Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Holiday ya X-Mass na Mwaka mpya mara kadhaa imeleta kizaazaa kwa wapenzi hasa mmoja anapokosa kuwa na uaminifu kwa mwenzake.
Mapumziko ya leo nchana tulitia timu ya watu watano kupata lunch. Maongezi ujuavyo kwa siku hizi ni masimulizi ya matukio ya X-mass, funga na fungua mwaka mpya.
Kioja mmoja kaanza topic ambayo ilituvutia, kwani mdada huyo kasema rafiki zake kadhaa wamekuja kubaini wapenzi wao wana wasichana zaidi ya mmoja na hivyo kusababisha kuvunja mahusiano kwa vile wasingeweza kutoka na wote kusherehekea funga Mwaka.
Dada alikuwa wazi zaidi kwa kutuambia yeye mpenzi wake waliwekeana miadi kwenda kwenye burudani ya fungamwaka na kuukaribisha mwaka mpya. Alimsubiri aje kumchukua na kuona muda unapita na simu yake haipokeleki tena. Akafikiri kapata tatizo labda njiani. Punde tu kapigiwa simu na rafiki yake kwamba mpenzie yupo club nyingine na msichana fulani. Basi dada katoka mkuku kuona kulikoni huko na alipofika tu kabla hajajitosa ndani akamkuta mpenziwe yupo chemba na yule mbaya wake. Kwa vile ni mstaarabu, alimjongelea na kumwambia tu, asante kwa uliyonifanyia na bora ungeniambia ukweli kuliko kunidanganya. Yule msichana aliyekuwa na yule mwanaume akageuka na kuuliza kulikoni? Jibu lake kwa msichana mwenzake ni kwamba, sina ugonvi nawe kwani huyu ni mpenzi wangu lakni hajawa mkweli na ndio maana nimekuja kushuhudia na sasa bora abaki nawe kwa kuwa ndiwe chaguo lake.
Kusikia hivyo msichana mwenzake akatupa manyanga na kumwacha yule kijana peke, wale wakatokomea kwa vile mwenzake alikuwa na usafiri wake uliomfikisha mapema pale wakawa pete na kidole na kumwacha kijana wa watu ameduwaa, badala ya kupata akapatikana, ndo raha ya holiday ilivyowaishia wengine.
Rafiki yangu mzoefu na mambo ya facebook akacheka sana kisha akafungua simu yake na kuonyesha friends wake wa kike ambao wengi wao kuanzia mwaka mpya wameandika went from in relationship to single.