Royal Warrior
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 1,166
- 2,117
Assalaam Alaykum.
nafahamu wengi wetu ni wavivu wa kusoma vitabu, ila mie nimejikaza na kukisoma hiki kitabu cha Robert Kiyosaki cha Rich dad Poor dad. kwa kweli nimejifunza kitu kikubwa sana, na ningependa na nyie ma hustlers wenzangu tuweze kujikwamua kiuchumi na kifedha.
tuweke utamaduni wa kununua Assets na sio kufikiria kuongeza kipato (income, hasa mshahara).
najua wengi hapa mtakua hamuelewi inakuwaje tusiwe tunahangaika kuongeza kipato (income) ?
kuongeza kipato hakutakutajirisha, muda ambao kipato chako kitaongezeka basi na pia expenses (gharama) zako zitaongezeka hivyo utajikuta unalipa kodi (tax) zaidi, unatumia zaidi kulipa gharama za maisha kama rent,vyakula,mavazi, ada, nk. mwisho wa siku unakua upo pale pale kwenye vicious circle.
badala yake jitahidi kuongeza Assets zako,, nikisema assets namaanisha ni kitu/biashara inayokuingizia pesa bila ya ww binafsi kuwepo mahali ilipo hiyo asset physically. yaani kama ukiwa na Asset Dar, unaweza kwenda Mwanza kupumzika ila huku dar bado asset inakufanyia kazi ww (inakutengezea kipato).
hii ndio namna ya kuifanya pesa kuwa mtumwa wako. pesa inakufanyia kazi wewe na sio wewe kuifanyia kazi pesa.(ifanye pesa kuwa mtumwa wako, na sio wewe kuwa mtumwa wa pesa) na uzuri wa pesa inakufanyia kazi usiku na mchana. na hizo pesa zinazo zalishwa na hiyo asset. zitumie kuwekeza kwenye asset nyingine. yaani wewe kazana kwenye kuongeza assets zako kadri uwezavyo... and time will tell... (its just a matter of time).
Pia tujue kutofautisha kati ya Asset na liability.
najua hapa baadhi ya wahasibu hawatakubaliana 100% na jinsi Robert Kiyosaki alivyozi elezea. ila kwa ufupi.
Asset ni kitu kinachokuingizia pesa mfukoni (kinatengeneza pesa). kwa mfano hisa, biashara ambayo haihitaji uwepo wako, nk.
Liability ni kitu kitu kinachotoa pesa mfukoni mwako. mortgage (mkopo wa nyumba),
Gari (service, mafuta, insurance, na gharama nyingine zinazoambatana na gari) nk.
hii haimaanishi kwamba usiwe na gari, hapana. gari unatakiwa kuwa nayo, ila tu pale ambapo utakuwa umewekeza asset za kutosha kuweza kuihudumia hiyo gari. sijui kama mmepata picha kidogo.
Hivyo unapopata pesa fikria kwanza kuwekeza kwenye asset na sio kununua liabilities.
Ahsanteni, (wenye maswali mnakaribishwa).