Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,355
- 2,739
wamiliki wa gazeti watakuwa nani...? JF au JF members....?
JF members na ikiwezekana hisa ziwekwe. Tutasonga mbele. Lakini cha kukaa mioyoni mwetu ni kupigania nchi.
we cannot re-invent the wheel, Tayari yapo magazeti yanapigania maskahi ya taifa. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu huko? Na namna nzuri ya kuwekeza nguvu zeti ni kuhakikisha kila mmoij awetu ananunua nakala yake kila wiki. ][/SIZE]
Wazo lako ni zuri naunga mkono hoja, ukiangalia jumla ya members wa jamii forums ni kama 32,000 tu Tanzania nzima ambayo ina wakazi milioni arobaini.
Kwa takwimu hizi ni vigumu watu kuelewa nini kinajadiliwa humu ndani juu ya mustakabali wa maisha na taifa kwa ujumla. Si kila mtu mwenye uwezo/nafasi ya kutumia mtandao sehemu kubwa ya Tanzania haijafikiwa na huduma hii, hivyo basi njia rahisi ya kuieneza JF ni kupitia gazeti ambalo ni rahisi kufikiwa/kusomwa na kila mtanzania.
Ningependa kuona jambo hili linaungwa mkono na wadau wengine humu ndani.
senene
Kwa muda mrefu sasa Jamii Forums imeshajulikana na sifa kemkem imepata. Lakini kwa kiasi kikubwa inajulikana sana kwa wasomi na wachache wenye uelewa wa masuala ya internet. Kwa utafiti nilioufanya japo sio rasmi, nimegundua kuwa tunapokaa sehemu na kuanza kuongea mambo mbalimbali, tunaombwa source, na kila tunapotaja Jamii Forums, wengi na ambao tunawapigania hushangaa na wengine hutaka waione hiyo jamii forum wakidhani kuwa ni gazeti. Sasa ndo nikapata wazo kuwa kazi nzuri tunayoifanya kuipigania nchi yetu, si vibaya na walengwa wakalijua hili. Hivyo mawazo yangu ni kuwa viranja waandae Business Plan nzuri ikiwa na lengo la kuanzisha gazeti. Baadae tukijua gharama za kuanzisha hilo gazeti, kila mwana JF mwenye moyo atajua achangie kiasi gani kwa ajili ya kufanya kitu fulani.
Gazeti hili la jamii forums litasomwa kwanza na sisi wadau na ndio itakuwa njia mojawapo ya kuichangia JF kwa njia rahisi. Sio mbaya gazeti hili hata likitoka mara moja kwa wiki. Wananchi watajua ukweli na harakati zote tunazozifanya. Hii kwa mawazo yangu najua itasaidia sana. Mapambano tunayoyafanya humu yanaonwa na wachache ukisema uanzishe movement wenye taarifa ni wachache. Naomba niwasilishe kwa wadau na mniambie imekaaje hii. Nasubiri comments.
Wakuu,
Tembelea Fikra Pevu | Kisima cha busara! kwa sasa, huenda mkajenga hoja zaidi.
Aidha, nunueni T-shirts za JF ambazo zitakuwa mtaani karibuni katika kuhakikisha JF inakuwa na kipato japo kidogo
Tunazisubili....Wakuu,
nunueni T-shirts za JF ambazo zitakuwa mtaani karibuni katika kuhakikisha JF inakuwa na kipato japo kidogo
kwa mtazamo huu... tungeishia kuwa na gazeti la uhuru, daily news, kiongozi na mfanyakaziwe cannot re-invent the wheel, Tayari yapo magazeti yanapigania maskahi ya taifa. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu huko? Na namna nzuri ya kuwekeza nguvu zeti ni kuhakikisha kila mmoij awetu ananunua nakala yake kila wiki. ][/SIZE]