Fundi muashi anapobadilisha mawe

SHILINDE

Member
Jul 23, 2010
14
6
Sioni kama ni tatizo pale Fundi Muashi anapoamua kutumia jiwe kujengea ukuta ambalo kwenye msingi aliona halifai, kwa manguli wa wajenzi wataungana na mie katika hili.

jiwe lilionekana kutofaa kwenye msingi linaweza kufaa kwenye ukuta, sasa utashangaza watu wakianza kumtangazia fundi huyu kwamba hajui atendalo. fundi huyu katumia ueledi wa ki ukandarasi katika kuamua kuchukua na kulitumia jiwe hilo.

lakini pia misaafu iliandika jiwe lililoachwa na mjenzi likawa ndio jiwe la kona ya msingi, sasa fundi huyu ameona asiliache jiwe ambalo linaweza tumika pia huku juu.

"FUNDI MUASHI ANAENDELEA KUJENGA'
 
Nimeelewa ila pia ifike mahala fundi aone aibu maana wakati analiacha jiwe kwenye msingi alilikana na kuonyesha mbwembwe kibao kuwa hilo sio jiwe bali ni dongo tuu na sie hatujengi nyumba ya udongo....

anyway pia alipoliacha jiwe mama na baadae akaja kulitoa jiwe mtoto tuliamini kuwa mwamba unaotoa hayo mawe yanayokataliwa na fundi mkuu haufai kama tulivyoaminishwa na fundi huyohuyo.

Angalizo langu ni kuwa fundi mkuu awe na akiba ya maneno na pia muda ni tiba ya matatizo mengi ya mwanadamu....

ajifunze kutumia hekima na busara kisha ije haki na sheria iwe ni ya mwisho kabisa katika utendaji wake la sivyooo.....FUNDI IPO SIKU ATATUMIA JIWE ALILOLIKATAA KUWEKA KWENYE PAA BADALA YA KUGONGA MISUMARI.
 
Bahati mbaya inakuja pale unapojenga msingi kwa tofali za kuchoma, halafu unatumia mawe kunyanyua ukuta...

Lazima ukuta ushuke tu.
 
Ni kweli unaweza tumia tofali/jiwe ulilikataa awali ila kwa fundi yule bure kabisa, nasema bure kabisa anachukua jiwe alilolitoa ukutani tena akidai lina kinyesi.
Bure kabisa fundi yule na nyumba nzima imeharibika si kwa ubaya wa jiwe lile ila kwa sababu ya mwashi yule na hafai kupewa tenda zaidi next time.
 
Jiwe alilitumia katika ujenzi wake lakini likashindwa kufit kwenye msingi wake. Sasa kalichanganya kwenye zege,kila mtu anamsifia.
 
Sioni kama ni tatizo pale Fundi Muashi anapoamua kutumia jiwe kujengea ukuta ambalo kwenye msingi aliona halifai, kwa manguli wa wajenzi wataungana na mie katika hili.

jiwe lilionekana kutofaa kwenye msingi linaweza kufaa kwenye ukuta, sasa utashangaza watu wakianza kumtangazia fundi huyu kwamba hajui atendalo. fundi huyu katumia ueledi wa ki ukandarasi katika kuamua kuchukua na kulitumia jiwe hilo.

lakini pia misaafu iliandika jiwe lililoachwa na mjenzi likawa ndio jiwe la kona ya msingi, sasa fundi huyu ameona asiliache jiwe ambalo linaweza tumika pia huku juu.

"FUNDI MUASHI ANAENDELEA KUJENGA'
Mungu wangu bado hujaona nyumba ya miti halafu juu flat roof na jamaa anakwambia maganda ya miwa ni matamu kuliko miwa?lakini mkuu nakushukuru sana maana nilikua usingizini umeniamsha
Wachache wataelewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom