SHILINDE
Member
- Jul 23, 2010
- 14
- 6
Fundi muashi atashangaza sana watu pale ambapo atatumia lugha ambayo atashindwa kuelewana na vibarua na wafanyakazi wake katika ujenzi. lakini ufanisi wa kazi ambao unategemea sana mawasiliano murua utakamilika pale fundi huyu atakapokuwa anatumia lugha ya nyumbani, ambayo vibarua watamuelewa, atumie lugha hiyo hata akienda kununua vifaa vya ujenzi nje ya nchi, kwa kufaya hivo si kwamba hajasoma la haasha..! kusoma sio kuongea lugha za wageni. usomi wake tunaupima wakati wa ujenzi, anavyonyoosha matofali na kuwasimamia vibarua ipasavyo. hatujamuajiri Fundi aongee lugha za kigeni sisi!
Na ifahamike tu kwamba sio kila jambo linatakiwa kubezwa au kubishiwa. hasa na vibarua wanaojenga pagala la jirani. inapofika katika masuala ya Kitaifa na kimaendeleo "mchawi ashikwe lakini haki yake apewe'.
katika hili ambalo Fundi muashi huyu amejipambanua tangu alipopewa tenda ya ujenzi na kuonesha thamani ya kiswahili ndani na nje ni la kumuunga mkono.
fundi huyu ameonesha njia, sasa wenye dhamana za kukuza kiswahili lugha hii adhimu wakiwemo Wizara ya Elimu, Baraza la Kiswahili, vyuo na taasisi mbalimbali waweke na kusimamia mikakati pia kwani lugha hii ndio utambulisho wetu, ndio alama ya umoja wetu na historia ya kujivunia.
mtu yoyote asiyethamini au kutokujua historia yake ni sawa na mti ambao hauna mizizi.
[HASHTAG]#Proudly[/HASHTAG] Swahili