FTA Dish Vs VING'AMUZI Kipi bora?

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,700
Reaction score
4,126
Wana Jf!
Naomba kuuliza hapa kati ya visimbusi vyote na kuwa na dish la free to air kipi bora zaidi?

+-Kuna wengine wanasema ukiwa na fta unaweza pata channel zote mfano za startimes kama B4u,NatGEo n.k

+-Kuna wengine pia wanasema kuwa visimbuzi ni cheap kuliko fta na mengine mengii...

Najua hapa tuna wataalam tofauti tofauti naomba mnisaidie ili sasa nijue kipi ni kipi.

N.B Kauli zisizofaa zitaziruhusu ntazireport kwa Uongozi.

Ahsanteni.
 
kwenye ulimwenge wa Tv

1st = DSTV
2nd = FTA
.
.
.
.
.
.
.
10th = Startimes na wenzake
 
kwenye ulimwenge wa Tv

1st = DSTV
2nd = FTA
.
.
.
.
.
.
.
10th = Startimes na wenzake

Sawa mkuu!nasikia pia kuna channel za dstv zipo fta kama Animal planet?
 
Tafuta dongles au receiver zinaitwa Qsat Q11G hizi zunakula FTA zote na Dstv zikuwemo sasa issue inakuja kama unadish kubwa unafunga lnb hata mbili hizo azamtv,startimes na dstv zote unapata ...vinapatikana hapa bongo
 
Kaka vinapatikana wapi? kama unajua ntakutafuta kiongozi. Manake kwanini nipate shida ya kulipia kwa mwezi huduma zenyewe poor mara no service mara no signal mara oooohhhh huku kwa wazawa channel zao hazikidhi matakwa yangu.....bora nije huko japo dah kwenye nyumba za kupanga kuweka dishi nayo nooooma....dah nchi hiii....tutafika tu! it is the matter of time.
 
Dooh nazitaka hizo mkuu saidia hizo receiver zinapatikana duka gain?
 
Dishi unanunua la 50,000/- futi tatu au 40,000/- futi 2.5 ...haya kwa nyumba ya kupanga hayana shida ni madogo sana...kingamuzi kinauzwa 295,000/- na Fundi wakufunga dishi na installation ni 30,000/-
Wire futi 28 bei 7000/- pale kariakoo na lnb moja ya hd ni 10,000/-
Vingamuzi vipo mtaani vingi na kkoo vingi lkn kkoo utabamizwa 350,000/- ....
Ukitaka ntakuunganisha na fundi kama upo Dar nahisi anaweza kuja kukufanyia installation
 
Sio mtaalam lakini umenifurahisha kwa kutumia neno sahihi 'kisimbuzi' Wataalam wa bakita wametuambia king'amuzi ni sawa na neno la kingereza 'detector'..... 'to decode' ni kusimbua kwa hiyo neno sahihi kwa decoder ndio kisimbuzi. Naomba wandugu sasa tuwache hii neno 'king'amuzi' itulie kwake.
 
Dooh nazitaka hizo mkuu saidia hizo receiver zinapatikana duka gain?

Madukani ni vigumu japo nimesikia kuna kkoo pale wanaziuza sijajua duka mm nimefunga juzi tu ni kuwasiliana na mafundi tu ila angalia asikubamize bei
Kama upo interested Pm me ntakutumia namba zake maana siwez ziweka in public hapa bila ruhusa yake
 
#Ahsante kiongozi #kkimbwembwe kwa maneno yako yenye Hekima.
 
Madukani ni vigumu japo nimesikia kuna kkoo pale wanaziuza sijajua duka mm nimefunga juzi tu ni kuwasiliana na mafundi tu ila angalia asikubamize bei
Kama upo interested Pm me ntakutumia namba zake maana siwez ziweka in public hapa bila ruhusa yake

Poa ngoja nifanye hivyo sasa hivi.
 
Wakuu sisi wa madongo kuinama lini tutavipata hivyo visimbusi mfano singida!
 
Wakuu sisi wa madongo kuinama lini tutavipata hivyo visimbusi mfano singida!

Kaka A.J.K mi nakushauri bora ununue FTA DISH ninaushahidi kuwa visimbuzi vya Tz kikiongozwa na startimes ukiacha Dstv havikidhi matakwa na mahitaji mengi ya baadhi ya watz hasa walio mjini zaidi.So ukiweza bora nunua FTA DISH kama ninavyojipanga mimi sasahivi.
 
mbona mimi nina FTA dish ila ninapata channel za ipp tu pamoja na za Msumbiji tu, shida ni nini?
 
FTA siku hizi inasumbua sana sijui zinahujumiwa au!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…