Fundi Abomoa Nyumba ya Jamaa Aliyekataa Kumlipa Pesa Zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fundi Abomoa Nyumba ya Jamaa Aliyekataa Kumlipa Pesa Zake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Sep 24, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  September 24, 2009

  Fundi ujenzi wa nchini Uingereza mwenye hasira ya kutolipwa pesa zake akishirikiana na mwanae alitumia masaa sita kulibomoa paa la nyumba aliyomaliza kuijenga baada ya mwenye nyumba kugoma kumlipa pesa zake.

  Fundi ujenzi wa Uingereza Roydon Toon mwenye umri wa miaka 59 akishirikiana na mwanae Gavin, 33, walilibomoa paa la nyumba waliyoijenga huku mwenye nyumba na familia yake wakiwa ndani.

  Toon na mwanae waliamua kulibomoa paa la nyumba hiyo yenye thamani ya £450,000 (Zaidi ya Tsh. Milioni 900) baada ya mwenye nyumba kugoma kuwamalizia pesa walizokuwa wakimdai tangia walipomaliza kazi yake ya ujenzi miaka mitano iliyopita.

  Toon na mwanae walitumia masaa sita kung'oa vigae vya paa la nyumba hiyo na kukata mbao zinazolishikilia paa hilo huku magari ya polisi zaidi ya 10 na helikopta moja angani zikiwa zimewazunguka.

  Toon alianza shughuli ya uharibifu kwenye nyumba hiyo iliyopo kwenye mji wa Barlborough kuanzia saa mbili asubuhi na aligoma kuwasikiliza polisi waliokuwa wakimuamuru ashuke chini.

  Waliendelea kufanya uharibifu huo mpaka mida ya mchana waliposhuka chini na kukamatwa na polisi kwa kosa la jinai la kufanya uharibifu kwa nia ya kuhatarisha maisha ya watu.

  Toon alisema kuwa alikuwa akimdai mmiliki wa nyumba hiyo James Arthur kiasi cha paundi £47,000 kwa ujenzi wa vyumba vya ziada katika jumba lake la kifahari.

  Toon alisema kuwa bwana Arhur alimlipa kiasi cha paundi 32,000 na kukataa kumalizia deni la paundi 15,000 baada ya kazi ya ujenzi kumalizika kwasababu kulikuwa na gesi inayovuja katika mojawapo ya vyumba vipya vilivyojengwa.

  Toon alisema kuwa kabla ya kufanya uharibifu huo alimtumia Arthur barua akimtaarifu kuwa atafanya uharibifu huo kwakuwa amegoma kumlipa pesa anazomdai kwa miaka mitano sasa.

  Akiongelea kukamatwa kwake Toon alisema "Nashangaa hatua ya polisi kutukamata, hakutaka kulipa deni , nilimtumia barua kumtaarifu uamuzi wangu lakini alinipuuza".

  "Kulikuwa na helikopta ya polisi angani iliyotuzunguka muda wote huku magari 10 ya polisi yakitusubiri tushuke chini. Sijutii chochote nilikuwa natafuta haki yangu" alimalizia Toon.

  Toon na mwanae walitupwa mahabusu kwa muda mfupi na baadae waliachiwa huru kwa dhamana huku wakiwa wameishamtia hasara kubwa mwenye nyumba zaidi ya pesa wanazomdai.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Looks like dawa sahihi kwa wazulumaji....ha!ha!ha!aa
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehehe hii sawa na jamaa mmoja siku ya Idd Mbezi beach alikuwa analinda jumba la mfanya biashara mmoja sasa alikuwa amelima kibustani cha mboga bill ya maji ikatoka jamaa anadaiwa 100,000/= yule mwenye nyumba alikuwa bado hajahamia akamwambia yule mlinzi wake alilipe hilo deni kwani maji alikuwa anatumia yeye kwenye mboga jamaa akakataa basi ukawa ugomvi yule mwenye akamwambia jamaa anamfukuza kazi na kuleta walinzi wa security.

  Yule mlinzi kuona hivyo akajua kazi hakuna akamwomba tajiri wake pesa ya sikukuu tajiri akakataa basi siku ya Idd jamaa akapiga mnazi na gongo akachukua ubao akaanza kubomoa vioo nyumba nzima kuanzisha chini mpaka gorofani alafu akakimbia tajiri kuja asubuhi anakuta nyumba haina vioo hasara yake ina karibia milioni 20 nyumba nzima kisa maji ya laki moja.
   
 4. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dah! huyo naye alikuwa noma.
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  teh teh teh,,,,, fundi anatakiwa apewe tuzo ya ujasiri
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ubahili sio mzuri kwakweli.
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Salut! kwa fundi manake mie kuna kampuni ya wazungu naidai wananizungusha kitambo toka mwaka jana naona bora nichukue uamuzi kama wajamaa manake ukileta usomi na ustaarabu unaumia tu.

  Safi sana fundi! manake ukienda mahakamani itakucost zaidi bora mkose wote na mahakamani aende yeye, kwani nini bora kichafuke
   
 8. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Ha ha ha.
   
 9. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  mi mjasiriamali, wewe fisadi unaniletea urembo kwenye changu!! nakuzingua tu, kama vipi vipi tu kwa bei yoyote, hasira hapa mtaani muhim, la sivyo utaota sugu bila fweza yoyote. mah!!
   
 10. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mafundi wanapewa new technics sasa. Kazi ipo
   
Loading...