figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,653
- 59,077
Salaam Wakuu,
Hapa chini nimewawekea hotuba nzima ya Luhaga Mpina bila kuchakachua kitu.
Angalizo, hii Hotuba ilitolewa tarehe 27 Oktoba, lakini Document ya hotuba imetoka leo. Naipost hapa kuweka kumbukumbu sawa kwa Vizazi vijavyo kwa Matumizi ya Shule na kuwajengea watu wa Dunia ufahamu na Uhalisia wa Siasa za Tanzania
Twende kazi...
1. UTANGULIZI
Leo tarehe 27 Oktoba 2025 natoa hotuba yangu hii ikiwa nchi zetu za
Afrika Mashariki zikiwa kwenye huzuni na majonzi makubwa kufuatia Kifo cha Mwanasiasa Maarufu na mpigania Demokrasia wa kweli nchini Kenya na Afrika kwa ujumla, Hayati Raila Amolo Odinga ambaye aliaga dunia tarehe 15 Oktoba 2025 akiwa kwenye matibabu nchini India na amezikwa kwa heshima zote za kitaifa Kijijini kwake Bondo Kaunti ya Siaya nchini Kenya.
Nichukue nafasi hii kuungana na Wananchi wa Jamhuri ya Kenya, Wana Afrika Mashariki na Dunia nzima kuomboleza Msiba huu mkubwa ambao umetutia majonzi na simanzi kubwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu
ampe pumziko la amani Mzee Wetu, Raila Amolo Odinga, wengi
tulipenda kumuita BABA.
Hayati Raila Odinga atakumbukwa kwa namna alivyoongoza harakati za kujenga mfumo wa Vyama vingi vya Siasa, alitetea hadi kufanikisha kupatikana Katiba Mpya ya Kenya mwaka 2010 iliyotoa uhuru na demokrasia zaidi.
Raila alitumia maisha yake kujenga upinzani wa kweli na wa Kikatiba uliosaidia sana kubadilisha mwelekeo wa siasa nchini Kenya.
Aliwahi kufungwa jela kwa miaka kadhaa kwa makosa ya uhaini
kutokana na msimamo wake wa kisiasa lakini hakuwahi kukata tamaa na aliheshimika ndani na nje ya Kenya kama mtu aliyejitolea kwa ajili ya nchi kuliko maslahi binafsi.
Alikuwa zaidi ya mwanasiasa, alikuwa mwalimu wa siasa, mzalendo wa kweli na mtu ambaye alitumia maisha yake yote kutetea wanyonge.
Huyu ndiyo Raila Amolo Odinga ninayemfahamu mimi. Lala salama Baba wa demokrasia Raila Amolo Odinga. Mbegu za kusimamia ukweli, kupiga vita rushwa na ufisadi na kutetea wanyonge alizopanda zitaendelea kumea kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bara zima la Afrika. Pole sana familia, pole sana Rais wa Kenya, Mhe. Dk. William Samoei Ruto, Poleni sana Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na Wakenya wote kwa ujumla.
2. KUKATA RUFAA MAHAKAMA YA RUFAA
Ndugu Wananchi, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 5 Agosti, 2025 Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliwateua Ndg. Aaron Kalikawe na Luhaga Joelson Mpina kuwa wagombea nafasi ya Rais ambapo katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo uliofanyika tarehe 6 Agosti 2025 Mlimani City jijini Dar es Salaam wajumbe wa Mkutano Mkuu walinichagua kwa kura 559 kati ya Kura 610 zilizopigwa na kupata ushindi wa 92.3% huku Ndg. Kalikawe alipata kura 46 sawa na 7.7%.
Kwa matokeo hayo Chama kilinichagua mimi Luhaga Joelson Mpina kuwa Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa tiketi ya ACT Wazalendo na baadaye Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilinikabidhi Fomu ya uteuzi mnamo tarehe 15 Agosti 2025 kwa ajili ya kutafuta wadhamini katika mikoa
10, kuapa Mahakama Kuu ya Tanzania na kulipia kiasi cha Tsh. 1,000,000 hatua ambazo nilizikamilisha kikamilifu.
Ilipofika tarehe 26 Agosti 2025 saa 11 jioni Msajili wa Vyama vya Siasa
aliandika barua ya kubatilisha Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo ya kuniteua kuwa Mgombea wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na siku hiyo hiyo tarehe 26 Agosti 2025 saa 5 usiku Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) nayo iliandika barua ya kunizuia
kurudisha fomu kesho yake tarehe 27 Agosti 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya uteuzi wa wagombea wote nafasi ya Rais na Makamu wa Rais.
Baada ya uamuzi huo wa INEC wa kunizuia kurejesha Fomu mimi na Chama changu cha ACT Wazalendo tulifungua Shauri la Kikatiba Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dodoma kupinga uamuzi huo ambapo ilipofika Tarehe 11 Septemba 2025 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dodoma ilitoa uamuzi wa shauri hilo kuwa nilionewa na sikupewa haki ya
kusikilizwa na nilienguliwa kinyume cha Sheria na kuagiza INEC ipokee
fomu zangu na kuendelea na mchakato wa uteuzi pale ulipoishia.
Mnamo tarehe 13 Septemba 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilipokea Fomu zangu za Uteuzi katika Ofisi za INEC zilizoko jijini Dar es Salaam na kuniteua kuwa Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama changu cha ACT Wazalendo.
Baada ya kuteuliwa na INEC kugombea nafasi ya Rais niliwekewa Mapingamizi matatu (3) ambapo pingamizi la kwanza liliwekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ndg. Hamza Said Johari ambapo kwa maoni yangu aliyeniwekea pingamizi hili ni Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk. Samia Suluhu Hassan, Pingamizi la pili liliwekwa na Mgombea Urais wa Chama cha NRA, Ndg. Almas Hassan Kisabya na pingamizi la tatu liliwekwa na Mgombea Urais wa Chama cha AAFP, Ndg. Kunje Ngombale Mwiru.
Inashangaza kuona wagombea wa nafasi ya Rais watatu kuniwekea pingamizi baada ya kuteuliwa na fomu zangu kuwekwa kwenye ubao wa matangazo wa INEC lakini wakati wagombea wenzangu 17 wanateuliwa hakuna aliyewekewa pingamizi hata mmoja. Kwanini Mpina? Kwa kosa
gani? Na kwa manufaa gani? Ni manufaa ya Taifa au manufaa binafsi?
Nimechukulia kwa uzito mkubwa taarifa aliyoitoa hivi karibuni Mwanasiasa Mkongwe na Mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini, Mheshimiwa Suleiman Said Bungala (Senior) kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa amekuwa akitumika kutengeneza migogoro ndani ya Vyama vya upinzani
ili kudhoofisha demokrasia na nguvu ya upinzani nchini.
Kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia michakato ya uchaguzi ndani ya Vyama vya upinzani na kujigeuza kuwa mtoa maamuzi na hukumu bila kujali utaratibu uliowekwa Kikatiba, Kikanuni na miongozo katika kufikia maamuzi ya vyama hivyo, kutengeneza taarifa za uongo na
kuzifanyia kazi ni mambo yanayostaajabisha sana.
Fungua kiambatanisho HAPA kusoma Hotuba yote ya Ndugu Luhaga Mpina.