FUNYUKI (Fuga Nyuki Kibiashara)

FUNYUKI (Fuga Nyuki Kibiashara)

asante kwa kujibu. langstroth ni bei gani na inakuwa na frem ngapi boss wangu? Na pia kwanda site kuna gharama yeyote?
Langstroth ina 10 frame ni 150,000/=. Ndiyo kwenda site unachangia shilingi elfu 10 ya nauli kwenda na kurudi lakini kama unausafiri wako hautochangia chochote.
 
SAFI SANA, SASA TUNAENDAJE? LINI, NA MUDA GANI?
Kwenda ni kesho tunakutana asubuhi saa mbili nanusu uwe umefika mwenge mataa. Lakini piga 0762936519 ili kujiandikisha majina yako namba za simu na mahali unapotokea.
 
Kwenda ni kesho tunakutana asubuhi saa mbili nanusu uwe umefika mwenge mataa. Lakini piga 0762936519 ili kujiandikisha majina yako namba za simu na mahali unapotokea.
poa kesho asubuhi nikifanikiwa kuamka salama nitakupigia.
 
Mashamba yapo DSM Bagamoyo Kiwangwa.

Heka moja unaweka mizinga 60 hadi 70

Shamba likiwa chini ya usimamizi wetu utachangia gharama kulingana na idadi ya mizinga mfano mizinga 10 hadi 30 utachangia 30,000/= kila mwezi.

Na ukikamilisha malipo yako unapatiwa hati miliki.

Sisi ni TANZANIA INTERNATIONAL BEE COMPANY na Mr kuku hausiki kwa vyovyote vile kwenye mradi wetu. Lakini pia unaweza kututembelea siku yoyote ya kazi ofisini kwetu.




ukichukua hekari 1 ya shamba ina thamani ya 1.2m na ukisema unaanza na mizinga 10 ya kisasa mzinga 1 unauzwa 150,000 hivyo mizinga 10=1.5m,,,jumla ya gharama zote ni (1.2m+1.5m) =2.7M, hivyo badala ya kutoa 2,700,000 kwa pamoja utalipia 810,000=30% ya gharama zote ,, na salio linalo baki ambalo ni 1,890,000 utagawa kwa miezi 20 =94,500 TU ndiyo utakayokuwa ukitakiwa kulipia kidogo kidogo ndani ya miezi 20 wakati huo ukivuna mazao yako kama vile ASALI,CHAVUA, GUNDI,NTA n.k
nimeelewa kiasi? je hiyo gharama ya mwezi nitaanza kuilipa nitakapoanza kuvuna? maana najua mizinga itachukua muda kujaa. au napaswa nianze kuwalipa hiyo pamoja na gharama za usimAmizi kabla sijavuna?

Na je kwa idadi ya mizinga hiyo kumi lengo litafikiwa?
 
nimeelewa kiasi? je hiyo gharama ya mwezi nitaanza kuilipa nitakapoanza kuvuna? maana najua mizinga itachukua muda kujaa. au napaswa nianze kuwalipa hiyo pamoja na gharama za usimAmizi kabla sijavuna?

Na je kwa idadi ya mizinga hiyo kumi lengo litafikiwa?
Gharama ya mwezi unatakiwa Kuanza kulipa kila mwezi hiyo ni constant,,,(labda uamue kulipia Deni lako lote kwa pamoja Ni ruksa pia).
Mizinga 10 kwa kawaida kwa sababu kwenye mashamba haya Kuna wataalamu kazi yao Ni kuhakikisha nyuki wanaingia kwa muda mfupi kwa kutumia njia za asili ama njia ya colony division hivyo haitachukua muda mrefu zaidi ya mwezi mizinga yako kumi inaweza kuwa na nyuki,,,hivyo mwezi wa pili Kam unavuna mazao ya muda mfupi Kama chavua,unaweza kuanza kuvuna ukisubiria asali.
 
Naomba kufahamu mahali panapofaa kuweka njia/sehemu ya nyuki kuingia kwenye mzinga.
Kuna wanaotoboa matundu matatu pembeni kwa mzinga.
Wengine wanakata mstatili mdogo wenye kimo cha kama sm.1 na urefu kama sm.10 hadi 15.
Ipi inayofaa?
 
Back
Top Bottom