Fungua ITV hotuba ya Mh. Rais inarudiwa

Fungua ITV hotuba ya Mh. Rais inarudiwa

Nimekupenda bure.

Mwingine angela za na kukosoa kwa pont hizo hizo ulizosema. Wewe umetoa Kama maoni ktk lugha sahihi kabisa. Hongera kwa uzalendo.

Wenye kazi yao ni wasikivu, wamekusikia na wamepokea kwa MIKONO miwili na tunaamini watazingatia.

Queen Esther

Leo Magufuli katoa hotuba nzuri sana kupita nyingine zote zilizowahi kutolewa na raisi wa Tanzania kwa miaka 30 iliyopita. Ni kweli magufuli na serikali yake ya watu wawili wanahitaji maombi na msaada wetu katika kufanikisha hii sera ya hapa kazii tu. Ila inabidi tuwe makini haya matukio tunayoshangilia kila siku yasitufanye tupoteze dira ya nchi.

Kwa sasa gumzo la mitaani ni yaliyojiri bandari, stanbik, hoteli morogoro, kuchelewa kazini na kadhalika. Tusichozungumzia ni nini tunakipoteza tunapoendelea kujadiliana mambo ya matukio yanayopita. Kesho litakuja tukio jipya , na tutasahau yaliyotokea leo kama ambavyo IPTL na EPA zilivyogeuka kuwa hadithi.

Tutamsaidia magufuli kama tutalazimisha hoja na mijadala yetu iwe ikijaribu kutatua matatizo yajayo, kuweka misingi itakayowapa watoto wetu nguvu za kushindana kwenye soko la dunia na kutufungua kutoka kwenye minyororo ya madhulumu- ya kihistoria haswa ya kikoloni. Kwa sasa kama alivyosema Msigwa akili ndogo bado inatawala akili kubwa, yaani ushabiki wa kisiasa na story za vijiweni ndo zinaongoza dira ya nchi badala ya malengo ya mda mrefu. Sisi wanajamii tunachangia mapungufu hayo kwa kushangilia vitu vya ajabu visivyo na tija ya mda mrefu. Nakubali kwamba kila mtu ana mambo yaliyo muhimu kwake na huwezi mlazimisha afikirie tofauti.

Tujiulize, je Tanzania ina vijana wenye ujuzi wa kutosha kufanya kazi -pale uchumi wa gesi utakapoanza?

Je, tumejitayarisha kuhakikisha gesi inatengeneza uchumi mbadaala badala ya kuwa malighafi kuimarisha uchumi wa nchi nyingine? Au tutakuwa Nigeria inayohitaji kuagiza mafuta yaliyosafishwa?

Je tumejenga mihimili ya serikali imara inayofanya watu wawe na uchu mkubwa wa kuijenga taifa lao badala ya kuiuza kwa mataifa mengine? Mfano stanbink rushwa

Ni lini tutaacha kuwa watumwa wa nchi nyingine, hatujengi chochote hatuna utaalamu wowote na hatuna nguvu ya kusimama na kusema tunataka mkataba huu uwe hivi kulinda maslahi ya nchi.

Hakuna nchi iliyokuwa kiukweli kiuchumi kama uchumi wake wa ndani ya nchi haujaimarika. Jirani yetu Zambia wanalia kwa sababu uchumi wao umetikiswa na kupungua kwa bei ya coper kwenye soko la kimataifa. Je technolojia ikikua na kufanya gesi ishuke bei tutajilinda vipi? Au tutakubali yaliyotokea kwenye kilimo cha katani pale kamba na magunia ya niloni zilipoingia kwenye soko.

Ni kwa sababu ya mpungufu hayo machache, Stanbink benk inawaibia watanzania kisha inawalipa Uk $36 millioni na Tanzania inapata $7 millioni tu. Na tusisahau rada waliyolipwa $200 million na Tanzania $28m

Sitaki kuandika mengi, nachoomba tu.. tuendelee kuwapa pongezi Magufuli na Majaliwa kwa kazi nzuri wanayofanya ila tusijisahau na kuwa mashabiki wa matukio. Hoja ya msingi inayotakiwa kuwepo kwenye midomo yetu kila siku ni Tanzania gani tunataka kuwaachia watoto wetu. Tuchanganue kila kitu tulichonacho na ni jinsi gani kinaweza kuongeza tija kwa taifa. Na pale kwenye mapungufu tujiulize nini cha kufanya

Hotuba aliyotoa magufuli kwa wafanyabiashara ndo iwe gumzo la mitaani na siyo fulani anavunjiwa nyumba au kufukuzwa kazi kwa kuchelewa. Magufuli anajaribu kuweka dira ya nchi, tumsaidie kuhakikisha kila mtanzania anaimini na kuichangia.
Tusikubali hotuba ya Magufuli iwe tukio jingine, bali iwe dira ya taifa.

Mungu ibariki Tanzania,

Nawakilisha.
 
Jamaa aliyekuwa anamsema ambae aliyejichukulia eneo la wazi sijui ni Manji?, maana ndo alitaka kujichukulia koko beach
 
Jamaa aliyekuwa anamsema ambae aliyejichukulia eneo la wazi sijui ni Manji?, maana ndo alitaka kujichukulia koko beach

Bi Manji, yani kwa hapa nampa tano magufuli, sijui wanataka maskin wakastarehe wapi km maeneo yote wanataka kuhodhi
 
..nashauri uanzishwe uzi (thread) inayoitwa "trash" ili maadmin mliobusy kuhamisha post za watu muwe mnatupia kule kila aina ya uchafu unaowekwa jamvini!. Tunashuhudia watu wanapost picha za ajabu humu mara nesi amelala muhimbili mala makontena mengine haya hapa mara picha za paka amelala mnaziacha zinaendelea ku "crowd" post zenye mashiko. Watu wengine wanafanya uchambuzi kidogo wa speech ambayo lengo lake ni kuchochea mijadala...mnahamisha post zao na kuzificha kwenye thread moja! Bado nashindwa kuelewa weledi unaotumika ni upi kwenye hili, basi chonde chonde mtuwekee na hiyo thread ya TRASH ONLY ili kila machafu iwe rahisi kwenu kuyahamishia huko!!!!
 
Hivi wanachogomeaga hizo efd ni nini?
Wanataka usawa katika biashara. Magufuli anajua wanachogomeaga ndio maana kamtaja Minja pia kasema kwanini zisigawiwe Bure? Ukifuatilia kwa u makini utagundua kuwa wafanyabiashara walikuwa na point Ya msingi. Haukuwa na haki. Haiwezekani we bandarini upitishe mzigo Bure halafu kodi tulipe Sawa na mashine ninunue kwa bei Ya kulanguliwa. Magufuli yupo Sawa na wafanyabiashara wanaofanya biashara za haki watampemda na hawatakuwa na ubishi tena wa kutumia EFD
 
Back
Top Bottom