Fundi mzuri wa suti za harusi Arusha

Fundi mzuri wa suti za harusi Arusha

Kuna jamaa mmoja matata sana anaitwa senzia yupo maeneo ilipo Barclays bank na ofisi za sopa lodge.ukishapita aicc hospital mbele unakunja kulia.ukiuliza utampata.
 
Ukipata fundi Mzuri na kitambaa kizuri za Kutungua hazioni ndani kitu unapimwa according to your body

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo mafundi wengi hawafuati maelekezo ya wateja wao.....

Mimi nilishakoma kushona kwa hawa mafundi wetu wa kiswahili......

Miezi michache ya nyuma nilimpelekea kitambaa changu kizuri cha suti fundi wangu na akachukua vipimo vizuri na mimi nikampa maelekezo ya ziada ya namna suti yangu ningependa iwe, tena nikamuonyesha na sample ya suti ninavyotaka iwe, lakini suti aliyonishonea huyo fundi ikawa kichekesho....

Hadi hivi leo nimekoma kabisa kushona suti wala suruali zangu kwa mafundi......

Hivi sasa mimi nimekuwa mtu wa "kutungua" special za kichina madukani.
 
Ni kweli kabisa suti za kutungua ni nzuri na bei nafuu kama utapata inakutosheleza.

Nimeelekezwa niende dar posta kwa Khimji. Ila bei zake nikipiga na gharama za usafiri kutoka Arusha naona gharama zitakuwa juu sana..

Ndiyo maana nikaona niulizie kwanza kama naweza kupata fundi mzuri hapa Arusha Town.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom