Full tutorial: Tengeneza Paypal na link na kadi yako ya benki

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,715
39,801
Ukitaka kufungua paypal inabidi ufuate njia hizi

1. visit website ya paypal
Nenda http://paypal.com ukifika utaregister acount na kila kitu i hope haitakushinda. Hakikisha unatumia email ya ukweli na kama unafanya real business ni bora ikawa email ya siri unayoijua wewe tu ili kuepuka wizi.

2. Nenda benki yako husika
Mfano mimi nilitumia crdb nilienda bank nkaomba waifungue card yangu ya master card ili itumie internet (visa pia inakubali) kuna fomu watakupa ujaze itataka card namba (sio acount) kujua kadi namba utaona chini huko. Ukimaliza kujaza wape fomu yao na waulize itakua tayari baada ya muda gani?. Mara nyingi baada ya masaa 24 inakua tayari.

3. rudi tena website ya paypal
Hapa ushakua member so wewe utalogin tu ukilogin utaona message ya kuverify card yako click hapo na ingiza details za card yako ambazo zitakua

-card no (sio account no)
VisaDebitImage_Features.jpg

Herufi B ni card no
Herufi D ni jina na expiry date
-Utaeka na expire date kama inavoonekana
-utaeka digit 3 za nyuma kama inavoonekana kwenye picha chini.
security_code_visa.png

Ukimaliza watakukata dola 1.94 na watataka uiverfy card kwa benk statement.

rudi benki baada ya siku 3
Mambo ya online yanachelewa baada ya sku tatu statement yako itakua tayari sorry sipo njiani ila nkipata muda ntawatumia picha namna ya kuisoma hio code ila hapa ntawaonyesha theorotically
Ipo namna hii

++++++++pp*xxxxCODE

Huo ndo mfano wake code ya kuverify inakaa kati ya neno pp* na neno CODE yani hizo xxxx zinakua 4

5. Rudi paypal
Hapa utaclick tena verify then utaingiza hizo 4 code then ur done paypal ipo integrated na card yako.

how it works?
Bahati nzuri nimenunua domain na hii njia. Na fata njia hizi na wewe kununua safe.

-kwanza ingia website ya kununua hicho kitu unachotaka then chagua malipo kwa paypal

-utaletwa page ya malipo ya paypal ingiza details zako za paypal (username na pass). Hakikisha adress juu ni paypal na ipo katika secure conection

- ukisha login utaona card yako pale select it kufanya hayo manunuzi na paypal wao watakata hela bila wale jamaa unaonunua kwao kujua details za acount yako

- utamaliza manunuzi na kusubiria siku 3 tena ili bank yako ihamishe hizo fedha.

Hii ndo njia salama ya kununua vitu online kama una tatizo usisite kupost chini.
Scan.jpg
 
Nashukuru sana nimesha register PayPal bahati nzuri Card yangu ya CRDB ni MasterCard na niliisha register kwa huduma za internet Banking,nimeshaanza na kununua Software online.
 
Nashukuru sana nimesha register PayPal bahati nzuri Card yangu ya CRDB ni MasterCard na niliisha register kwa huduma za internet Banking,nimeshaanza na kununua Software online.

Tupo pamoja nashukuru kwa kuleta feedback
 
Mkuu ishu huwa inakua Benki kwenye kutrace ile Code sababu ideally kwenye statement zetu tunazopewa huwa haionekani mkuu.

Hiyo ni mpaka wadau ndo wanaweza ku spool out hiyo statement inayoonyesha secreat message yenye code
.

Wengi wamekwama hapo kwenye code mkuu.
 
ningependa kufahamu je,ukishanunua kitu online,kwa mfano,laptop au headphones huku bongo,utavipataje,posta,au,unaletewa ulipo,inakuwaje?
 
ningependa kufahamu je,ukishanunua kitu online,kwa mfano,laptop au headphones huku bongo,utavipataje,posta,au,unaletewa ulipo,inakuwaje?

Kama upo Tanzania, ni changamoto kweli kweli....unachotakiwa kufanya ni kwamba, kabla huja-bid kitu chochote(tangible) online, anza kwanza kuwasiliana na seller na mwulize endapo anaweza ku-ship hiyo kitu hadi Tanzania. Sellers wengi hawa-ship bidhaa kuja huku kwetu lakini kuna wengine wanaweza ku-ship.
 
Kama unatumia Ebay... Seller huwa anaeleza kama anaship worldwide au US pekeee nk pia anasema Nchi ambazo hawezi kuship by any means.
 
Kama unatumia Ebay... Seller huwa anaeleza kama anaship worldwide au US pekeee nk pia anasema Nchi ambazo hawezi kuship by any means.

Ni kweli, lakini kuna wengi tu wanasema wana-ship worldwide wakati kwenye baadhi ya nchi hawafanyi!! Wale wanao-locate US ni kwavile ni free shipping there4, kama una-organise nao at ur expense some can ship the item provided uwezekano huo upo-----those people are doin business, so we kama ume-bid mzigo wa thousands of dollars na kuna possibility ya kufanya shipment; they can do it!
 
yep thats right have u ever heard about This

I want to try it kwa wale ambao hawataki kabisa kuship huku kwetu na wana items nzuri
 
mkuu email ya siri na ambayo sio ya siri zitatofautianaje? Make mimi najua siri ya account ni serial number yako.
 
mkuu email ya siri na ambayo sio ya siri zitatofautianaje? Make mimi najua siri ya account ni serial number yako.

unapofungua account paypal email adress yako ndio inakua kama username na unaweka na password.

Ntakapoona email adress yako ntajua ulipofungulia lakini ukieka siri email yako (usiri huu ni wewe ndo unauweka na sio kuna email za siri) yani usimwambie mtu yoyote ujue hata watu kukuibia acount itakua ngumu.

Mfano nimeijua email yako ni mimi@sisi.com moja kwa moja najua umefungulia sisi.com so nahack sisi.com napata pass zako then naenda paypal kuforgot password napata pass yako ya paypal then nakuibia account. Thats why nkasema kama business ni serious better hata email ueke ya siri
 
Sa mi mzembe kuweka pesa benki..... mtanifanya nifanye hvyo je vipi kufungua USD A/C coz zetu nitsh na wanakata usd so u cant buy anything with TSHS
 
Sa mi mzembe kuweka pesa benki..... mtanifanya nifanye hvyo je vipi kufungua USD A/C coz zetu nitsh na wanakata usd so u cant buy anything with TSHS

Automatic zinakua converted kua usd tena zinakua cheap si unajua benk wana viwango vidogo vya ku exchange fedha za kigeni
 
Back
Top Bottom