Fumanizi: Epuka wanaoshauri kuachana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumanizi: Epuka wanaoshauri kuachana!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 9, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Fumanizi husababisha hisia zenye maumivu, hasira, kutokuaminiana, woga, aibu na kujilaumu. Lakini kufumania au kufumaniwa hakupaswi kuwa sababu ya kuwa mwisho wa ndoa yenu, ingawa kunaweza kuwa pia.

  Baada ya fumanizi, inabidi ujitahidi kuelewa na kuweza kujenga tena ndoa yako, pengine sasa ikiwa ni ndoa imara zaidi. Hata hivyo hii inataka kujituma kwingi na uvumilivu na subira .

  Ndoa inaweza kuendelea hata baada ya fumanizi kwa kutumia ushauri, kupeana muda na kushirikiana. Kuna ndoa ambazo zimeweza kudumu zaidi baada ya fumanizi kutokea.

  Pale kutoka nje kwa mwanandoa mmoja kunapogundulika hupelekea hisia kali kwa wanandoa wote, mshtuko, aibu, kujilaumu, kujiona mkosaji, hasira kali na wasiwasi. Kutokana na hisia hizi zote mara nyingi wengi hufanya maamuzi yasiyo mazuri kama kutengana au kuachana kabisa.

  Badala ya kufanya hivyo katika kipindi kile cha muda mfupi baada ya fumanizi, tunahitaji kuwa watulivu sana ili tuweze kuchukua hatua zinazofaa.

  Kupata msaada:
  Kwa uzima na afya yako mwenyewe, tafuta msaada kutoka kwa familia, rafiki, mchungaji, shekhe au mshauri yeyote unayemwamini wewe na kujihisi huru kwake. Kuongea kuhusu hisia zako kwa wale unaowapenda sana itakusaidia wewe kupunguza nguvu za hisia za maumivu ya tukio hilo. Kuongea na watu wengine kunaweza kukupa wewe uwezo wa kuelewa zaidi hisia zako na kupata mtazamo mwingine kuhusu tukio.

  Pengine aliyetoka nje inawezekana hatosheki katika mahusianao katika ndoa yake au hawajibiki vizuri katika ndoa. Au pengine hawezi kudhibiti mihemko yake.

  Mabadiliko ya maisha kama kuzaliwa mtoto au upweke wa aina fulani, unaweza kuwa ndio sababu ya kutoka nje. Inabidi haya yatazamwe kabla mtu hajaamua lolote.

  Kwa hiyo kujua sababu ya mwingine kutoka nje ni muhimu sana na hii inaweza kukupa ahueni, kwani unaweza kubaini kitu ambacho kinaonesha kwamba, kwako pia kuna matatizo.

  Hatua zitakazokusaidia kujenga upya ndoa yako baada ya fumanizi ni nyingi. Lakini hizi ni baadhi tu ambazo kwa mazingira yanayokukabili, zinaweza kukusaidia.

  Kuacha kutoka nje ya ndoa:
  Hatua ya kwanza ni kwa mwanandoa kuacha tabia ya kutoka nje ya ndoa kiukweli.

  Kukubali kuwajibika:
  Kama umetoka nje ya ndoa, kuwa tayari kuwajibika katika vitendo vyako.

  Onyesha nia ya malengo yako:
  Kuwa na uhakika kuwa wote wawili mko tayari kujenga upya ndoa yenu.


  Onana na mshauri wa wanandoa:
  Mtafute mshauri wa ndoa ambaye atakusaidia kujenga upya ndoa yako kama itakuwa inahitajika. Onana na mshauri wa ndoa ambaye alishawahi kukutana na kusaidia kutataua matataizo ya fumanizi. Mwepuke mshauri ambaye anaamini kufumania au kufumaniwa ndio mwisho wa ndoa yenu.

  Kuchunguza tatizo:
  Kufumania au kufumaniwa huzua matatizo katika ndoa. Chunguzeni kwa makini mahusiano yenu ili uweze kujua nini kilichosababisha au kilichopelekea kutoka nje ya ndoa na nini mfanye ili kuzuia kutoka nje ya ndoa tena


  Kila mmoja apewe nafasi:
  Kila mwanandoa anahitaji kupumzika kwa ajili ya kuondoa msongo na wasiwasi kutokana na tukio la fumanizi, hii ni kwa sababu huwa ni vigumu kusikiliza ushauri wakati mihemko iko juu sana.

  Pata muda:
  Epuka kujua undani zaidi kuhusu fumanizi la mwenzi wako kwa wakati wa mwanzoni. Ahirisha mjadala huo kwanza mpaka uzoee ile hali ya kumfumania mwenzi wako.

  Mwisho wa ndoa au hapana ?
  Siyo kila ndoa iliyoguswa na suala hili la fumanizi ni lazima imalizike kwa kutokuachana. Wakati mwingine kunakuwa na uharibifu mkubwa na wanandoa hawana budi kuachana na pia kama wanandoa hawako tayari kuwa pamoja tena.

  Lakini kama wote mko tayari kujenga upya ndoa yenu, basi suala hili huwa rahisi sana na uhusiano utaendelea kuwa mzuri na wa amani zaidi.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  sasa wewe unataka mtu afanyaje..
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kuna fumanizi la dharau ambalo kwa hali yoyote unalazimika kujiweka pembeni. Usiombe yakakukuta hayo wewe! Nami siombi yanikute japo du! We acha tu!
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Nilinusurika kukutwa - siwezi rudia na siwezi sahau!!!
   
 5. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi anachokisema kina logic,sio lazima kila fumanizi lipelekee kuachana, lakini endapo wewe uliyefumania uko tayari kuendelea na mahusiano labda kwa vile unampenda sana mwenzio,ni lazima uwe makini kuchunguza ili kujua kama msaliti naye yuko tayari kuendelea na mahusiono! Epuka kuonyesha dalili zozote za kulazimisha muendelee na mahusiano! Kwa mf; unaweza kumfumania mwenzako,ukataka akueleze nini hasa sababu lkn yeye akawa hayuko tayari kueleza! Au mwingine haongei chochote,yaani kosa halikili wala msamaha haombi anang'ang'ania tu yaishe yaishe basi! Kuendelea na mahusiano na mtu kama huyu ni hatari!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Fumanizi:Fanya maamuzi binafsi!!
   
 7. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi anachokisema kina logic,sio lazima kila fumanizi lipelekee kuachana, lakini endapo wewe uliyefumania uko tayari kuendelea na mahusiano labda kwa vile unampenda sana mwenzio,ni lazima uwe makini kuchunguza ili kujua kama msaliti naye yuko tayari kuendelea na mahusiono! Epuka kuonyesha dalili zozote za kulazimisha muendelee na mahusiano! Kwa mf; unaweza kumfumania mwenzako,ukataka akueleze nini hasa sababu lkn yeye akawa hayuko tayari kueleza! Au mwingine haongei chochote,yaani kosa halikili wala msamaha haombi anang'ang'ania tu yaishe yaishe basi! Kuendelea na mahusiano na mtu kama huyu ni hatari!
   
 8. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Msamaha unawezekana tu kama sababu za kutoka nje zimewekwa bayana na aliyetoka nje ya ndoa amekiri kwa dhati kuwa hatorudia. Haina maana kumsamehe mtu ambaye ataendelea na uzinzi tena na same person kwa maana ya kuwa ameshaweka kiota kwa hiyo nyumba ndogo/kidumu. Kuna wengi wakibambwa wanaomba msamaha na inakuwa ni kikomo cha tabia hiyo ya kutoka nje. Na inabidi ufanye uchunguzi wa kina kujua kama aliyefumwa ni kweli kaachana na huyo mzinzi mwenzie; ni rahisi kufuatilia kama umeshajua mwizi wako ni nani.

  Kusameheana wakati uzinzi unaendelea si msamaha ila ni kukubali matokeo (aka compromise) kitu ambacho mimi sioni kama ni sawa.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  La heshima je, lipo?
   
 10. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna fumanizi watu wanakuja na mabouncer na kumbaka mtuhumiwa mfululizo hili nalo unalichukuliaje? unaweza kuendelea na mwenzako aliyebakwa?
   
 11. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  La heshima labda mume kaenda na suit, hahahaaaa halafu anaongea taratiiibu bila ku shout
   
 12. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi,inakuaje mtu umeowa au kuolewa unakuwa na tamaa tena ya kuwa na kidumu au vidumu! Tz bila vvu itawezekana kweli?
   
 13. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  bora uuulize mwaya,mie naona tusioane tunadanganyana tuuu....
   
 14. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Fumanizi nyingine mitego, we wasusa wenzio twala
   
 15. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  maji ya kidumu ni kwa kazi ndogo ndogo tu, ndio maana huku uswazi vina chati sana hivyo vidumu
   
Loading...