Mbunge wangu ana sifa hizi:
i.Ni mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura wakati wa uchaguzi
ii.Mbunge aliyejenga nyumba yake kwenye kiwanja chetu cha kujenga soko
iii.Mbunge aliyetangazwa na Fuime kwa maagizo ya JK
iv.Mbunge aliyetangazwa baada ya kuzimwa umeme
v:Mbunge ambaye jimbo lake lina shida ya maji kuliko yote hapa mjini Dar na anatamba hajali maana
hatukumchagua kwani alishinda kwa pesa yake'
anasema Tanganyika iliungana na Zimbabwe
Mi Mbunge wangu naona hata aibu kumtaja ila inabidi kwa mujibu wa thread hii. Anaitwa Ndugu....ayiiiiiii!!! Hana udugu huyu. Kila siku anaongea pumba na kugombana na Kisu ( Lissu). Nikisikia kaongea kitu huwa najificha kwanza ili wenzangu wasinicheke!!! 2015 mbali sana.
Wa kwangu ni mbinafsi, visasi na chuki sana kwa wanaomhoji utendaji wake, alijenga ofisi kubwa ya spika jimboni kwake kama vile atakuwa spika wa maisha. Kwa ufupi HAFAI.
Mzee WAPIGWE ndio jembe langu.
Khaa!! kama aliwaahidi wakati wa kampeni yake ina maana alikuwa anawatapeli?mkuu kazi ya mbunge ni kusambaza maji? Hebu fafanua hapa...
Hahaaa mkuu kumbe tuko jimbo moja.Nimeipenda hiyo yaani badala yakusambaza maji yeye kutwa kucha anasambaza namba za viongozi ili watukanwe utadhani hao ndio waliotuomba dhamana 2010.
Wa kwangu ni mbinafsi, visasi na chuki sana kwa wanaomhoji utendaji wake, alijenga ofisi kubwa ya spika jimboni kwake kama vile atakuwa spika wa maisha. Kwa ufupi HAFAI.
bi kidude nini?
Kweli wangu ni JEMBEEEEEEEEEEEEE
jimbo langu CDM na NCCR wamedhihirisha ubinafsi na kwamba wapo tayari kutawaliwa milele,wamechakachuana hatimaye wameiachia CCM nafas zote za.M/kiti na Makamu wake
Daah.,mi ndo humu nimegundua yaweza ikawa jimbo zima mimi tu ndo naijua JF...Mi wangu ni yule mwenye kiburi,mzee wa kubetua mdomo kama anasutana..wanamuita Mzee wa kanuni,kifungu cha 65(b) fasili ndogo ya 4 ukurasa wa 64 wa kitabu cha Kanuni za kudumu za Bunge...huyu jamaa anatudharau sana...akienda jimboni hataki maswali,ukimuliza swali anakuitia polisi wakunuse mdomo,anasema huwezi kuwa jasiri ivo kumuliza maswali kama hujaswata ulanzi na kuvuta ganja!...anakutia ndani kwa sheria ya Vinywaji Baridi na Vileo...eti sheria hiyo haimtaki mwananchi kunywa pombe isiyo na muhuli wa TBS....Ajabu wakati wa kura za maoni anawahonga watu na vijombero vya ulanzi,mana huwa hatupigi kura za Mbunge,akipita tu kura za maoni hana mpinzani anapita bila kupingwa!!Kama unataka kile kimnyama kinyegere kije kuvunja mlango kikwarue chukua form umpinge kwa upinzani