Fukuza Marekani nchini

Kabla ya kufanya hivyo ujipange. Una sasa mwenyekiti wako analia kila siku Zimbabwe iondolewe vikwazo mpaka sasa Hawana hela yao wanatibiwa SA na nchi jirani. Sasa kwa wewe hapa Tz Anza na wagknjwa wanaopata ARV wapatao 2m plus wanaopata dawa bila kukata for 5 years kata uone msipo tanga a janga la kitaifa mpaka viongozi wenu.
 
haya wafukuzeni!!
 
marekani itabak kuwa juu kwa kiherehere cha viongoz wako. mbna misaa ya USA husemi huitak, na kaa ukujua dunia ya 3 bila msaada toka dumia ya 1 wamekwisha..
The one who feeds u controls u...
Msaada gani wanaoutoa kwetu? Acheni uzushi!
 
Naukubaliana na wewe. Nina waogopa sana watanzania. Watanzani wa leo wako tayari kutusaliti kirahisi tu.

Nina wasi wasi na Rais wetu. Anamtindo wa kuwang'ang'ania dazu ambao yeye anajua fika kuwa ni Wasaliti kama Makamba Junior.
 
Kichaa kimekuanza lini? Ni mara ya kwanza au umewahi kuugua siku za nyuma pia?
 
Ni sawa useme ung'oe kizazi kwa mwanamke ili kukwepa maumivu ya hedhi.ni ujuha.
Kwa Diplomasia tutakaa nao sawa
 
Haya kumbukeni PKagame ni mtu wao Mabeberu
 
Kitu unachotakiwa kujua katika dunia hii ya sasa ni kwamba hakuna kitu sirini unachoweza kukifanya mmarekani asiwe na taarifa, kwanza lazima ufahamu kuwa ndani ya serikali kuna pandikizi za wamarekani wanalipwa kwa kazi hiyo sasa wao kutoa tamko hawakurupuki hata video ya matukio yanayofanyika mkijua hamna aliyeona au mwingine anayejua basi ujue wao wanazo, wakati mwingine hapo waliongea kwa mafumbo huelewi wameongea nini kwa undani, kuhusu Ujambazi na uporaji nenda extra mile ndio utaelewa hilo.
 
Msaada gani wanaoutoa kwetu? Acheni uzushi!
Hizo ARV unatoa wewe? Na zile barabara kama ile ya Tunduma- Sumbawanga-Katavi, hela walitoa ukoo wako? Na ule umeme uliounganishwa zaidi ya vijiji 5,000 hela walitoa mizimu ya kwenu? Na hizo hela mnazopewa na kukopa WB, huko WB waliweka familia yako? Wasingeweka hao mabeberu mngekopa nini? Hata huko African Bank unajua hela nyingi ni ya nani? Au unadhani ni ya nchi za Africa? Kweli aheri ulemavu wa viungo kuliko kukosa uelewa.

Hakuna nchi hata moja iliyowahi kufanikiwa kwa kugombana na hao wakubwa ikafanikiwa. Wachina walirukaruka, wakaishia kuvaa nguo zenye viraka matakoni na magotini lakini hakuna kilichoeleweka. Wakasalimu amri, mabeberu wakaenda kuwekeza China, ukuaji wa uchumi wa China ukawa unaongoza Duniani. Mpaka leo, makampuni makubwa kabisa 10 nchini China, kampuni ya China ni moja tu. Mengine yote ya mabeberu. Na sahizi Trump anaitesa China, mpaka ukuaji wa uchumi wa China umeshuka. Na baadhi ya makampuni yameridhia kupunguza uwekezaji wake nchini China.

Kuna wakati mbwa anaweza kubweka na hata kumwuma anayemtunza. Lakini anayemtunza anaweza kummaliza wakati wowote akitaka.

Simu hiyo huwezi hata kuitumia Marekani asipotaka. Hata kagari kako huwezi hata kuwa nako, kama mabeberu wangesema tusiuziwe. Dhahabu yako na almasi vinaweza kuwa kokoto na mchanga usio na maana kama hayo mataifa makubwa yakisema hairuhusiwi kununua madini ya Tanzania.

Tanzania haiwezi kuwepo bila ya mataifa makubwa lakini mataifa makubwa yataendelea kuwepo hata bila ya uwepo wa Tanzania. Somalia leo hakuna Taifa. Nchi gani kubwa imeathirika?
 
Mbona povu sana bro kwani mnyamwezi akionya raia wake wewe inakuwasha nini.au ebola imetia timu nini naanza kuwa na mashaka makubwa
 
Waambie hao. Hata Nyerere alitaifisha Mwadui, kilichomkuta nadhani kinajulikana, Almas ya Tanzania ilisusiwa na hata vipuri vya mgodi hawakuuziwa mpaka Mwadui ikafa
 
Waandishi wao wamebanwa sasa hivi wameamua kuingia kazini wenyewe kuchapisha propaganda za kihuni
 

Mkuu IKWETA KONZO huyu Robert Heriel ni mwandishi mwenye credibility kweli?
Ashakum mkuu lakini naona kama haya maoni yamejaa assumptions, fantasies na wishful thinking za kitoto.
Marekani ni taifa lenye umri wa karibu nusu ya kikwe(millenia) na kwa zaidi ya karne tatu wakiiongoza dunia kwa innovations za sayansi na teknolojia.
Je, ni option yenye tija kuanza kupambana nao kwa ajili ya hisia zetu kuwa hawatutendei haki hata kama hizi hisia zinaibuliwa tu na tafsri potofu za habari zinazowahusu zaidi wao wenyewe na wananchi wao?
Yaani kuwaonya wananchi wao wanaosafiri sehemu mbalimbali duniani kuhusu uwepo wa elements hatarishi ndio na sisi tujibu mapigo kwa kuwafukuza? Alafu unamfukuza nani anyway, balozi, wawekezaji, mashirika ya misaada au watalii? Na kwa faida gani?
Hebu tuachane na irrational thinking au ndoto za mchana au ulevi au vyote.
P S. Ningependa kujua maana ya hilo neno ‘Taikon’ mkuu. Na suspect limetoholewa kutoka lugha ya ‘mabeberu’!
 
Ameandika kwa hisia hasi ajui chochote nadharia ya uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…