakati mwingine, huenda ndio aliokutana nao Mzito Kabwela
 
Hii ni kweli kabisa.

Nimewahi kua msimamizi wa mradi wa ndugu yangu, pale wafanyakazi wengi walikua wa kike, nikafanya technical mistake nikawatafuna 2 tena wale waliokua wachapa kazi wazuri, mambo yalianza kuharibika mwisho ilibidi nitimuliwe mimi😂.

Kula wafanyakazi hasa wewe ukiwa ni kiongozi hapo ni kosa kubwa sana.
Ulifanya Assassination 🤣
 
Mimi nilipita Kibaha jioni na umeme ulikuwepo kama ni issue ya mgao ulianza baada ya saa za kazi. Nimekuwa mteja wa muda mrefu wa benki hii tangu ilipokuwa Tanzania Postal Benki, hadi walipoungana na Twiga na Benki ya wanawake TWB na imefanya mabadiliko makubwa sana katika utendaji na Huduma kwa wateja na hata ukuaji wa faida mwaka hadi mwaka ungetembelea matawi yao mengine kama mlimani City. Arusha Dodoma na kadhalika ili uone mabadiliko makubwa yaliyotokea kwenye uendeshaji wa Benki kuanzia muonekano hadi Huduma kwa wateja
 
Mkuu, jamaa anaongelea tawi la Kibaha na sio benki hiyo kwa ujumla wake. Ndio maana amemaliza andiko lake kwa kuwaomba viongozi waliangalie tawi la Kibaha. Wewe unapomshauri atembelee matawi ya Mlimani City au Dodoma na Arusha, hayajibu hoja zake kuhusu uendeshaji wa Kibaha branch.
 
Back
Top Bottom