From a painful heart... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

From a painful heart...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, May 6, 2012.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nikaa nikatafakari, nikaona kama vile nakata tamaa na maisha ya Tanzania...nimekua nikijiuliza hivi ni kweli hawa marais wanaochaguliwa huwa hawajui undani wa timu wanazozichagua kushirikiana nao katika uongozi? Katika kila Rais aliyepita ni lazima tuwe na manung'uniko, ni kwa nini? Hivi kweli kwa mwendo huu tutaweza kujiondoa kwenye hili wimbi la umaskini?
  Huyu Kikwete tuliyenaye kwa sasa (walau nisirudi nyuma sana kwa Mkapa na Mwinyi) alishapata funzo kipindi cha Lowasa alipojiuzulu...inamaana hakutafuta undani wa hao aliowateua mpaka tukafikia hapa ambapo imebidi avunje baraza lake la mawaziri kwa mara ya pili? Ni kwa nini Marais wetu wanafanya mzaha kwenye hii nchi yetu? Inaumiza sana...Ukweli ni kwamba, hatutapata maendeleo kama kila waziri anayeingia kwenye wizara anakaa miaka miwili then anaondolewa. Huwezi kua na maendeleo kwa style hiyo. Ina maana sera na utaratibu ulioanzishwa na waziri aliyepita kama ulikua mbovu, waziri mpya anaubadilisha...sasa hao watendaji waliopo chini wata adopt changes ngapi ili waweze kuwa productive.
  Nafikiri sasa wakati umefika Marais wawe serious na kuacha ushikaji. Marais watambue kwamba wanatuangamiza sisi rais tulio chini. Wao wanajuana na wanaweza kucheza kwa kupokezana nafasi kama wanavyotaka, lakini mwisho wa siku tunaoumia ni sisi raia wa kawaida.
  Jamani, mh. Kikwete na marais mtakofuata, acheni utaratibu wa kujaribu...chagueni watu kwa kujua undani wao...vinginevyo mtatuingiza kwenye janga lisilotakiwa. Naweza kusema kwamba, marais mnaochaguliwa hamko serious na mnaingia serikalini bila kujipanga...kwa mawazo yangu, rais yeyote anayegombea, lazima awe na timu yake ya uongozi kichwani na lazima aiamini hiyo timu na awe tayari kuchukua hatua pale ambapo anaona mmoja wa timu haendani kulingana na matakwa ya uongozi. Lakini kwa Tanzania kuwajibishana imekua tatizo...
  Tutabadilisha mawaziri mara ngapi? Kwa mimi kama ningekua Rais ningewaamuru mawaziri wote ambao wamevuliwa uongozi kutokana na ubadhilifu warudishe mishahara yote waliyopokea tokea 2010 kama walikuwepo... Hii ni kutokana na kwamba hawaja deliver kulingana na job description, so they deserve that punishment. Tukienda kwa utaratibu huu, mawaziri watakua serious. Inauma sana una walipa mawaziri kwa kutumia kodi za wananchi, halafu mwisho wa siku wanaboronga, unawatoa uwaziri bila hatua za ziada, na wanaendelea kula posho ya ubunge. This is insane!


  AAAAaaaaaa ahhhhhhhhhh, inauma......
   
Loading...