Fukuza Marekani nchini

Ona aibu hata kidogo basi! Hata hiyo internet unayotumia ya kwao. Aliye kuzidi kakuzidi tu! Maneno matupu hayavunji mfupa!
Unataka kusema hata wakitaka kumuzimia internet hatutapata mawazo yake sio? subiri wamuzimie internet.
 
Kwahiyo tatizo ni sisi sio wao? hilo nalo ni shida
 
Hata kwa Ebola WHO ilibatilisha usemi wao
 
Kwahiyo tatizo ni sisi sio wao? hilo nalo ni shida
Wametuzuia vipi kuendelea wakati tuna mali kuliko wao.Mfano Congo DRC tu ndio nchi ya kwanza kwa Mali asili duniani utake nini ukose si mafuta ,gas,bandari,maji,madini,ardhi.Jiulize wakoloni waliweza vipi kutuletea maendeleo na sisi tunashindwa vipi kujiletea maendeleo kwa hali na mazingira yaleyale waliyoweza wakoloni?
 
Hawa inabidi tuseme nao kisela tu ndio watatuelewa.
Nalog off
 
Sasa mbona hili nalo ni jipya. Yani Duniani maliasili nyingi Mungu aliziweka Africa sio kwa wazungu? Sasa mbona Africa ndo kwenye umasikini zaidi kuliko kwa wazungu? Au tulivyotawaliwa na wazungu zamani kuna vyakula walitulisha tukawa hivi tulivyo?
 
Baada ya miaka 20 ijayo ukirudia kukikusoma ulicho kiandika hapa lazima upate sononeko kubwa sana. Mambo mengi yaacheni kama yalivyo, dunia mkia wafisi, ukiushika ukuasi.
 
Sasa mbona hili nalo ni jipya. Yani Duniani maliasili nyingi Mungu aliziweka Africa sio kwa wazungu? Sasa mbona Africa ndo kwenye umasikini zaidi kuliko kwa wazungu? Au tulivyotawaliwa na wazungu zamani kuna vyakula walitulisha tukawa hivi tulivyo?
Africa haijapata mfumo sahihi Wa uongozi,uliopo unapwaya na ndio chanzo cha umasikini wetu.
 
Mleta made unajua unachkongea kweli. Waulize wazimbabwe kilichowakuta. Chezea nchi nyingine lakini siyo marekani. Marekani akituwekea vikwazo jua pia washirika wake watatuwekea vikwazo. Zimbabwe wallenda kwa wachina baada ya kuwakaribisha kama investor kumbe wakawa wanaiba tu na uchumi wake ukaelekea shimoni. Mpaka Leo wameshindwa kutoka shimoni.
 
MKUU YOU MADE UP MY DAY.
EBU PATA KINYWAJI NALIPIA.
 
Tahadhari wamepewa raia wa Marekani ila mapovu wanayatoa raia wa Tanzania tena kutoka huko Matombo na Nanguruwe.

Mkuu waliopewa Tahadhari ni raia wa Marekani sasa wewe unaumia vipi? Je Tanzania kuwapa tahadhari raia wake waishie Marekani kuwa kuna ubaguzi wa rangi na wawe makini ni kosa? Je huoni huo ni kama upendo usiomithirika kwa raia wetu?

Je wewe unaona lile Tangazo la mkuu wa mkoa wa Dar la kuwasaka mashoga nyumba hadi nyumba Marekani hakuwa na umuhimu wa kuwapa tahadhari raia wake ambao wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuwa wakitembelea Tanzania wanaweza kukamatwa?

Hivi wakenya wakiwapa tahadhari raia wake kuwa Tanzania kuna mauaji ya maalbino ili kuwapa alert raia wake wenye albinism watembeleapo Tanzania watakuwa wanakosea?

Mkuu, kama sisi hatuna hizo tamaduni za kuwalinda/kuwajali raia wetu walioko nje au wanaopanga kwenda nje basi usilazimishe hiyo kasumba na wenzetu wawe nayo, sisi tumechagua kuishi hivyo na wamarekani wanaishi hivyo so tuwaache waishi wapendavyo bila kuwapangia mambo yao.
 
Vyombo vya magharubi vimefanikiwa kukufanya usijitambue.Pole.
 
Mimi naona Mabeberu ya humu ndani Ni mabaya na maovu kuliko Marekani. Mabeberu yanayoua na kuskomeza watu kwenye viroba, yakipiga watu risasi hadharani mchana, hayawezi kushindwa kuficha chochote!!!
 
Msaada gani wanaoutoa kwetu? Acheni uzushi!
China pamoja na kuwa imetuzidi kwa uchumi na technolojia lakini company mmoja ya Marekani Google ilitetemesha nchi nzima. Palikuwa hapatoshi China. Kiufupi China ilitia huruma.
Sasa wewe kajamba nani unakimbizana na ukosefu wa madawati unaanza kuivimbia Marekani. Kila kitu unachotumia ni cha mabeberu. Hapo ulipo unapata hivyo vihela na wewe unaona umefika. Hawa mabeberu waache kama walivyo. Hii JF unayotumia bila mabeberu hata usingeiona. Mimi napata pesa kutoka kwenye makampuni ya mabeberu kama Propeller ads na ad.fly. Search engine unatumia ya mabeberu, movie unaangalia za mabeberu, elimu umeipata ya mabeberu. Bila mabeberu sasa hivi ungekuwa unachunga ng'ombe. Huwa unaangalia video YOUTUBE? Unaishi kwenye dunia ya 3 kwahiyo kuwa mpole.
 
Vyombo vya magharubi vimefanikiwa kukufanya usijitambue.Pole.
Huo ndiyo ukweli. Wewe kajamba nani tangu 1961 unakimbizana na madawati na maji. Uhaba wa matundu ya choo kwenye shule unakutoa jasho halafu leo unataka kuanzisha ligi na Marekani. Aisee
 
Nimejaribu kukuelewa ulichoandika, lakini naona bado kina ukakasi. Kwanza umetumia vibaya jina la Yesu, kiufupi umedhalilisha dini ya wengine (Ukristo). Pia, lazima uelewe, kila Taifa, lipo responsible kulinda usalama wa raia wake. Tahadhari zinazotolewa, za ugaidi au magonjwa ni muhimu kwao, labda tu kama wamekosea protokali za kidiplomasia, katika kuwapa ujumbe raia wao, of which, sio sababu ya msingi ya kuingia katika vita. May be unaweza kujiuliza, katika suala la Ebola, nani anafaidika zaidi, Tz kukataa uwepo wake au wageni kulazimisha kupata taarifa muhimu kuhusu ugonjwa huo...??
Pia, Tz ina shida nyingi sana, umasikini, magonjwa, maji duni, elimu duni, miundombinu duni, nishati duni, siasa duni, uongozi duni,uchumi duni, yaan kila kitu kwetu ni duni. Tujiimarishe katika hayo, kwa maana yanawezekana katika mazingira haya ya amani, ya ndani na hata ya nje. Kama tumeshindwa kujisimamia vyema na kujiendesha kwa maslahi mapana ya Taifa, wakati huu wa amani, unadhani itawezekana, kwa wakayi huo wa vita...??
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…