Uchaguzi 2020 Fujo kwenye mikutano ya kampeni ni vitendo vya kukemea

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,444
2,000
Nimekua nikifuatilia kampeni tangu zianze. Niseme kwamba kampeni za mwaka huu zinautulivu kuliko kampeni za 2015.
Kuna vitu vichache ambavyo vinahitaji kukemewa.

Kitendo cha mtu kuzomea, kuzuia, ama kufanya fujo kwenye mkutano wa kampeni si cha kufumbiwa macho na kiongozi yeyote awe wa kisiasa, wa kidini ama wa kijamii.

Nimeona Matukio yakifanywa na watu kadhaa katika hizi harakati za kisiasa za uchaguzi ambayo sio mazuri Wala hayana umuhimu.

Nitoe mifano michache.

1. Lissu akiwa Hai alizomewa na vijana na hata mmoja wa hao vijana kuhatarisha maisha.

2. Magufuli akiwa Bukoba wamesimama vijana wakidai hawamtaki. Huku wafuasi wake eneo lile walikuwa wamefurika kuliko kawadia

Matukio kama haya yanaeweza kuleta maafa makubwa sana.

Nitashangaa iwapo viongozi wetu wa kisiasa wataendelea kushangilia matukio ya aina hii.

Ukiona mgombea anamwaga sera mpinge kwa sera kwenye mkutano wako. Mtu akiwa na wafuasi wake anakuwa na ulinzi mkali kuliko hata ulinzi wa jeshi lenye mizinga.

Chonde chonde, tuache mara moja.

Nawatakia uchaguzi mwema.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
2,358
2,000
Hiyo ya Magufuli kuzomewa hata siamini, Kuna hata ka'clip' tuone uongo wako? 🤔🤔🤔
Aaah wapi, ni uzushi tu wa mitandaoni, na Baadhi ya watu walitegemea kusingelitokea mwitikio mkubwa kama huo na Baadhi yao kutegamea kwamba atazomewa tu kulingana na ukweli wa Magufuli kuwaambia Yeye hakuleta tetemeko bukoba

Sasa la kutokuitikia watu wengi lilishindikana, watu wakajaa Ile nyomi kuliko kawaida, Mitandao ikazusha tu kuwa kumetokea zomeazomea, wakati hakuna kitu kama hicho.

Magufuli anakubalika mpaka Kwa wapingaji wake, wanampiga midomoni tu, na siku ya uchaguzi watampa Kura, hii ni Hadi Kwa M/kiti wa Chama kileee atampa Kura Magu.

Amini nakuambia
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,219
2,000
Nimekua nikifuatilia kampeni tangu zianze. Niseme kwamba kampeni za mwaka huu zinautulivu kuliko kampeni za 2015.
Kuna vitu vichache ambavyo vinahitaji kukemewa...
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Hai na Kagera , Hai kulikuwa na kikosi kimeandaliwa kumdhuru Lissu na Mbowe ambacho kiliandaliwa na DC , Kagera wananchi wameulizwa kama watamchagua Magufuli wakasema hawatamchagua , jambo ambalo ni la kidemokrasia tu
 

REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,996
2,000
Nimekua nikifuatilia kampeni tangu zianze. Niseme kwamba kampeni za mwaka huu zinautulivu kuliko kampeni za 2015. Kuna vitu vichache ambavyo vinahitaji kukemewa...
Acheni kutafuta huruma nyie ficcm wananchi wanaonyesha hisia zao na reaction nyie mnasema fujo.

Mnatafuta sababu au siyo? kweli Lissu kawapiga za kende! Mmepoteana.

Hongera wanakagera!
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,444
2,000
Kuna tofauti kubwa sana kati ya Hai na Kagera , Hai kulikuwa na kikosi kimeandaliwa kumdhuru Lissu na Mbowe ambacho kiliandaliwa na DC , Kagera wananchi wameulizwa kama watamchagua Magufuli wakasema hawatamchagua , jambo ambalo ni la kidemokrasia tu
Kila mtu anaweza akatetea upande wake

Kuna watu wanadai jazazomewa.

Democracy huzaa fujo na vifo Kama haijalindwa vizuri.

Mtu anaweza akasema pia kwamba hao walipangwa na CDM ili kuleta machafuko kwenye uchaguzi.

Tuachane na huu upuuzi. Sikiliza Sera pinga kwa Sera.

Wale wafuasi wa Magufuli walio kuwa wamejaa pale walikuwa na uwezi wa kupiga hata kuuwa hao wengine kwa sababu tu ya kuudhiana.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
3,941
2,000
Nimekua nikifuatilia kampeni tangu zianze. Niseme kwamba kampeni za mwaka huu zinautulivu kuliko kampeni za 2015. Kuna vitu vichache ambavyo vinahitaji kukemewa...
Magufuli ndo kaleta ubabe leo kagera. Wewe unawauliza watu watu wamesema hawakupi kura si upotezee tu!

Hivi hata wewe ungekuwa muhaya, kwa yale masimango kwenye suala la tetemeko na kwa kuteswa kwa kabendera na mama yake, leo kwenye lile swali la magufuli ungejibuje? Weka unazi pembeni
 

magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
3,597
2,000
Nimekua nikifuatilia kampeni tangu zianze. Niseme kwamba kampeni za mwaka huu zinautulivu kuliko kampeni za 2015. Kuna vitu vichache ambavyo vinahitaji kukemewa...
Hebu weka video clip tuone sije ikawa ya kutengeneza mbona nilikuwa naangalia live Cjannel 10 sikuona labda ilinipita leta tuone hiyo ya Bukoba!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom